Vatican News
Tarehe 25 Januari 2020 Papa Francisko amekutana na Rais wa Iraq Tarehe 25 Januari 2020 Papa Francisko amekutana na Rais wa Iraq  (AFP)

Papa Francisko amekutana na Rais wa Iraq Bwana,Barham Salih

Papa Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Iraq Bwana, Barham Salih, mjini Vatican ambaye mara baada ya mkutano huo amekutana pia na Kardinali, Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akisindikizwa na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher,Katibu wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na ushirikiano wa Nchi za Nje.

Jumamosi tarehe 25 Januari 2020 Papa Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Iraq, Bwana, Barham Salih, ambaye mara baada ya mkutano huo amekutana na Kardinali, Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akisindikizwa na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vaticani kwa ajili ya Mahusiano na ushirikiano wa Nchi za Nje.

Wakati wa Mkutano wao, viongozi hawa wameonesha uwepo wa  mahusiano mazuri kati ya nchi hizi mbili na kutazama hali halisi ya changamoto za nchi, umuhimu wa kutafuta namna ya kuwa na msimamo na mchakato wa ujenzi kwa upya wa nchi, huku wakiwatia moyo hasa ya kufuata njia ya majadiliano na kutafuta suluhisho linalofaa kwa ajili ya wazalendo na kuheshimu uhuru wa kitaifa.

Wakiendelea na mazungumzo hayo pia wamebainisha juu ya umuhimu wa kulinda uwepo wa historia ya wakristo katika nchi hiyo ambayo ni sehemu fungamani na maana ya mchango ambao unapelekea ujenzi wa jamii nzima na kuonesha ulazima wa kuhakikisha usalama ili kuweza kupata nafasi ya wakati endelevu wa Iraq.

Hatimaye, katika  mazungumzo hayo, viongozi hawa wameweza kujikita juu ya migogoro tofauti na kipeo kikubwa cha kibinadamu kinachoikumba na kuiyumbisha Kanda nzima huku  wakisisitiza juu ya umuhimu wa jitihada zilizokwisha timizwa  kwa msaada wa Jumuiya ya Kimataifa ili kuwa na msimamo wa imani na kuweza kuishi kwa amani.

25 January 2020, 12:48