Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Gàbor Pintèr kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Honduras Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Gàbor Pintèr kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Honduras 

Askofu mkuu Gàbor Pintèr, Balozi wa Vatican nchini Honduras

Askofu mkuu Gàbor Pintèr alizaliwa mwaka 1964 huko Kunszentmárton, Hungaria. Akapadrishwa tarehe 11 Juni 1988. Alianza utume wake wa kidiplomasia mjini Vatican tarehe 1 Julai 1996. Na tangu wakati huo ametoa huduma za kidiplomasia huko nchini: Haiti, Bolivia, Uswiss, Ufaransa, Ufilippini na Aus. Tarehe 13 Mei 2016, akateuliwa kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Belarus.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Gàbor Pintèr kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Honduras. Kabla ya uteuzi huu Askofu mkuu Gàbor Pintèr alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Belarus. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Gàbor Pintèr alizaliwa tarehe 9 Machi 1964 huko Kunszentmárton, Hungaria. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 11 Juni 1988 akapewa daraja Takatifu ya Upadre. Alianza utume wake wa kidiplomasia mjini Vatican tarehe 1 Julai 1996. Na tangu wakati huo ametoa huduma za kidiplomasia huko nchini: Haiti, Bolivia, Uswiss, Ufaransa, Ufilippini na Aus.

Tarehe 13 Mei 2016, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Belarus. Akawekwa wakfu kuwa Askofu mkuu tarehe 15 Julai 2016 na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenye Kanisa kuu la Jimbo Katoliki la Vac, nchini Hungaria. Tarehe 12 Novemba 2019 akateuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Honduras.

Honduras
12 November 2019, 14:54