Mtakatifu Yosefu na Papa Francisko ni kama vile Papa Pio XII!
Na Sr. Angela Rwezaula –Vatican
Kama ilivyokuwa miaka 64 iliyopita, bila umati kwa sababu yetu ya siku za janga ,lakini na mlinzi huyo huyo wa wafanyakazi ambaye anatazama kikundi ambacho kimeguswa kwa namna ya pekee ya ugumu wa kazi na mtazamo kwa wote, kama ilivyokuwa hata katika mkesha wa enzi za kijamii ambazo zilikuwa zinapaswa kuijenga kwa upya nchi ya Italia mara baada ya vita.
Sanamu kutoka Milano hadi Roma
Zaidi ya tofauti za kihistoria,kuna mambo yanayofanana sana juu ya sanamu ya Mtakatifu Joseph ambayo ililetwa mjini Vatican siku ya Alhamisi 30 Aprili alasiri na kuwekwa katika kikanisa cha Mtakatifu Marta, kwa matazamio ya Misa iliyoadhimishwa katika asubuhi ya Mei Mosi, 2020 na Papa Francisko katika siku kuu ya Mtakatifu Yosefu. Na hii ilikuwa ni mwaka 1956 sanamu kama hiyo ilibarikiwa kunako Mei Mosi na aliyekuwa Askofu Mkuu wa Milano Giovanni Battista Montini na kunako Mei 2 ilisafirishwa na helikopta kuja Roma ili ibarikiwe pia na Papa Pius XII wakati wa Mkutano uliokuwa unafanyika siku hiyo na Chama cha wakristo wafanyakazi wa Italia (ACLI). Ni Mkutano ambao uliangukia miezi kumi na mbili baada ya Misa ambayo Papa Pacelli alikuwa ameifanya katika liturujia ya kuweka wakfu sherehe ya Mchumba wa Maria na mlinzi wa Yesu kwenye sikukuu ya wafanyakazi ambayo ilikuwa inaadhimishwa ulimwenguni kote .
Sanamu kuletwa mwaka 2015
Chama cha wakristo wafanyakazi wa Italia (ACLI) kama leo hii ambao wamependelea kulemtea Papa Francisko sanamu iliyotengenzwa kwa shaba na mchoraji Enrico Nell Breuning, ina urefu wa sentimeta 150, iliyotunzwa katika makao makuu ya chama chao Roma. Kiukweli, sanamu hiyo ilikuwa tayari imewekwa mbali na Papa Francisko, wakati ilipoletwa katika maandamano wakati wa Katekesi katika Ukumbi wa Papa Paul VI kunako tarehe 23 Mei 2015.
Kazi iliyo huru na ya mshikamano
Mchezo wa marudio ambao unajumuisha mambo ya sasa, na wasiwasi mwingi unaotikisa ulimwengu wa kazi, kama vile wa zamani na katika kumbu kumbu ya wale waliotutangulia na ambapo, kwa mujibu wa maandishi ya Rais wa kitaifa wa Chama cha Wakristo Wafanyakazi Italia, (ACLI ) Bwana Roberto Rossini, kwa Papa Ftancisko anasema : “inatutia moyo kufanya kazi ili kama ulivyo wewe Baba Mtakatifu ambaye umesisitiza mara kwa mara kuwa, hakuna mfanyakazi ambaye hasiweze kuwa na haki na kazi iwe huru, ya ubunifu, shirikishi na ya mshikamano” "