2020.12.04 Bodi ya EBU 2020.12.04 Bodi ya EBU 

Ebu:wajumbe tisa watendaji wamechaguliwa kwa kipindi cha miaka miwili 2021-22

Kwenye bodi hiyo pia kuna naibu mkurugenzi wa Idara ya Masuala makuu ya Kitengo cha Baraza la Kipapa la Mawasiliano,Giacomo Ghisani,kama mwakilishi wa kisheria wa Redio Vatican.Ebu inatimiza miaka 70 mwaka huu ambayo inaleta pamoja watangazaji wakuu wa huduma za umma barani Ulaya na ulimwenguni kote.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumuiya ya Utangazaji Ulaya ambayo ni chama kikubwa zaidi ulimwenguni cha vyombo vya habari katika huduma kwa umma, kimefanya upyaisho wa  bodi kuu ambayo katika miaka miwili ijayo itakuwa karibu na rais mpya Delphine Ernotte Cunci wa Televisheni ya Ufaransa na makamu rais Petr Dvořák wa Televisheni ya Czech katika usukani.

Viongozi wapya

Miongoni mwa wajumbe  hao tisa, ni naibu mkurugenzi wa Idara ya Masuala Makuu ya Kitengo Usimamizi, katika Baraza letu la Mawasiliano,  Giacomo Ghisani, aliyethibitishwa kuendelea kwa muhula wa pili kama mwakilishi wa kisheria wa Radio Vatican. Na katika uthibitisho wake kufuatana na uchaguzi huo ametoa maoni yake kwamba :"Ninaamini kuwa uamuzi huu ni kutambua kazi iliyofanywa na Radio ya Vatican, ambayo ni mwanachama mwanzilishi wa EBU”, na “kwamba kwa matangazo yake inatambua kutimiza utumishi wa kweli wa umma kwa niaba ya jamuiya na wema wa pamoja katika kipindi hiki cha janga ni muhimu sana.”

Wengine, waliochaguliwa na mkutano mkuu wa 85 wa EBU, ni Thomas Bellut, mkurugenzi mkuu wa ZDF (Ujerumani), Cilla Benkö, mkurugenzi mkuu wa SR (Sweden), Marcello Foa rais wa Rai, Monika Garbačiauskaitė-Budrienė, wa LRT (Lithuania), Sebastian Sergei Parker, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Channel One (Urusi ). Gonçalo Reis, rais na Mkurugenzi Mtendaji wa RTP (Ureno), Fran Unsworth, Mkurugenzi wa Mambo ya Sasa wa BBC na na Alexander Wrabetz, meneja mkuu wa ORF ya Austria.

Uwezo na uzoefu wa kudumisha msimamo kijiografia

Kwa mujibu wa maoni ya rais Ernotte Cunci kufuatia na uchaguzi huo amesema "Nimefurahia kuweza kuunganisha pamoja namna hii  idadi kubwa ya ujuzi na uzoefu na kuweza kudumisha msimamo  wa tofauti za kijiografia, kiuchumi na kiutamaduni wa wajumbe  wa EBU katika muundo wa Bodi mpya ya Wakurugenzi”,na kuongeza kusema:"Kwa mara ya kwanza, najivunia pia kujumuisha wanawake 3 kwenye bodi ya wakurugenzi." Bodi mpya itaanza kazi mnamo Januari 1, 2021 na itamaliza muda wake mwishoni mwa Desemba 2022.

EBU inawafikia watu bilioni 1 ulimwenguni

Sehemu ya EBU  kwa sasa katika hatua yake ya miaka 70 na chama kikubwa zaidi cha  huduma ya umma ulimwenguni (PSM): Kinahesabu masafa 115 katika nchi 56, na washirika wengine 34 wa bara la Asia, Afrika, Australia na Amerika. Umma inayofuatilia programu za EBU inazidi watu bilioni moja ulimwenguni, na matangazo katika lugha zaidi ya 160. Radio Vatican, kama ilivyotajwa, imekuwa ni mwanachama mwanzilishi tangu 1950.

04 December 2020, 17:02