Vatican News
Kuna nafasi kwa ajili ya Mungu, lakini nafasi hiyo imefungwa ndani ya fumbo la maisha. Wema uliofanywa hata hivyo unabaki.Katika kaburi tupu la Kristo,kuna utupu wa matarajio yetu,siyo utupu wa Mungu. Kuna nafasi kwa ajili ya Mungu, lakini nafasi hiyo imefungwa ndani ya fumbo la maisha. Wema uliofanywa hata hivyo unabaki.Katika kaburi tupu la Kristo,kuna utupu wa matarajio yetu,siyo utupu wa Mungu. 

Italia#Covid-19.Kard.Filoni:Katika kusubiri Pasaka swali:Je Mungu yuko wapi?

Katika kipindi hiki cha covid-19kuibuka maswali mengi ya kujiliuza hasa kwa kufikiria dunia iliyokuwa imeegema uhakika wa kimkamakati na kisayansi,mwasali haya ni kama:je imekuwaje mambo haya kutoroka mikononi mwetu?Ni kitu gani ambacho hakikuweza kufanya kazi? Je tufanye nini na nini tusifanye?Je kipindi hiki kitadumu hadi lini?Je ni wangapi watakufa?Ni kutoka tafakari ya Kardinali Ferdinando Filoni Mkuu wa Shirika la Ulinzi wa Kaburi Takatifu Yerusalemu

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika kipindi hiki cha janga  (Covid-19), kilichoikumba mipango ya maisha yetu,imetetemesha uhakika wetu unaojijenga kimkakati na kiyasansi na ambayo katika dunia inatishia na mambo yake ya majanga ya vifo, maambukizi, upweke wa kulazimishwa, uhusiano uliovunjwa, wa kazi zenye shida na kuona vikwazo vya kushindwa kwetu kwa kuanza kujiuliza, je imekuwaje mambo haya kutoroka  mikononi mwetu? Ni kitu gani ambacho hakikuweza kufanya kazi? Je tufanye nini na nini tusifanye? Je kipindi hiki kitadumu hadi lini? Je ni wangapi watakufa? Kuna hali ya kuonesha hofu, hasira, uchungu, matumaini; tunatimza ibada, ishara za ukarimu; unajielezea mahhitji, tunstunza, tunazika, tunachoma; lakini yote hayo Mungu yuko wapi? Utafikiri hata sala hazina majibu, Mungu anasikiliza? Na kwa nini yanatokea hayo yote? Ni kutokana na kasoro zetu ambazo hatuwezi kupata jibu? Ndiyo tafakari ya Kardinali Ferdinando Filoni  mkuu wa Shirika la Ulinzi wa Kaburi Takatifu Yerusalemu “Order of the Holy Sepulchre of Jerusalem”, iliyowekwa katika tovuti ya ya shrika hilo (www.oessh.va).

Katika  tafakari anazidi kutoa maswali, hali akiandika kuwa tunakosa ufunguo  kwa mara nyingine tena  ambao unafunga ubunifu, anga lenye jengo, upinde wa daraja na hatari kwamba kila kitu kitaanguka, kwamba kila kitu kimekosa maana. Mungu yuko wapi? Swali moja la ndani na la kina linarudi kila wakati. Tendo la nimekosa mimi ni ibada, kitendo kinachochochewa na hali isiyodhibitiwa? Je! Ni  tunda au matokeo ya kazi yetu mbaya? Swali, “Mungu yuko wapi?”: Je! Ni wa juu au haina maana? Na je! Mungu ana uhusiano wowote na hilo au la? Je ina maana kujiuliza Mungu yuko wapi? Je ni majibu gani tuliyo mayo?  Je majibu yapo? Yako katika mwelekeo wa muda? Hata maswali hayo yanarudisha katika muda mwingine.

Ukweli unatupeleka kutokuwa na jibu, ambalo, kwalo lenyewe, linapatikana. Kama ilivyo kuwa kwa Ayubu wa kibibilia. Majibu ni juu ya maswali halisi. Ikiwa hii ndiyo kesi, tunabaki na utupu bila jibu. Isipokuwa utainua mtazamo juu, na siyo kuwa na jibu juu ya kesi hiyo ya kutatuliwa, lakini ili kujua kwamba, ikiwa Mungu hayupo au hana mahali katika shida hii, kila kitu kimefungwa katika hali ya mtiririko? Ikiwa Mungu yuko, basi sikutambua hitaji la kuwa na jibu, bali kuwa na “msamaha”. Kila kitu kimefanywa! ya Kristo msalabani ni msamaha ("Na akainamsha kichwa akarudisha roho". (Yh 19, 30) kwa Baba, ambaye kwa hakika anamuomba huyo ‘Misterium vitae’ yaani siri ya vita ambayo ilimleta duniani kama sehemu yake. Ubaba (wa Mungu) hahusishi mipaka ambayo Mungu mwenyewe alikuwa amemwekea mwenyewe katika ubaba" wake.

Muktadha unarudi kwetu, Kardinali Filoni anaandika kwa maana kwamba unarudi kwetu. Si kwa ajili ya kujiuliza na kutatufa tena maana ya jibu ambalo tunasubiri, badala yake ni kuwa na maana ya mwenendo, ili tujiulize na bado tunatafuta jibu lakini jibu lisilotegemewa, badala ya kuwa na akili ya tabia, dhidi ya kishawishi zaidi cha ama kuishi kama Mungu vile hakuwepo, au kujazwa na maswali  ya adhabu ya Mungu na kila kitu kama sehemu ya toba; Vinginevyo, kilichobaki ni kumkabidhi kila kitu kwa Mungu tena, na kukubali kwamba katika "wakati huu wa mwanadamu", leo hii siyo kitendo cha kuamini msamaha hakipaswi kutengwa, “kwani katika mikono yako, ee Baba, naiweka roho yangu” yaani mahali ambapo kila kitu kinamalizika kuwa, “Baada ya kusema haya akakata roho(Lk 23, 46).

Amani ya roho iko katika kurudi kwa amani yake  ya awali ambayo kila kitu kilianzia yaani tangu mwanzo hapakuwa na kitu au Mungu. Ikiwa hakuna kitu kinachotoka kwa kitu, ina maana kwamba ni Mungu pekee anayesalia. Kuna nafasi kwa ajili ya Mungu, lakini nafasi hiyo imefungwa ndani ya fumbo la maisha. Wema uliofanywa, hata hivyo, unabaki. Deni lake bado haliwezekani kulipwa. Wema ni wetu na hii ina maana lakini sifa kuu, ambayo ni ya maadili na ya kiroho, hupitia mikononi mwa Mungu. Wema huo haujazimwa kamwe! Katika kaburi tupu la Kristo, kuna utupu wa matarajio yetu, siyo utupu wa Mungu. Katika ukimya, kuna ukimya wa majibu yanayotarajiwa na siyo ukimya wa Mungu. Tunasubiri Pasaka.

08 April 2020, 14:08