Vatican News
2020.05.15 Chuo Kikuu cha Kipapa Laterano 2020.05.15 Chuo Kikuu cha Kipapa Laterano 

Barua ya Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki:uhusiano ni kitovu cha watu katika elimu!

Kuna haja ya mwingiliano wa kipekee katika mahusiano licha ya janga,kupitia skrini za kompyuta au unganisho la ulimwengu wa digitali ili kukutana na watu halisi.Hivi ndivyo Baraza la Kiapapa la Elimu Katoliki lnaelezea katika barua yake na kuomba jumuiya za kielimu kushiriki mkataba mpya wa elimu kwa malezi ya vijana na mamlaka yawekeze zaidi katika elimu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Barua ya Baraza la Kipapa la Elimu Katoliki kwa ajili ya shule, vyuo vikuu na taasisi za elimu ikiwa inaongozwa na mada: “Kuweka tena uhusiano katikati na mtu halisi” ambayo imetiwa sahini na Rais wa Baraza hilo Kardinali Giuseppe Versaldi na Katibu wake Askofu Mkuu Angelo Vincenzo Zani. Katika barua hii inaanza na mananeo ya Papa Francisko ya kuwa kuenea kwa Covid-19 ilibadilisha sana uwepo wetu na njia tunayoishi: “Tulijikuta tukiogopa na kupotea”. Kama wanafunzi wa Injili, tulishtushwa na dhoruba isiyotarajiwa na yenye nguvu”. Mbali na shida za kiafya, zipo za kiuchumi na kijamii. Mifumo ya elimu ulimwenguni kote imekumbwa na janga hilo katika viwango vya shule na masomo.  Barua hiyo inasema kuwa kila mahali, juhudi zimefanywa ili kuhakikisha mwitikio wa haraka kupitia majukwaa ya digitali ya kujifunza kwa umbali, ambapo ufanisi hata hivyo umeoneshwa na tofauti kubwa katika fursa za elimu na teknolojia. Kwa mujibu wa baadhi na data nyingine za hivi karibuni zilizotolewa na mashirika ya kimataifa, ni kuwa karibu watoto milioni kumi hawataweza kupata elimu katika miaka ijayo, na kuongeza pengo la elimu lililopo tayari. Katika hili inaongezwa hali mbaya ya shule Katoliki na vyuo vikuu ambavyo, bila msaada wa kiuchumi kutoka kwa serikali, vina hatari ya kufungwa au kupunguzwa nguvu kabisa. Lakini hata hivyo katika kesi hii, taasisi za elimu Kikatoliki (shule na vyuo vikuu) vimeweza navyo kuwa na wasiwasi wa kielimu na kujikita katika huduma ya jumuiya ya kikanisa na jamii ya raia, kwa kuhakikisha huduma ya mafunzo na kiutamaduni wa asili ya umma, kwa faida ya jamuiya nzima.

Elimu na uhusiano

Katika muktadha huu, Barua ya Baraza la Kipapa la Elimu inasema kwa bahati mbaya bado haujadhibitiwa katika sehemu mbali mbali za ulimwengu, kwani changamoto nyingine zimeibuka. Awali ya yote juu ya kujifunza kwa umbali ingawa ni muhimu katika wakati huu mgumu uliokithiri umeonyesha jinsi mazingira ya kielimu yanayoundwa na watu wanaokutana, wakishirikiana moja kwa moja na kibinafsi, haimaanishi tu muktadha wa nyongeza kwa shughuli za kielimu, lakini kiini cha uhusiano huo wa kubadilishana na mazungumzo (kati ya walimu na wanafunzi), ni muhimu kwa malezi ya mtu na kwa uelewa wa muhimu wa ukweli. Katika madarasa, ba maabara kuna makuzi ya pamoja na kujenga utambulisho wa uhusiano. Katika miaka yote ya maisha, lakini hasa katika utoto, ujana na utu uzima, mchakato wa ukuaji wa kisaikolojia na ufundishaji hauwezi kufanyika bila kukutana na wengine na uwepo wa mwingine hutengeneza hali zinazohitajiana, kwa kushamiri kwa ubunifu na ujumuishaji. Katika uwanja wa utafiti wa kisayansi, uchunguzi wa kielimu na, kwa jumla, shughuli za kufundisha, uhusiano kati ya watu unaunda nafasi ambayo katika nidhamu na ufuatiliaji unaibua vigezo vya kiutamaduni msingi ili kufunika hatari za kugawanyika na kutengana kwa maarifa, na vile vile kwa ufunguzi wa maarifa hayo hayo katika nuru ya Ufunuo.

Mafunzo ya walimu

Kuenea na kuendelea kwa janga hilo kwa muda kumeibua hali ya kutokuwa na uhakika hata kwa maprofesa na waalimu. Mchango wao wa maana sana umebadilishwa kwa kina kwa miaka hivi, kutokana na maoni ya kijamii na ya kiufundi ambapo inahitaji kuungwa mkono kupitia muundo thabiti unaoendelea ambao unajua kukidhi mahitaji ya nyakati, bila kupoteza muundo huo kati ya imani, utamaduni na maisha, ambayo ni jiwe kuu la ujumbe wa elimu unaofanywa katika shule Katoliki na vyuo vikuu katoliki. Walimu hubeba majukumu mengi na jitihada lazima kuzidi kuwa hatua halisi, ya ubunifu na ya umoja. Shukrani kwao, roho ya udugu na ushirikishaji haikuzwi tu na wanafunzi, bali pia kati ya vizazi, dini na tamaduni, na vile vile kati ya mwanadamu na mazingira.

Mtu ndiye kitovu

Ili hili liweze kufanyika, uhusiano na mtu halisi na kati ya watu halisi ambao hufanya jamuiya ya elimu lazima iwekwe katikati ya hatua ya kielimu; uhusiano ambao hauwezi kupata nyumba ya kutosha katika mwingiliano uliopatanishwa na skrini au katika unganisho lisilo la kibinafsi la mtandao wa digitali. Mtu halisi na halisi ni roho ya michakato hiyo rasmi na isiyo rasmi ya kielimu, na pia chanzo kisichoisha cha maisha kwa sababu ya asili yake ya uhusiano na jamuiya, ambayo kila wakati inamaanisha nafsi kuu mara mbili (iliyo wazi kwa muungano na Mungu) na usawa (muungano kati ya watu). Elimu ya Katoliki inayoongozwa na maono ya Kikristo ya ukweli katika maneno yake yote, inalenga malezi muhimu ya mtu fungamni amayeitwa kuishi wito maalum kwa njia inayowajibika hasa ya mshikamano na watu wengine. 

Katika ulimwengu ambao kila kitu kina uhusiano wa karibu, tunahisi umoja katika kutafuta kwa mujibu wa elimu ya Kikristo michakato ya kozi mpya za mafunzo ambayo inaturuhusu kukua pamoja kwa kutumia zana za uhusiano ambazo teknolojia ya leo hutupatia, lakini zaidi ya yote kwa kwa kufungua kusikiliza kwa dhati sauti ya yule mwingine, kumpatia muda wakati wa tafakari na upangaji, kuthamini historia binafsi na mipango shirikishi ya pamoja, mafundisho ya historia na hekima ya vizazi vilivyopita. Katika mchakato kama huo wa malezi katika uhusiano na utamaduni wa kukutana, unapata nafasi na thamani hata katika nyumba yetu ya pamoja na viumbe vyote kwani watu, kama vile walivyoundwa katika mantiki ya umoja na mshikamano, tayari wanafanya kazi ili kurudisha utulivu na maelewano na uumbaji na ili kubadaili ulimwengu kama nafasi ya undugu wa kweli (taz. Gaudium et spes, 37). 

Huduma kama hatima ya mwisho

Hali ya sasa imeleta hitaji kubwa la makubaliano ya elimu mabayo daima ni zaidi ya jumuiya na kushirikishana na ambayo inapata nguvu kutoka katika Injili na mafundisho ya Kanisa, kwa maana inachangia katika harambee ya ukarimu na ya wazi kueneza utamaduni halisi wa kukutana. Kwa sababu hiyo, shule Katoliki na vyuo vikuu vinaalikwa kufundisha watu walio tayari kujiweka katika huduma ya jamii. Huduma ya janii kwa hakika tunaweza kufanya uzoefi kuwa ni furaha ya sana ya kutoa kuliko kupokea (Mdo At 20, 35) na kwamba huduma yetu haiwezi tena kuwa wakati wa kutokujali, ubinafsi na mafarakano: Ulimwengu wote unateseka na lazima tujikute tumeungana katika kukabili janga hili, kwani changamoto tunayokabiliana nayo inatuunganisha sisi sote na haina tofauti kwa watu. Huduma yetu haiwezi tena kuwa wakati wa kutojali, ubinafsi na mafarakano: Ulimwengu wote unateseka na lazima tujikute tumeungana katika kukabili janga hili, kwani changamoto tunayokabiliana nayo inatuunganisha sisi sote na haileti tofauti yoyote kwa watu. Malezi ya kutoa huduma katika jamii kwa ajili ya kuhamasisha ustawi wa wote inatoa unatoa wito kwa kila mtu kujiunga na juhudi katika ushirikiano mpana wa kielimu wa kuunda watu wakomavu, wenye uwezo wa kushinda mgawanyiko na tofauti na kujenga upya muundo wa uhusiano wa ubinadamu wa kidugu zaidi.

Kufanya kazi katika mtandao

Ushuhuda ni kwamba janga hilo limeangazia jinsi sisi sote tunavyoathirika na kuunganishwa na linataka haya taasisi za elimu ikiwa ni Katoliki na siziso katoliki kuchangia katika kuunda makakati wa mshikamano wa kielimu ambao, kama harakati za timu, zenye lengo la kupata hatua ya pamoja ya kufufua jitihada kwa ajili vizazi vya vijana vijana, kusasisha shauku ya elimu iliyo wazi zaidi na inayojumuisha, inayoweza kusikiliza kwa kwa uvumilivu, mazungumzo ya kujenga na kuelewana. Hii inaweza kupendelewa na mtandao shirikishi zaidi wa ushirikiano, ambao unaonesha kama sehemu ya kuanzia ili kuweka na kushirikishana malengo kadhaa ya lazima ambayo inawezekana kuungana kwa njia ya ubunifu na halisi wa mifano mbadala ya kuishi pamoja kwa jamii zile zinazosimamiwa na zenye ubinafsi. Hili ni jukumu pana na wazi kwa wale wote ambao wana moyo ujenzi wa mpango mpya wa elimu wa muda mrefu, juu ya msingi wa mahitaji ya kimaadili na sheria shirikishi. Mchango muhimu unaweza kutolewa na huduma chungaji ya shule na vyuo vikuu na pia na Wakristo waliopo katika taasisi zote za elimu.

Hitimisho: katika elimu kuna mbegu ya tumaini la amani na haki

Baraza la Kipapa la Elimu ya Katoliki kama ilivyoonyeshwa tayari katika mazungumzo ya tarehe 14 Mei 2020, inasasisha ukaribu wake na kutoa shukrani za dhati kwa jamuiya zote za elimu, shule za Kikatoliki na vyuo vikuu ambavyo, licha ya dharura ya kiafya, vimehakikisha utekelezaji wa shughuli zao wenyewe ili wasisumbue mlolongo wa elimu ambao si msingi wa maendeleo ya kibinafsi tu, bali pia kwa ajili ya maisha ya kijamii. Katika matarajio mtaala wa shule wa baadaye na upangaji wa masomo, licha ya kutokuwa na uhakika na pia wasiwasi uliopo, viongozi wa jamii wanaalikwa kutoa umuhimu zaidi katika elimu kwa vipimo vyake vyote rasmi na visivyo rasmi, kuratibu juhudi za kusaidia na kuhakikisha, katika wakati huu mgumu, jitihada za elimu kwa wote. Ni wakati wa kutazama mbele kwa ujasiri na matumaini. Taasisi Katoliki zinaye Kristo, njia, ukweli na maisha (taz. Yoh 14: 6), Msingi wao na chanzo cha kudumu cha maji ya uzima (taz. Yn 4: 7-13) ambayE Anaonyesha maana mpya ya kuwepo na kuibadilisha. Kwa njia hiyo, lazima kuamini kwamba katika elimu kuna mbegu ya tumaini: matumaini ya amani na haki.

10 September 2020, 15:50