Vatican News
2020.06.25  - Papa Francisko na Sheikh Mohammed Bin Zayed bin Sultan Al-Nahyan mfalme wa Abu Dhabi 2020.06.25 - Papa Francisko na Sheikh Mohammed Bin Zayed bin Sultan Al-Nahyan mfalme wa Abu Dhabi 

Udugu wa kibinadamu:Tani 50 za msaada kutoka Abu Dhabi hadi Amazonia!

Tani 50 za madawa na vifaa vimetumwa nchini Peru.Ni matunda ya jitihada za ushirikiano kati ya Baraza la kipapa la Elimu na Nchi ya Falme za Uarabuni.

VATICAN

Licha ya anga kuwa wazi bila mizinguko ya hapa na pale kutokana na vizuizi vya kujikinga na virusi vya corona au Covid-19, lakini mshikamano mpya unaendelea kufungua anga hilo. Na huu ni msaada  kutoka Abu Dhabi, katika nchi za Falme za uarabuni kwenda Lima nchini Peru, ambapo tarehe 25 Juni 2020, ndege yenye kubeba tani 50 za msaada wa kibinadamu imesafiri kwenda katika mji mkuu wa Amerika ya Kusini. Na kwa njia ya barabara, pia  tani hizo zinatapelekwa hadi   mji wa Iquitos,  wenye wakazi 400,000 ambapo wanapakana na Rio ya Amazonia, yaani katikati ya msitu wa Amazonia.

Safari ya ndege inapeleka vifaa muhimu kwa ajili ya kuweza kuzuia kuenea kwa janga hili, ambalo nchini Amerika ya Kusini  kwa sasa imekuwa ni kitovu kipya cha ulimwengu. Barakoa, glavu, oksijeni ya matibabu na vyakula ambavyo vitaweza kutatengwa na Kanisa mahalia na kusambazwa kwa watu wenye kuhitaji zaidi. Sehemu nyingine ya vifaa vitapelekwa katika vituo vya afya na mafundisho; vingine vinavyobaki vitasambazwa katika familia za eneo hilo.

Mpango huu umejumishwa kwa  kushirikiana na Mfuko wa Taasisi ya Kipapa ya elimu (Gravissimum Educationis Foundation), inayofanya kazi ndani ya Baraza la Kipapa la  Elimu Katoliki. Sheikh Mohamed bin Zayed, Mfalme wa Abu Dhabi, ameitikia mwaliko wa Papa Francisko kusaidia watu maskini zaidi wa ulimwengu kwa kutoa vifaa vya afya. Ushirikiano huo ni sehemu ya Hati ya Udugu wa kibinadamu wa amani na umoja wa ulimwengu, uliotiwa saini huko Abu Dhabi kwenye fursa ya  ziara ya Papa Francisko.

Na kwa mujibu wa maoni ya Monsinyo Guy-Réal Thivierge, Katibu Mkuu wa Mfuko wa Elimu amesema “Idadi ya watu wote hawakabiliani na janga la virusi tu, bali pia na umaskini, ambao umezidishwa na janga hili” “Katika hali kama hii kipaumbele chao ni kuishi. Kwa njia hii lazima kwanza tutulize mahitaji msingi kama vile (chakula na vifaa vya afya), na baadaye mahitaji ya kielimu. Ni njia ambayo inafungua njia ya elimu fungamani”.

25 June 2020, 12:17