Vatican News
CENTENARY CENTENARY 

Ni roho Mtakatifu anayeongoza vyama vya Wakristo!

Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Umoja wa Wakristo limeandika barua yao katika fursa ya ujumbe wa Papa Francisko alioutuma kwa njia ya video tarehe 31 Mei 2020 katika fursa ya tukio la Thy Kingdom Come” huko Uingereza.

Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Umoja wa Wakristo limeandika barua yao katika fursa ya ujumbe wa Papa Francisko alioutuma kwa njia ya video tarehe 31 Mei 2020 kwa tukio la Thy Kingdom Come” yaani “Ufalme wa Mungu Uje” huko Uingereza. 

Baraza la Kipapa la uhamasishaji wa Umoja wa Wakristo katika barua yao wanakumbusha kuwa Pentekoste inatukumbusha kuwa ni Roho Mtakatifu anayeongoza vyama vya Wakristo kuelekea ule msimamo wa umoja ambao Kristo mwenyewe aliomba  wakati wa kusali kwenye  Karamu kuu  ya mwisho.

Chama cha ‘Thy Kingdom Come’ kama vile Askofu Mkuu Welby, ni fursa kwa ajili ya wakristo waliounganika katika sala kwa ajili ya uinjilishaji ulimwenguni. Katika ujumbe kwa njia ya  video, Papa Francisko amesali ili wakristo wote waweze kuwa na umoja wa kina na kama ushuhuda wa huruma kwa ajili ya ubinadamu uliojaribiwa na kukumbusha kuwa “ hatuwezi kuomba ubinadamu ubaki na umoja ikiwa tunakwenda katika njia tofauti”.

Kadhalika katika ujumbe wake Papa ameonyesha kuunga mkono chama hiki cha ‘Thy Kingdom Come’ yaani ‘Ufalme wako Uje’ kama alivyopenda Askofu Mkuu kwa wito wake kwa Umoja, hasa kwa kuongozwa na  katika kusikiliza sala ya Yesu “ili wote wawe na umoja… na ili ulimwengu upate kuamini”(Yh 17, 21).

31 May 2020, 14:04