2020.10.21 Heshima ya Udaktari wa Bartolomeo I 2020.10.21 Heshima ya Udaktari wa Bartolomeo I 

Patriaki Bartholomew I atunukiwa heshima ya Udaktari katika falsafa ya Laudato si!

Ndiyo Heshima aliyopewa Patriaki wa Kiekumene na Mkuu wa Kiorthodox katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Antoniaum wakati wa uzinduzi wa mwaka wa masomo.Katika hotuba yake, Kardinali Parolin amethibitisha kuwa katika suala la utunzaji wa kazi ya uumbaji,magisterium ya Papa Francisko isingeweza kupata kumbu kumbu iliyo bora zaidi ya hiyo kutokana na kiongozi huyo kuwa mstari wa mbele katika kushughulikia mada hiyo tangu katikati ya miaka ya 90.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 19 Oktoba 2020 siku moja kabla ya mkutano katika uwanja wa Campidoglio Roma kati ya viongozi wa dunia kuombea amani, ambapo miongoni mwao ameshiriki Papa Francisko, katika fursa mpya ya uekumene na ushirikishano, alikadhiwa Heshima ya Udaktari katika falsafa ya Laudato si, Patriaki wa kiekumene Bartholomew I. Aliyeongoza  afla  hiyo ya kukabidhiwa  tuzo hiyo alikuwa ni  katibu wa wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin ambaye amesema kwamba kama Mkuu wa Kanisa la Constantinople ameonesha kwa dhati maelewano na Shughui ya Kuhani Mkuu ambayo inajionyesha ule umoja wa kiekumene kati ya Makanisa ya Mashariki na Magharibi. Aliyekabidhi mikononi mwa Patriaki alikuwa ni Kansela wa Chuo Kikuu hicho Padre Michael Anthony Perry.

Katika hotuba yake, Kardinali Parolin amethibitisha aidha kuwa kuhusu utunzaji wa kazi ya uumbaji, magisterium ya Papa Francisko isingeweza kupata kumbukumbu iliyo bora na salama namna hiyo kwa ajili ya  Patriki Bartholomew I, ambaye amekuwa mstari wa mbele kushughulika na mada hii tangu katikati ya miaka ya 90. Kujitoa kwa muda mrefu kwa Mchungaji wa Kiekumene wa Konstantinople katika utunzaji wa kazi ya uumbaji ilikuwa chanzo cha msukumo kwa Baba Mtakatifu Francisko ambaye amemnukuu moja kwa moja akikumbuka hata saini ya pamoja huko Nchi Takatifu kunako 2014 kuhusu wito wao wa pamoja kwa ajili ya umoja wa kikristo na kwa ajili ya kutunza kazi ya uumbaji hadi kufikia waraka  katika fursa ya Siku ya Kazi ya Uumbaji ulimweguni iliyotiwa saini na Papa Francisko kunako tarehe 7 Agosti 2015, aidha na  sala ya kiekumene ya terehe 1 Septemba ya kila mwaka. Kadinali, ameendelea  akiangazia jinsi Papa Francisko na Laudato si, alivyoongozwa na baadhi ya  maandishi ya Patriaki na  ambayo yanabainisha uhusiano wa karibu kati ya uchumi na ekolojia, na ambayo yote inatokana na mzizi wa pamoja yaani wa nyumba.

Kabla ya kupokea utambulisho huo kutoka mikononi  mwa Fra 'Michael Anthony Perry, Padre Mfransiskani wa Ndugu  wadogo na Kansela Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Antoniaum, zimetolewa salamu za makadinali wengine waliokuwepo kwa niaba ya Papa wakizielekeza kwa Patriaki Bartholomew I.  Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Wakristo, amesisitiza jinsi makanisa ya Roma na Constantinople yalivyo kama Maanisa dada na kukumbusha juu ya maelewano kati ya Patriaki na  Papa na ambayo yalionesha tayari katika Misa ya kuanza kwa utume wa Upapa kwani Patriaki Bartholomew I alipendelea kuwepo.

Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungamani ya Binadamu  kwa upande wake  amekumbusha  jinsi roho ya Kiorthodox, kuwa kila uovu una sababu ya kiroho na kila shida ina asili ya dhambi na kwamba  “Ikiwa mwanadamu atagundua tena wito wake wa zamani kama mlinzi wa bustani, basi mgogoro utakuwa umesuluhishwa”.

21 October 2020, 16:57