Ufafanuzi wa Rehema Kamili Mwezi Novemba mwaka huu kwa mujibu wa Idara ya Toba ya Kitume Ufafanuzi wa Rehema Kamili Mwezi Novemba mwaka huu kwa mujibu wa Idara ya Toba ya Kitume 

Idara ya Toba ya Kitume:Hati Kuhusu Rehema Kamili mwezi Novemba

Katika kumbukumbu za marehemu kwa mwezi Novemba mwaka huu lazima zifuate mantiki ya dharura ya kiafya inayohusishwa na janga.Kwa maana hiyo Idara ya Toba ya Kitume imetoa hati iliyosainiwa na Mhudumu Mkuu wa idara hiyo Kardinali Piacenza, kuhusiana na kuongeza muda wa msamaha kwa Novemba kwa waamini waliofariki kutokana na mabadiliko na masharti ili kuhakikisha usalama wa waamini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa agizo la Papa, ili kuepusha mikusanyiko, Idara ya Toba ya Kitume imaamua  kwamba msamaha kamili kwa wale wote wanaotembelea makaburi  kuwaombea wafu hata ikiwa ni kwa kimawazo, ambayo kwa kawaida huwekwa tu kwa siku binafsi kuanzia tarehe 1 hadi 8 Novemba, kwa sasa inaweza kuhamishiwa kwa siku nyingine za mwezi huo huo, hadi mwisho wake. Siku hizo, zilizochaguliwa kwa hiari na mwamini binafsi, zinaweza pia kutenganishwa  kulingana na kila mmoja. Msamaha kamili  wa dhambi  wa tarehe 2 Novemba, ulioanzishwa katika fursa ya kuwakumbuka waamini marehumu wote kwa wale ambao kwa uaminifu hutembelea Kanisa au sehemu nyingine ya ibada  ili  wasali sala ya Baba yetu na kanuni ya Imani, wanaweza kuhamishiwa sio tu kwa siku ya Jumapili iliyotangulia au inayofuata au kwa siku ya sherehe ya Watakatifu Wote, lakini pia siku nyingine ya mwezi Novemba, kwa hiari binafsi.

Kwa kuongezea, aidha wamesema wazee, wagonjwa na wale wote ambao kwa sababu kubwa hawawezi kutoka nyumbani  pia kwa sababu ya masharti ya Mamlaka ya kiafya, wataweza kupata rehema kamili ikiwa tu, wataungana kiroho na waamini wengine wote,  hasa kwa kujitenga na dhambi na nia ya kupokee Sakramenti ya Upatanisho, ushiriki wa Ekaristi na sala kwa ajili ya nia za Baba Mtakatifu, mbele ya picha ya Yesu au ya Bikira Maria;  Vile vile wasali  sala kwa ajili ya wafu, kwa mfano Masifu ya asubuhi na jioni ya Ofisi ya Wafu, Rozari ya Maria, na ya Huruma ya Mungu, sala nyingine kwa ajili ya marehemu  walipendwa wao  au kujikita kwa upendo zaidi  katika usomaji wa kutafakari wa kifungu kimoja cha Injili kilichopendekezwa na liturujia ya wafu, au kutimiza kazi ya huruma  kwa kuitoa kwa  Mungu kwa  uchungu na usumbufu wa maisha waliotangulia mbele ya haki.

Idara ya Toba ya Kitume hatimaye inaomba makuhani wenye vitivo vinavyofaa  kujitoa kwa ukarimu hasa kwa kuadhimisha sakramenti ya Kitubio na kutoa Komunyo Takatifu kwa wagonjwa. Na, kwa kuwa roho zilozko  Purgatori zinasaidiwa na maombezi ya waamini hasa kwa sadaka  ya altareni inayompendeza Mungu, makuhani wote wanaalikwa kwa uchangamfu kusherehekea Misa Takatifu mara tatu siku ya kumbukumbu ya waamini wote waliotutuka. Hata hivyo ni lazima kukumbuka kwamba Kanisa linafundisha kuwa Rehema kamili ni msamaha mbele ya Mwenyezi Mungu kwa adhabu za muda kwa ajili ya dhambi ambazo kosa lao limekwishafutwa, msamaha ambao Mkristo mwamini aliyejiweka vizuri huupata baada ya kutimiza masharti yaliyotolewa na Mama Kanisa, kwa tendo la Kanisa ambalo likiwa ni mgawaji wa ukombozi hutumia kwa mamlaka yake hazina ya malipizi ya Kristo Yesu na ya watakatifu wake. 

23 October 2020, 17:17