Habari zilitolewa na Shirika la habari la kimisionari ulimwenguni Fides,zinasema 2019 wamisionari 29 waliuawa na 18 wakiwa ni Mapadre,shemasi wa kudumu mmoja,watawa 2 na walei 6. Habari zilitolewa na Shirika la habari la kimisionari ulimwenguni Fides,zinasema 2019 wamisionari 29 waliuawa na 18 wakiwa ni Mapadre,shemasi wa kudumu mmoja,watawa 2 na walei 6.  

Ripoti ya Fides:Ni wamisionari 29 waliouwawa mwaka 2019!

Habari zilitolewa na Shirika la habari la kimisionari ulimwenguni Fides,zinasema 2019 wamisionari 29 waliuawa na 18 wakiwa ni Mapadre,shemasi wa kudumu mmoja,watawa 2 na walei 6.Hii inaonesha wazi aina ya utandawazi wa vurugu ambao umeripotiwa na idadi kubwa ya vifo imejiorodheshwa katika bara la Afrika!

Na Padre Angelo Shikombe,- Vatican

Baba Mtakatifu Francisko mnamo tarehe 11 Desemba, 2019  alitoa katekesi yake  jijini Vatican juu ya sadaka ya kifodini, kwa maisha ya wakristo na jumuiya zake, ikiwa ni njia ya kumfuata Yesu Kristo.  Kutokana na habari zilitolewa na Shirika la habari la kimisionari ulimwenguni Fides, zinasema wamisionari 29 waliuawa na 18 wakiwa ni Mapadre, shemasi wa kudumu mmoja, watawa 2 na walei 6. Idadi hii inazidi kuwa kubwa barani Afrika ikiashiria ukiukwaji wa haki za binadamu ulimwenguni.

Kutokana na taarifa zilizotolewa na Shirika la habari la kimisionari Fides, Barani Afrika mapadre 12 watawa 2 na mlei mmoja waliuawa mwaka 2019. Barani Amerika mapadre 6 shemasi mmoja wa kudumu, mtawa 1, walei 12 waliuawa. Wakati huohuo huko barani Asia mlei mmoja aliuawa na katika bara la Ulaya mtawa mmoja aliuawa. Mauaji haya yanayozidi kuenea ulimwenguni hayafungamanishwi na chuki dhini ya Imani bali yanatokana na kudorora kwa maisha ya kijamii. Sehemu nyingi yametokea katika mazingira ya kurupushani za machafuko ya kijamii. Kuenea kwa umwagaji damu barani Afrika, Amerika na Asia kunaashiria kuwepo kwa ulegevu katika usimamiaji wa sheria.  

Tabia hii ya ukiukwaji wa haki za binadamu inapaswa kupingwa vikali na Kanisa mahalia kwa kuwa  inalenga kumwondoa kuhani katika jamii. Ijulikane wazi kuwa kumuua kuhani ni zaidi ya mauaji ya mtu wa kawaida na  hali hii ya ugaidi huenea ili kuhalalisha mazingira ya rushwa zinazoendelea. Mifano halisi ni Mauaji ya Padre David Tanko kutoka  Takum Nigeria, aliyeuawa na watu wenye silaha wakati akiwa njiani kuelekea  kijiji cha Takum Nigeria katika kazi za kitume. Pia  mauaji ya kikatili ya kikongwe katika Jamhuri ya Afrika ya kati Sista Inyesi Nieves Sanko aliyekuwa akitoa mafunzo ya biashara kwa vijana.  Mauaji ya Padre Paul Mc Wuley ambaye mwili wake ulikutwa kwenye jumuiya wa wanafunzi wa Salle.

Ushuhuda wa maisha ya kidini ya wamisionari hawa unadhihirisha kuwa walikuwa watu ambao walijibidisha katika maisha ya kila siku ya ushuhuda  wa Injili ya upendo na kutoa huduma iliyopunguza mateso ya wadhaifu na kuinua sauti zao katika ulinzi wa haki zao,  kukemea uovu na dhuluma, kufungua mioyo ya watu kwa matumaini ya Kristo. Baba Mtakatifu Francisko alitoa wito kwa Taasisi za kidini, kisiasa na za kijamii kudumisha ushirikiano, wakitambua kuwa umisionari unahitaji kutoa huduma bora za kiroho na za kijamii kwa watu wote  bila kujali imani, ukabila  na itikadi zao. Huduma zinazotolewa ni pamoja na maisha ya kiroho,  elimu   mashuleni na vituo vikuu na  huduma za afya katika hospitali.

Changamoto kwa wamisionari ni kubwa kwani ni vigumu sana kukusanya orodha ya sensa kwa Maaskofu, makuhani, watawa, wamisionari na walei wakatoliki ambao wameshambuliwa, kupigwa, kuibiwa, kutishiwa  kwa sababu ya imani yao. Hali hiyo inahatarisha usalama wao wenyewe na usalama wa nchi husika, makanisa  yakipochomwa moto, sanamu na picha takatifu kuharibiwa, waamini kushambuliwa wakati wamekusanyika katika  ibada, utekaji nyara wa makuhani na watawa  kwa  baadhi ya mabara unaashiria uvunjifu wa amani.

Padre Paolo alikuwa miongoni mwa wawakilishi wa kikundi cha kiitaliano kiitwacho “Dall'Oglio”, waliotekwa tarehe 29 Julai, 2013 huko Raqqa,  nchini Siria, ambapo pia kumekuwa na tetesi nyingi katika miaka ya hivi karibuni, bila ya uthibitisho wowote. Na huko Colombia mmisionari mtawa Sista Gloria Secilia Narvaez Argoty, alitekwa nyara mnamo Februari 8, 2017.  Baba Mtakatifu Francisko katika mwezi wa kimisionari 2019 amepokea shuhuda nyingi za vifo dini, wamisionari wakishuhudia imani katoliki katika mazingira ya aina tofauti tofauti.  Shirika la habari la kimisionari duniani  Fides, limetoa habari juu ya wito wa Baba Mtakatifu Francisko kwa wabatizwa wote waliofanywa kuwa mwili wa fumbo la Kristo kuendelea kuitetea imani ulimwenguni.

03 January 2020, 15:20