Uwakilishi wa Ofisi ya Katibu wa Vatican kutembelea wafungwa Regina Coeli
VATICAN
Jumapili asubuhi tarehe 2 Februari 2020 kikundi kutoka katika Ofisi ya Katibu wa Vatican kimetembelea Gereza la wafungwa wa Regina Coeli jijini Roma, ili kushiriki maadhimisho ya Misa Takatifu ya Domiminika na kuwakabidhi zawadi za mshikamano uliokusanywa kutoka kwa wafanyazi wa Taasisi ya Vatican wakati wa kipindi cha Majilio na cha Kuzaliwa kwa Bwana kwa ajili ya watu wenye shida zaidi. Hayo yote yameelezwa na msemaji mkuu wa vyombo vya habari Vatican, Dk. Matteo Bruni.
Uhamasishaji wa kibinadamu
Baada ya maadhimisho ya misa ambayo pia kulikuwapo na maombi ya waamini wafugwa pia walikwenda kutembelea hata kituo kikuu cha Chama cha kujitolea kinachoongozwa na Mafrateli wafransiskani wakonventuali Vo.Re.Co,. Shughuli yao ikiwa katika kuhamasisha ubinadamu na ukristo kwa kuwasaidia wafungwa na wale wote ambao baada ya kutoka kifungoni wanatelekezwa na jamii.
Rosari zilizobarikiwa na Papa
Kabla ya kurudi Vatica, wawakilisho hao wameweza kukabidhi Padre msimamizi ya Kanisa dogo la magereza Vittorio Trani, rosari zilizo barikiwa na Papa Francisko ambazo alipokea wakati wa ziara yake nchini Thailand kwa lengo la kuwazawadia wenye shida.