Askoffu Mkuu Paul Richard Gallagher amekutana na Waziri wa mambo ya nchi za Nje wa Jamhuri ya watu wa China Bwana  Wang Yi Askoffu Mkuu Paul Richard Gallagher amekutana na Waziri wa mambo ya nchi za Nje wa Jamhuri ya watu wa China Bwana Wang Yi 

Vatican na China:ahadi za kuendeleza mchakato wa safari ya majadiliano!

Mazungumzo huko Monaco kati ya Askofu Mkuu Gallagher na Waziri Mkuu wa nchi za Nje wa China ambapo wamejikita kutazama umuhimu wa Mkataba ya makubaliano ya muda juu ya uteuzi wa maaskofu na utashi wa kuendelea na mchakato wa safari ya majadiliano kwa ajili ya maisha ya Kanisa Katoliki wa China na ustawi wa watu wa China.

Vatican

Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher Katibu wa Vatican wa Mahusiano na ushirikiano wa nchi za Nje amekutana  na  Waziri Mambo ya nchi za Nje wa Jamhuri ya watu wa China Bwana  Wang Yi, kando ya Mkutano wa Kimataifa kuhusu Usalama uliofanyika huko Monaco nchini Ujerumani tarehe 14 Februari 2020. Ilikuwa ni miaka 70 tangu mkutano wa namna hii rasmi ufanyike.

Katika mazungumzo yao wameonesha hali ya utulivu kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu  Vatican na kwamba wamekuwa walikuwa wakiwasiliana sehemu zote mbili na kukuza mawasiliano chanya kwa kipindi sasa. Kwa namna ya pekee wamebainisha juu ya umuhimu wa mkataba wa Muda kuhusu uteuzi wa Maaskofu, uliotiwa sahihi kunako tarehe 22 Septemba 2018 na kupyaisha kwa mara nyingine tena utashi wa kuendelea katika njia ya majadiliano ya kitaasisi kwa ngazi zote mbili ili kuweza kusaidia maisha ya Kanisa Katoliki na kwa ajili ya wema wa Watu wa China kwa ujumla.

Hata hivyo wamepongeza kuhusu jitihada ambazo zinaendelea kutimizwa kwa ajili ya kupambana na mlipuko wa coronavirusi na mshikamano mbele ya watu walioshambuliwa na janga hili. Hatimaye katika mazungumzo yao ni matarajio kuendeleza mshikamano kimataifa ili hatimaye kukuza namna ya kuishi kwa pamoja kizalendo na amani duniani na wakati huo huo kubadilishana mawazo juu ya majadiliano ya kiutamaduni pamoja na haki za binadamu.

Kuhusiana na mlipuko wa coronavirusi, ikikumbwe kwamba siku ya Jumatano  ya wiki hii mara baada ya Katekesi ya Papa Francisko, alielezea ukaribu wake wa sala kwa watu wote wa Jamhuri ya nchi ya China na kuwaomba waamini wasali wote kwa ajili ya watu wanaoteseka na ugonjw mbaya huo  ili  waweze kupona haraka iwezekanavyo.

15 February 2020, 16:29