Vatican News
Kikosi cha wanariadha wa Fiamme Gialle wameawaandalia watoto wadogo na familia zao chakula cha mchana kama ishara ya sikukuu Kikosi cha wanariadha wa Fiamme Gialle wameawaandalia watoto wadogo na familia zao chakula cha mchana kama ishara ya sikukuu  

Mabingwa wa michezo ya olimpiki waandaa chakula kwa ajili ya watoto

Mabingwa wa olimpiki wawandalia chakula watoto na familia zao wa kituo cha afya cha Mtakatifu Marta Vatican ambao wamewakaribisha katika Kituo chao cha wanariadha wa Vatican huko Castelporziano Roma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Haiwezekani usifanye mshikamano wa dhati hata kwa njia ya lugha za dhati na mchezo wa kindugu ambapo wakuu wa michezo kiroho kwa Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu 16 Desemba 2019, Chama cha Riadha Vatican, Chama cha Michezo  , wamesindikiza watoto wanao wahudumia wa kituo cha afya ya watoto Cha Mtakatifu Marta katika Kituo cha wanamichezo cha Fiamme Gialle huko Castelporziano Roma  ili kuweza kuishi siku ya sikukuu kwa kushiriki chakula cha pamoja cha Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana na ili kuweza kugundua siri za washindi wakubwa wa Olimpiki.

Ni wanariadha wenyewe wenye kuwa na medali za olimpiki  na za ushindi wa kidunia  kama vile Tania Cagnotto, Fabrizio Donato na Antonella Palmisano  waliowapokea watoto na familia zao hata kupika chakula cha mchana na kuwahudumia mezani. Ishara nyingine nzuir ilikuwa ni ile ya kuondoa sahani na kuosha vyombo vyote.  Hata hivyo hazikukosekana zawadi kwa ajili ya watoto ikewemo keki kama utamaduni na wakati huo huo wakimtakia mateshi mema Mchezaji mkuu Papa Francisko wakati wa mkesha wa sikukuu yake ya kuzaliwa.

Ni wachazaji hao ho hao ambao hata katika fursa ya Pasaka walikuja Vatican moja kwa moja ili kukutana na familia katika makao ya kituo cha afya cha Mtakatifu Marta, kwa kutoa zwadi ya zana za vitabu vya shule na michezo kwa ajili ya watoto lakini pia hakukosa kuleta mayai ya pasaka kwa watoto hao. Katika mtindo huo mabingwa wa michezo wamewaeleza watoto hata juu  ya siri za michezo yao, na kuwafundisha hata hatua ndogo ndogo za michezo ya kufurahia na wakati huo huo hata mazoezi rahisi ya kunyosha viungo ili kujisikia vema.

Aliyewasindikiza familia na watoto wa kituo cha afya cha Mtakatifu Marta pia alikuwa ni mkurugenzi, Sr Maria Antonietta Collacchi, mwanashirika wa Wana wa Upendo akiwa na watu wa kujietolea. Pamoja nao walikuwa na  wawalikishi wengi wa riadha Vatican na Rais wake Monsinyo Melchor Sánchez de Toca, ambaye ni Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Utamaduni.  Kituo cha afya cha Mtakatifu Marta kinasaidia familia zenye shida hata madawa na mahitaji muhimu ya kwanza kwa ajili ya watoto kama vile maziwa ya unga, pedi vyakula vya watoto hata ikiwezekana kwa wazazi.

Na hii ni hali halisi ambayo tunazungumzia juu ya watoto 350 ambao wanawashughulikia moja kwa moja karibia na watu elfu moja. Lakini zaidi Sista anasema, wanariadha wa vikosi vya ulinzi ndiyo waliomstari wa mbele kuwezesha shughuli ya kujitolea ambapo kila siku wanabailishana zamu ya kuweza kukaa na watoto wadogo na familia zao ambao wanapata namna ya kuweza kubadilishana mawazo. Ni hali halisi ambayo inaendelea kuwa mwafaka na ambayo pia inasisimiwa na Mfuko wa sadaka ya Papa. Na mara nyingi Baba Mtakatifu amependa kuadhimisha Sikukuu yake na watoto hao. Sr  Antonietta, anamaliza kwa kusema leo hii, tunatafuta kuwaokoa familia dhidi ya hatari zinazosukana na soko la ajira nyeusi, madawa ya kulevya na ukahaba.

17 December 2019, 10:28