Vatican#coronavirus Papa atoa msaada wa vifaa muhimu vya kusaidia wagonjwa!
VATICAN
Vioo vya kujikinga, barakoa na vifaa vingine muhimu vya lazima vya msaada wa huduma kwa walioambukizwa vimeweza kufika katika Hospitali ya Regina Apostolorum la Shirika la Mabinti wa Mtakatifu Paulo huko Albano nchini Italia. Hivi karibuni nyumba hivyo imegeuzwa kuwa Kituo cha Wagonjwa wa Covid-19.
Msaada huo umetolewa na Papa Francisko ambao umeelekezwa kwa Askofu jimbo hilo Askofu Marcello Semeraro. Katika vifaa hivyo vya huduma Papa Francisko ameidha ametuma kifaa kingine muhimu sana cha kupumua kwa ajili ya matibabu ya wagonjwa katika vyumba vya mahututi katika kituo hicho hicho.
Kwa mujibu wa Papa Francisko amekusudia kuonesha ukaribu msaada huo kwa wasimamizi wote, kwa wafanya kazi wote na kwa namna ya pekee wale wote wenye maambukizi ya ugonjwa huo wa corona, ambapo Yeye binafsi yuko karibu na kila mmoja wao kiroho kwa sala na kwa maana hiyo amewabariki kwa Baraka ya Kitume kutoka moyoni, kama msaada na nguvu kutoka mbinguni na faraja inayohitajika katika wakati huu.
Hayo yote yanasomwa kutoka katika Barua iliyotumwa kwa mwakilishi wake wa Sadaka ya Kitume Kardinali Krejeweski. Kufuatia na tukio hili naye Askofu wa Jimbo Katoliki la Albano ametosa shukrani zake kwa Papa Francisko na kwa niaba ya uongozi wa Hospitali hiyo.
Shukrani pia zimemwendea Kardinali Konrad Krajewski, ambaye ni Msimamizi wa Sakadaka ya Kitume ambaye amemwakilisha hivi karibuni Papa Francisko kuwafikishia msaada wa zana hizo muhimu katika wakati huu mgumu.