Vatican News
Umuhimu wa kurudi katika liturujia ya kawaida na kushiriki ekaristi kwa wakristo ni muhimu hasa mahali ambapo kanuni za sheria ya janga zinaruhusu Umuhimu wa kurudi katika liturujia ya kawaida na kushiriki ekaristi kwa wakristo ni muhimu hasa mahali ambapo kanuni za sheria ya janga zinaruhusu 

Misa ya mitandaoni haiwezi kuondoa ushiriki binafsi katika Kanisa!

Katika barua iliyotolewa kwa ajili ya Marais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki,Kardinali Sarah anathibitisha hitaji la kurudi katika hali ya kawaida ya maisha ya Kikristo,ambapo dharura ya kiafya inayosababishwa na janga inaruhusu.Waraka unasisitiza kuwa kuhudhuria Misa kupitia vyombo vya habari hauwezi kulinganishwa na ushiriki halisi binafsi kanisani.

VATICAN NEWS

Ni muhimu kurudi katika hali ya kawaida ya maisha ya Kikristo na uwepo kimwili kwenye Misa, ambapo hali inaruhusu: hakuna maambukizi yanayolinganishwa na ushiriki binafsi au yanaweza kuchukua nafasi yake. Hivi ndivyo Kardinali Robert Sarah, Rais wa Baraza la Kipapa la Ibada na nidhamu ya Sakramenti anathibitisha, katika Barua kuhusu maadhimisho ya liturujia wakati na baada ya janga la Covid 19, yenye kauli mbiu “Turudi katika Ekaristi kwa furaha”. Waraka huu umeelekezwa kwa marais wa Mabaraza ya Maaskofu wa Kanisa  Katoliki, ambayo imeidhinishwa na Papa Francisko tarehe 3 Septemba iliyopita.

Ukuu wa jumuiya ya maisha ya Kikristo

Janga kwa sababu ya virusi vya Covid 19 - limeweka machafuko na siyo tu katika mienendo ya kijamii na familia, lakini pia katika maisha ya jamuiya ya Kikristo, ikiwa ni pamoja na mwelekeo wa kiliturujia. Kardinali Sarah anakumbusha kwamba ukuu wa jumuiya una maana ya kitaalimungu kwamba  Mungu ndiye uhusiano wa Watu katika Utatu Mtakatifu na anajiweka katika uhusiano na mwanamume na mwanamke na huwaita kuwa na uhusiano naye. Kwa maana hiyo, wakati wapagani walikuwa wakijenga mahekalu yaliyowekwa wakfu wa muuungu mmoja tu  kwani  hapakuwapo na watu, kwa upande wa Wakristo, mara tu walipoweza kupata  uhuru wa kuabudu, mara moja walijenga maeneo ambayo yalikuwa “domus Dei et domus ecclesiae’, yaani  nyumba ya Mungu na nyumba ya Kanisa ambamo waamini wangeweza kujitambua kama jamuiya ya Mungu . Kwa sababu hii nyumba ya Bwana inafikiriwa kuwa uwepo wa familia ya watoto wa Mungu.

Ushirikiano wa Kanisa na mamlaka ya serikali

Jumuiya ya Kikristo haijawahi kutengwa katika karantini na haijawahi kufanya Kanisa kuwa jiji lenye milango iliyofungwa. Kanisa ambalo limeundwa kwa thamani ya maisha ya jumuiya na katika kutafuta wema wa wote, Wakristo kila wakati wamekuwa wakitafuta kuingizwa katika jamii. Hata wakati wa dharura ya janga, hali kubwa ya uwajibikaji wa kusikiliza na kushirikiana na viongozi wa serikali na wataalam, iliibuka na  Maaskofu walikuwa tayari kuchukua maamuzi magumu na ya uchungu, hadi kusimamishwa kwa muda mrefu wa ushiriki wa waamini katika adhimisho la Ekaristi.

Dharura ya kurudi katika hali ya kawaida ya maisha ya Kikristo

Mara tu baada ya hali inaporuhusu, Kardinali Sarah anaendelea na kuthibitisha katika waraka huo  ni muhimu na haraka kurudi katika hali ya kawaida ya maisha ya Kikristo, ambayo ina jengo la Kanisa kama nyumba yake na sherehe za liturujia, hasa Ekaristi, kama kilele cha kuelekea katika hatua ya Kanisa na wakati huo huo chanzo ambacho nguvu zake zote hutoka ndani humo (Sacrosanctum Concilium, 10). Kwa utambuzi wa  ukweli kwamba Mungu hawaachi binadamu aliyowaumba, na kwamba hata majaribu magumu zaidi yanaweza kuzaa matunda ya neema, kwam tumekubali umbali kutoka katika altare ya Bwana kama wakati wa kufunga Ekaristi, muhimu kwa ajili ya kutufanya tugundue tena umuhimu wa maisha, uzuri na thamani isiyo na kipimo. Hata hivyo mapema iwezekanavyo, ni muhimu kurudi katika maadhimisho ya Ekaristi na hamu kubwa iliyoongezeka ya kukutana na Bwana, kuwa naye, kumpokea ili kumleta kwa ndugu na ushuhuda wa maisha yaliyojaa imani, upendo na matumaini .

Umuhimu wa ushiriki binafsi katika Misa

Kardinali Sarah aidha katika waraka huo anasisitiza kwamba, ingawa vyombo vya habari hufanya huduma inayothaminiwa kwa wagonjwa na wale ambao hawawezi kwenda kanisani, na wamefanya huduma kubwa katika kupeleka Misa Takatifu wakati ambapo hapakuwa na uwezekano wa kusherehekea na Jumuiya kimwili, lakini hakuna maambukizi yanayoweza kulinganishwa na ushiriki binafsi au yanaweza kuchukua nafasi yake. Kiukweli, maambukizi haya, peke yake, yana hatari ya kututenganisha na mkutano binafsi na wa karibu na Mungu aliye jifanya mwili, aliyejitoa kwetu na siyo kwa njia ya mitandao, bali  wa kweli, akisema: “Yeyote anayekula mwili wangu na kunywa damu yangu anakaa ndani yangu nami ndani yake”(Yn 6:56). Mawasiliano haya ya mwili na Bwana ni muhimu, na ya lazima, hayabadiliki. Mara tu hatua zinazofaa kutambuliwa na kupitishwa ili kupunguza maambukizi ya virusi, ni muhimu kwamba kila mtu aanze tena nafasi yake katika mkutano wa ndugu kuwatia moyo wale waliovunjika moyo, wanaogopa, wasiokuwepo au wanaosumbuliwa kwa muda mrefu sana.

Mapendekezo ya kurudi kwenye maadhimisho ya Ekaristi

Katika barua hiyo inapendekeza hatua kadhaa za kuhamasisha namna ya kurudi haraka na salama kwenye sherehe za Ekaristi. Kwa kuzingatia uangalifu wa usafi na viwango vya usalama inathibitisha, kuwa haiwezekani  kuzuia ishara na ibada. Kwa kuongezea, inasema wanaamini katika hatua ya busara lakini iliyo thabiti ya Maaskofu ili kushiriki kwa waamini katika maadhimisho ya Ekaristi usielekezwe na mamlaka ya umma hasa katika mikusanyiko. Kanuni za kiliturujia siyo mambo ambayo mamlaka ya kiraia yanaweza kutunga sheria, bali ni mamlaka zinazofaa za Kanisa (taz. Sacrosanctum Concilium, 22).

Kuheshimu kanuni za kiliturujia

Katika barua hiyo inashauri kurahisha ushiriki wa waamini katika madhimisho ya sherehe za liturujia, lakini bila mazaoezi ya kiibada ambayo uboresha na kwa kufuata kikamilifu kanuni zilizomo katika vitabu vya kiliturujia ambavyo vinasimamia shughuli nzima ya ibada na kutambua haki ya kupokea Mwili wa Kristo na kumwabudu Bwana aliye katika Ekaristi kwa waamini kwa njia zinazoonekana, bila mapungufu ambayo huenda hata zaidi ya yale yanayotabiriwa na kanuni za usafi zilizotolewa na mamlaka ya umma au na Maaskofu.

Kanuni ya uhakika: utii kwa maaskofu

Katika mtazamo huo, Kardinali Sarah anatoa maelekezo  sahihi: Kanuni ya uhakika ya kutofanya makosa ni utii. Kutii kanuni za Kanisa, na utii kwa Maaskofu. Wakati wa matatizo (kwa mfano tunafikiria vita, magonjwa ya milipuko) Maaskofu na Mabaraza ya  Maaskofu wanaweza kutoa kanuni za muda ambazo zinapaswa kuzingatiwa. Utii unalinda hazina iliyokabidhiwa kwa Kanisa. Hatua hizi zilizoamriwa na Maaskofu na Mabaraza ya Maaskofu huisha muda wake  tu wakati hali inarudia kuwa ya kawaida.

Afya ya umma na wokovu wa milele

Kwa kuhitimisha Kardinali Sarah anasema “Kanisa  linamlinda mwanadamu katika ujumla wake na kwa wasiwasi wa lazima kwa ajili ya afya ya umma, Kanisa linaunganisha tangazo na msaada wa kusindikiza kuelekea hatua ya  wokovu wa roho ya milele.

WARAKA WA BARAZA LA KIPAPA NIDHAMU

 

 

12 September 2020, 17:39