Papa Francisko amekutana na Rais wa Mali Bwana Irahimu Boubacar Keita mjini Vatican tarehe 13 Februari 2020 Papa Francisko amekutana na Rais wa Mali Bwana Irahimu Boubacar Keita mjini Vatican tarehe 13 Februari 2020 

Papa Fracisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya nchi ya Mali!

Papa Francisko amekutana mjini Vatican na Rais wa Jamhuri ya Mali, Bwana Ibrahim Boubacar Keïta

VATICAN

Kwa mujibu wa msemaji wa vyombo vya habAri Vatican amethibItisha kuwa Alhamisi 13 Februari 2020, Papa Francisko amekutana katika Jumba la Kitume na Rais wa jamhurI ya nchi ya Mali, Bwana Ibrahim Boubacar Keïta, ambapo mara baada ya mkutano huo pia amekutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akisindikizwa na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na ushirikiano na nchi za nje.

Katika mazungumzo yake na Katibu wa Vatican, yameonesha kuwa  katika hali nzuri na zaidi kuhusu uhusiano mwema baina ya  nchi hizi  pia kuzungumzia juu ya hali za ndani ya Taifa hili kwa namna ya pekee ile ya kibinadamu na usalama, ambao unatishiwa kutokana na kuenea kwa itikadi kali za kidini na kigaidi.

Aidha wamegusia pia baadhi ya masuala ya kikanda na kimataifa, miongoni yakiwa yale ya ukosefu wa usalama wa vyakula katika kanda ya Sahel, matukio ya uhamiaji na jinsi ya kukuza amani katika Afrika ya magharibi.

13 February 2020, 16:02