Balozi Carlos Antonio Cordero Suarez wa Honduras, tarehe 19 Desemba 2020 amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Balozi Carlos Antonio Cordero Suarez wa Honduras, tarehe 19 Desemba 2020 amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. 

Papa Apokea Hati za Utambulisho Kutoka kwa Balozi wa Honduras!

Balozi Carlos Antonio Cordero Suarez alizaliwa kunako tarehe 30 Julai 1948. Ameoa na kubahatika kupata watoto sita. Amebahatika kupata shahada ya uzamivu kwenye masuala ya kemia kunako mwaka 1973. Ni mtaalam wa masuala ya uchumi wa kampuni na kubahatika kuwa Kamanda wa Vikosi vya Zimamoto. Amewahi pia kuwa ni Mkurugenzi mkuu wa Duka la dawa la Corval.

 

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 19 Desemba 2020 amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Carlos Antonio Cordero Suarez, Balozi mpya wa Honduras mjini Vatican. Balozi Carlos Antonio Cordero Suarez alizaliwa kunako tarehe 30 Julai 1948. Ameoa na kubahatika kupata watoto sita. Amebahatika kupata shahada ya uzamivu kwenye masuala ya kemia kunako mwaka 1973. Ni mtaalam wa masuala ya uchumi wa kampuni na kubahatika kuwa Kamanda wa Vikosi vya Zimamoto. Kati ya mwaka 1974 hadi mwaka 1984 alikuwa ni Mkurugenzi mkuu wa Duka la dawa la Corval.

Kati ya mwaka 1985 hadi mwaka 1991 aliteuliwa kuwa ni Mkurugenzi mtendaji wa miradi ya maendeleo iliyokuwa inatekelezwa na Consulpane-Secplan. Kati ya mwaka 1991 hadi mwaka 1993 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya dharura kwenye Tume ya Kudumu ya COPECO. Kati ya mwaka 1993 hadi mwaka 2002 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Maendeleo Kisiwani Baia. Kati ya Mwaka 2003 hadi mwaka 2010 aliteuliwa kuwa Kamanda wa Vikosi vya Zimamoto. Kati ya mwaka 2011 hadi mwaka 2012 alichaguliwa kuwa Mshauri wa Rais. Kati ya mwaka 2012 hadi mwaka 2020 aliteuliwa kuwa Kamishna Msaidizi wa Tume ya Masuala ya Dharura, COPECO. Na tarehe 19 Desemba 2020 amewasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican.

Honduras

 

19 December 2020, 14:52