Mwaliko wa Kardinali Ayuso Guixot katika fursa ya Sikukuu ya mwisho wa mfungo wa Raamadhani kwa ndugu waislamu ni mshikamano na udugu katika muktadha wa Hati ya Udugu wa kibinadamu Mwaliko wa Kardinali Ayuso Guixot katika fursa ya Sikukuu ya mwisho wa mfungo wa Raamadhani kwa ndugu waislamu ni mshikamano na udugu katika muktadha wa Hati ya Udugu wa kibinadamu 

Ramadhani na ‘Id al-Fitr,viwe fursa ya kukua kindugu!

Katika ujumbe uliosainiwa na Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot,Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini na Katibu wake,Monsinyo Indunil Kodithuwakku Janakaratne Kankanamalage,wanasisiza kuwa maeneo ya utamaduni yana umuhimu mkubwa katika ukristo na katika Uislamu na kama ilivyo katika dini yingine.Hayo ni katika muktadha wa matashu mema ya fursa ya mwezi wa Ramadhani na sikuu ya Id al-Fitr 2020.

Na Sr.Angela Rwezaula – Vatican

Mwezi wa Ramadhani ni kitovu cha dini yenu kwa maana hivyo kwenu ninyi ni muhimu kwa ngazi binafsi, kifamilia na kijamii. Ni kipindi cha kuponya kiroho  kuku ana kushirikishana na maskini na kukuza ule uhusiano na ndugu na marafiki. Ndivyo unaanza ujumbe uliosainiwa  na Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot,Rais wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini na Katibu wa Bara hilo,Monsinyo Indunil Kodithuwakku Janakaratne Kankanamalage, katika fursa ya Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani  kwa Waislam na matarajio ya Sikukuu ya Id al-Fitr 1441 H. / 2020 A.D.

Ramadhana na Id al Fitr ni fursa ya kukua kindugu

Katika ujumbe huo, wanasema kwa upende wa  wakristo marafiki zao ni kipindi mwafaka cha kudumisha uhusiano wao na wao, kwa njia ya salam na kukutana, mahali ambapo kuna uwezekano  na kwa kushiriki iftar.  Ramadhan na‘Id al-Fitr  ni fursa maalum ya kukua kidugu kwa hakika kati ya wakristo na waislamu. Katika roho hiyo ndiyo maana Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini  wanatoa heri nyingi na maombi kwao. Kwa kufuata utamaduni wao, wamependa kushirikishana nao baadhi ya mawazo yanayoongoza pamoja kama kauli mbiu ya mwaka huu  kuhusu ulinzi wa maeneo ya ibada. Inaeleweka wazi kuwa katika maeneo ya ibada inachukuliwa umuhimu mkubwa sana katika Ukristo na Uislam, kama ilivyo hata katika dini nyingine, wanaandikia, kwani, kwa wakristo na kwa waislam, makanisa na misikiti ni nafasi ambazo zimewekwa kwa ajili ya sala binafsi na kijumuiya , katika majengo yaliyowekwa na kunakinishwa ili kusaidia ule ukimya wa ndani, tafakari na maombi.  Ni sehemu ambazo inawezekana kujikia kwa ukina wa roho na kurahisisha kwa maana nyingine ule ukimya na uzoefu wa kukutana na Mungu. Kwa njia hiyo mahali pa ibada ya dini yoyote ni “nyumba ya sala” (Isaya 56, 7). wanaandika.

Mahali pa kufanyia ibada ni sehemu ya ukarimu

Mahali pa ibada ni sehemu pia ya ukarimu kiroho, mahali ambapo wafuasi wa dini nyingine wanakusanyika hata kwa ajili ya sikukuu maalum kama vile arusi, mazishi, sikukuu za jumuiya na nyingnezo. Kwa kushiriki katika matukio hayo kwa ukimya na heshima inayotakiwa kudumisha dini za wafuasi na zile dini maalum, zote zinaonja ukarimu maalum uliodumishwa na kuhifadhiwa, wanaandika. Mazoezi haya ni ushuhuda maalum wa kile ambacho kinaunganisha waamini bila kupunguza au kukataa kile kinachotofautisha.

Katika  mantiki hii, ujumbe wa wakuu  wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini wamependa kukumbusha kile ambacho Papa Francisko alisema wakati wa kutembelea msikiti wa Heydar Aliyev, huko Baku (Azerbaijan), Dominika ya tarehe 2 Oktoba 2016 kwamba: “Ni ishara nzuri kukutana katika urafiki wa kidugu katika mahali hapa pa maombi, ishara ambayo inajidhihirisha maelewano ambayo dini kwa pamoja zinaweza kujenga, kuanzia uhusiano kibinafsi na wale wenye mapenzi mema hasa wanaohusika”.

Mashambulizi mahali pa ibada ni uovu

Katika muktadha wa mashambuli dhidi ya makanisa, miskiti, masinagogi, yanayo dhulumiwa na watu waovu ambao wanaonekana kuingia  kati mahali pa ibada kwa shabaha inayopendelewa na kutumia dhuluma yao  kipofu na isiyo na akili, kama inavyoeleza Hati ya Udugu wa Kibinadamu kwa ajili ya amani duniani na kuishi pamoja,  iliyotiwa sahihi na Papa Francisko na Imam Al-Azhar, Dk. Ahmad Al-Tayyeb, huko  Abu Dhabi, tarehe 4 Februari  2019: “Ulinzi wa mahali pa ibada, mahekalu, makanisa na misikiti ni jukumu linalodhibitishwa na dini, maadili ya mwanadamu katika mikataba ya kimataifa. Kila jaribio lolote la kushambulia maeneo ya ibada au kuwatishia kupitia shambulio au milipuko au uharibifu ni kupotosha kwa mafundisho ya dini,na vile vile ni ukiukwaji ulio wazi wa sheria za kimataifa.”

Matumaini ya kuheshimiana na kushirikishana pamoja

Kwa kuthamini juhudi zilizofanywa na jumuiya ya kimataifa katika ngazi mbali mbali katika kulinda mahali pa ibada ulimwenguni, ndiyo matumaini  na amatashi yao kwamba  kwa kuheshimiana na kushirikiana pamoja  kunaweza kuimarisha uhusiano wap wa urafiki wa dhati, na kuruhusu jamuiya zao kulinda mahali pa ibada ili kuweza kuhakikisha vizazi vijavyo vinapata uhuru msingi wa kukiri imani yao. Wanahitimisha ujumbe wao kwa kurudia kutoa salam za kidugu, na kwa niaba ya Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini wanawatakia matashi yenye matunda katika mwezi wa Ramadhani na furaha ‘Id al-Fitr.

01 May 2020, 12:00