Vatican News
2020.04.01 AFRICA CORONAVIRUS 2020.04.01 AFRICA CORONAVIRUS  

Italia#coronavirus:Euro milioni 6 kusaidia dharura!

Baraza la Maaskofu nchini Italia wameamua kutenga euro milioni 6 nyingine kutoka katika mfuko wa fedha"Otto per Mille"ambao unasaidiwa na wananchi wa Italia katika kutoa sadaka kwa Kanisa Katoliki ili kusaidia nchi za kiafrika na nyinginezo maskini katika hali ya sasa ya ulimwengu wenye shida.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Siku chache baada ya uingiliaji maalum kwa jumla ya euro milioni 16, zilizopangwa kukabiliana na dharura ya virusi vya corona  nchini Italia, Baraza la Maaskofu nchini  Italia wameamua kutenga euro milioni 6 nyingine kutoka katika wa fedha wa Otto per Mille  ambao wananchi wa Italia hutoa sadaka kwa Kanisa Katoliki ili kusaidia nchi za Kiafrika na zinginezo maskini katika hali ya sasa ya ulimwengu wenye shida.

Katika utambuzi ya kwamba  kwamba nchi hizi zinakabiliwa na ugumu zaidi katika kukabiliana na janga la corona  na kwamba hali tayari inaweza kuwa mbaya, Rais wa Baraza la Maaskofu Italia ameagiza kitengo cha Huduma  ya dharura kuingilia kati kwa ajili ya nchi maskini  Duniani na Caritas ya Italia kutengeneza mkakati wa haraka wa hatua ambayo inaingilia kati mipango ya hatua za afya na mafunzo.

Njia ya utekelezaji, ambayo imegunduliwa, inajumuisha kutafuta usaidizi hasa kwa upande hospitali na taasisi  Katoliki zinazofanya kazi katika maeneo husika. Kwa kusudi hilo, milioni 5 zimetengwa kwa ajili ya  huduma za afya na Euro Milioni moja kwa ajili ya  mafunzo. Lengo la  kwanza litakuwa ni kuandaa vifaa vya afya katika nchi hizi na vifaa vya kinga kwa wafanyakazi wa afya, muhimu kwa usimamizi wa dharura na zana za matibabu za kushughulikia janga hili.

Watakao barikiwa zaidi  ni wale ambao watakuwa karibu na majengo yaliyo karibu na idadi ya watu, wanaozunguka zaidi na ambao walikuwa  tayari wako katika mtandao wa vyombo vinavyojulikana na kuungwa mkono katika siku za nyuma, na ambazo zimedhibitishwa kuwa na ufanisi na mzuri. Kwa kuongezea, wanasema  hatua hisi  zitaungwa mkono kuhamasisha idadi ya watu  kuepuka kuambukizwa, kuongeza mafunzo na maandalizi ya kiufundi ya wafanyakazi wa huduma ya afya.

Hatua hizo za maombi  ya ufadhili yanapaswa kukubaliwa na taasisi za umma mahalia, kitaifa, kikanda na kimataifa na viongozi wanaosimamia na vyombo vyote vinavyohusika katika eneo hilo ili kutia moyo jamii zote, kulingana na mazoea ya kawaida na kulingana na zile zinazohitaji msada zaidi wa dharura.

Aidha maombi ya ufadhili kutoka kwa wenye nia, lazima yawasilishwe kuanzia tarehe 14 mwezi huu  hadi 30 Aprili 2020, kulingana na njia zilizoonyeshwa kwenye tovuti yao ya: www.chiesacattolica.it/sictm

Kwa kuzingatia uzito na uharaka uliopo wa hali hiyo, miradi hiyo inapaswa kukamilishwa ndani ya miezi mitatu kutokana na  ulipaji wa mchango ulioombewa.

03 April 2020, 14:06