Tarehe 15 Januari 2020,Papa Francisko amemteua Katibu mpya msaidizi wa Kitengo cha Ofisi ya Ukatibu Mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican,Dk. Francesca Di Giovanni Tarehe 15 Januari 2020,Papa Francisko amemteua Katibu mpya msaidizi wa Kitengo cha Ofisi ya Ukatibu Mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican,Dk. Francesca Di Giovanni 

Mwanamke ateuliwa kuwa Katibu mpya Msaidizi wa Vatican!

Papa Francisko amemteua Katibu Msaidizi katika Kitengo cha Ofisi ya Katibu Mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mjini Vatican,Dk.Francesca Di Giovanni.

Vatican

Tarehe 15 Januari 2020 Papa Francisko amemteua Katibu Msaidizi katika Kitengo cha Ofisi ya Ukatibu Mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican, Dk. Francesca Di Giovanni.  Alizaliwa huko Palermo, Italia tarehe 24 Machi 1953. Amepata shahada ya Sheria na kufanya mazoezi ya uwakili. Amefanya kazi katika mantiki ya sekta ya sheria kwa upande wa utawala katika Kituo cha Kimataifa cha Maria cha Chama cha Kitume cha Wafokolari.

Bi Francesca rasmi amekuwepo katika Ofisi ya Ukatibu Mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa mjini Vatican, tangu  tarehe 15 Septemba 1993. Aidha katika shughuli nyingine, amejikita daima katika huduma ya kitengo cha kimatifa hasa kuhusiana na masuala  ya: wahamiaji na wakimbizi, haki za kibinadamu kimataifa, mawasiliano, sheria binafsi kimataifa, hali za wanawake na mali ya kiakili na utalii.

15 January 2020, 12:32