Vatican News

Makumbusho na bustani za Vatican kufunguliwa tena kwa umma!

Mchanganyiko wa sanaa maalum katika makumbusho ya Vatican na ya kushangaza unaweza kutembelewa tena,kwa kuheshimu sheria za usafi na umbali.Ni kuanzia Mosi Juni 2020 na wakati huo huo bustani nzuri za Kipapa huko Castel Gandolfo zitafunguliwa tarehe 6 Juni.

VATICAN NEWS

Jumba la Makumbusho la Vatican linafungauliwa kwa mara nyingine tena kunako Mosi Juni, 2020 kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na mamlaka ya Italia hasa mara baada ya  kufungwa kwa karibia  miezi 3, na ambapo  kanuni sasa  zinaruhusu biashara nyingi na shughuli kuanza kwa mara nyingine tena. Vile vile hata kufunguliwa tena Bustani za Kipapa za Castel Gandolfo na safari mpya za Bus ya utalii vimetangzwa kuanza tena.

Kufuata kanuni za afya na sanaa

Kwa sababu ya hali ya sasa ya dharura ya kiafya, Majumba ya Makumbusho ya Vatican yatahakikisha usalama na mahitaji ya kiafya na mienendo yote ya ziara ndani ya makumbusho, bila kuathiri lengo la ziara hiyo. Kwa maana hivyo, kwa kuzingatia kanuni za usafi na umbali, wageni ambao watatakiwa kuja katika makumbusho watatakiwa kuwa chini ya ukaguzi wa joto la mwili na wataruhusiwa tu ikiwa watakuwa wamevaaa barakoa. Timu ya madaktari na afya kutoka kwa kikundi cha kujitolea cha Misericordie cha Italia na Idara ya Afya na Usafi wa Vatican vitahakikisha kila hitaji wakati wa masaa ya ufunguzi. Mahitaji mengine muhimu ya ufunguzi wa makumbusho yatarekebishwa mara kwa mara kulingana na hali halisi ya dharura itayotokea.

Maombi kupitia mtandaoni

Ili kuzuia idadi kubwa ya kuingia katika Makumbusho ya Vatican watakuwa wanatoa tiketi chache lakini kwa kupitia njia ya kuomba  katika mtandao tu  kwenye Tovuti rasmi :website www.museivaticani.va

Ada ya Euro 4 ya kuomba  kutembelea makumbusho kupitia mtandaoni katika kipindi hiki cha dharura ya janga haitakuwapo!

Masaa ya ufunguzi wa majumba ya makubusho:

- Jumatatu hadi Alhamisi: Mkusanyiko katika eneo la Kipapa litabaki wazi kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi saa 2.00 usiku, maingilio ya mwisho ni saa 12.00 za jioni (Kutoka katika sekta ya makumbusho kuanza saa 1.30 usiku)

- Ijumaa na Jumamosi: kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi 4.00 usiku, na kiingilio cha mwisho ni saa 8.00 usiku. (Kutoka katika sekta ya makumbusho saa 9.30 usiku). Ziara za makumbusho siku ya Ijumaa na Jumamosi zinaambatana na uwezekano wa kushiriki hata vinywaji katika viwanja ndani ya jengo la makumbusho ili kufurahia wakati huu. Hata hivyo kama ilivyokuwa kawaida ya kuingia bure katika makumbusho kwa siku ya Jumapili ya mwisho wa kila mwezi kwa sasa imesimamishwa.

Ziara mpya ya Bus na  Bustani za Kipapa

Mbali na ziara ya Makumbusho ya Vatican, kuna hata  safari mpya ya Bus iliyo wazi ya kiekolojia ili kuweza kuona uzuri wa bustani za Vatican. Inatoa ufikiaji wa kipekee na wa moja kwa moja katika moyo wa kijani wa Jiji la Vatican.

Ili kuomba kufanya ziara hizo, inawezekana kutuma ombi kupitia mtandao tu katika Tovuti: www.museivaticani.va itakayowezesha kupata maelezo yote yanayohusiana na safari hizo.

kutembelea  makazi ya Baba Mtakatifu na bustani zake katika kipindi cha jua inatumia muda mfupi  ambapo umejikita kwa siku ya Jumamosi na Jumapili tu, tangu saa 4.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni na kiingilio cha mwisho ni saa 11.00 jioni.

Ziara ya kwanza kwenda bustani ni tarehe moja Juni

Ziara ya kwanza ya kwenda kwenye Bustani za Kipapa imepangwa kufunguliwa kunako Jumamosi tarehe  6 Juni 2020. Hapa pia wageni wote watakuwa chini ya ukaguzi wa joto na mhusika ni ya lazima avae barakoa! Treni ya kwenda kwenye Bustani za Kipapa ambayo uchukua wageni kutoka kituo cha reli ya Vatican kwenda Castel Gandolfo, imesimamishwa kwa muda.

Ikumbukwe kunako tarehe 1 Machi, Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican ilitangaza kufungwa kwa tahadhari kwa majumba ya Makumbusho ya Vatican na safari nyingine za kutembelea kwa kushirikiana kwa hatua za mamlaka ya Italia ili kuzuia kuenea kwa COVID-19.

23 May 2020, 15:05