Maadhimisho ya Tukio la "Uchumi wa Francisko" sasa kufanyika tarehe 21 Novemba 2020 badala ya tarehe 26-28 Machi 2020. Maadhimisho ya Tukio la "Uchumi wa Francisko" sasa kufanyika tarehe 21 Novemba 2020 badala ya tarehe 26-28 Machi 2020. 

Tukio la "Uchumi wa Francesco" sasa kuadhimisha: 21 Nov. 2020

Kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika, tukio hili kwa sasa linatarajiwa kuadhimishwa hapo tarehe 21 Novemba 2020. Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka mjini Assisi zinabainishwa kwamba, zaidi ya vijana 2, 000 kutoka katika nchi 115 tayari walikuwa wamekwisha kujiandika ili kushiriki. Tukiwa hili hapo awali lilitarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 26-28 Machi 2020, huko mjini Assisi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko anasema, “Economy of Francesco” yaani “Uchumi wa Francisko” ni tukio ambalo lilitarajiwa kuwakusanya wachumi, wajasiriamali, pamoja na wachumi vijana kutoka sehemu mbali mbali za dunia, kuanzia tarehe 26 - 28 Machi 2020 huko Assisi, nchini Italia. Kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika, tukio hili kwa sasa linatarajiwa kuadhimishwa hapo tarehe 21 Novemba 2020. Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka mjini Assisi zinabainishwa kwamba, zaidi ya vijana 2, 000 kutoka katika nchi 115 tayari walikuwa wamekwisha kujiandika ili kushiriki.

Kamati kuu inasema, uamuzi huu umechukuliwa na Baba Mtakatifu Francisko baada ya kujadiliana na Kamati kuu ya Maandalizi ya Siku ya Uchumi wa Francisko. Kwa wakati huu imekuwa ni vigumu sana wanafunzi kutoka sehemu mbali mbali za dunia kusafiri kwa urahisi. Tarehe 28 Machi 2020, Kamati kuu itaungana na vijana kutoka sehemu mbali mbali za dunia kwa njia ya mtandao, ili kuendelea kuwahamasisha vijana kushiriki kikamilifu tukio hili la kihistoria. Hii ni sehemu ya mbinu mkakati wa utume wa Kanisa miongoni mwa vijana wa kizazi kipya, unaotekelezwa kwa namna ya pekee, na Baba Mtakatifu Francisko.

Hii itakuwa pia ni nafasi kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro, kukutana na kuzungumza na vijana wanaojifunza uchumi unaotekelezwa katika medani mbali mbali za maisha ya mwanadamu! Anataka kuzama zaidi katika uchumi unaohuisha na wala si ule unaowatumbukiza watu katika kifo. Uchumi fungamani unaojikita katika tunu msingi za utu na heshima ya binadamu; uchumi unaojikita katika utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote. Baba Mtakatifu katika barua ya mwaliko kwa wachumi na wajasiriamali vijana, anawataka kujizatiti katika mchakato wa kupyaisha uchumi duniani, kwa kujikita katika udugu kama alivyokazia Mtakatifu Yohane Paulo II, kwa kuuchagua mji wa Assisi kuwa ni kitovu cha amani na kwa sasa yeye angependa kuona mji wa Assisi unakuwa ni jukwaa la mchakato wa mfumo mpya wa uchumi duniani.

Uchumi wa Francisko
02 March 2020, 13:29