2020.07.02 Aif Mamlaka ya Usimamizi wa habari za Kifedha 2020.07.02 Aif Mamlaka ya Usimamizi wa habari za Kifedha  

AIF inageuka kuwa ASIF,muundo mpya wa Mamlaka ya Habari za Fedha

Papa ameridhia kwa maandishi yake Sheria mpya ya Mamlaka ya Habari za Fedha, ambayo tangu leo na kuendelea itaitwa Mamlaka ya Usimamizi na Habari ya Fedha(ASIF).Katika mahojiano na vyombo vya habari Vatican,Rais wake Carmelo Barbagallo ameonesha maana mpya ya sheria hiyo ambayo imeanza kufanya kazi leo kuwa inachangia umahiri fulani wa ndani

VATICAN NEWS

Katika mageuzi kwa ujumla kwa matashi ya Papa Francisko kwa ajili ya Vatican na Serikali ya Mji wa Vatican, inayolenga uwazi zaidi na uimarishaji wa udhibiti katika uwanja wa uchumi -kifedha, Baba Mtakatifu ameidhinisha Sheria mpya ya Mamlaka ya habari ya Fedha ambayo tangu tarehe ya leo, itaitwa kwa jina Mamlaka ya Usimamizi na Habari ya Fedha (ASIF). Marekebisho hayo yalikuwa ya lazima ili kuleta Mkataba huo kulingana na majukumu yaliyopewa, kwa kuongeza kazi ya asili ya ujasusi wa kifedha na kukabiliana na ufisadi wa fedha na ufadhili wa kigaidi. Hii ni mamlaka ambayo inafanya kazi tangu 2013 hata katika shughuli za usimamizi wa IOR, na kuanzisha mabadiliko makubwa ya shirika.

Kwa mujibu wa Rais wake Carmelo Barbagallo ameonesha maana mpya ya sheria hiyo ambayo imeanza kufanya kazi leo kwamba inachangia umahiri fulani wa ndani. Kwa kuongezea jina jipya, kati ya ubunifu mpya msingi kuna upyaisho wa ugawaji  wa majukumu kati ya Urais na Menejimenti, katika hali ya kimkakati kutoka  ile ya zamani, na ambayo sasa inayolenga kuleta ufanisi wa utendaji na mafanikio zaidi kwa hii ya mwisho na vile vile kuanzishwa kwa kitengo kipya, kilichopewa  jina la “Udhibiti na Masuala ya Sheria”.

05 December 2020, 15:21