Vatican News
Tarehe 19 Oktoba 2019 mchana imefanyika Semina kuhusu changamoto za Kanisa la Amazonia na uongozi wa maadili,lililoandalia na mfuko wa Ratzinger Tarehe 19 Oktoba 2019 mchana imefanyika Semina kuhusu changamoto za Kanisa la Amazonia na uongozi wa maadili,lililoandalia na mfuko wa Ratzinger  (Vatican Media)

Semina Vatican:uongozi wa maadili katika huduma ya Nyumba yetu!

Jumamosi tarehe 19 Oktoba mjini Vatican,katika mantiki ya Sonodi ya maaskofu kwa ajili ya Amazonia,imefanyika Semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Vatican wa Joseph Ratzinger-Benedikto XVI ikiongozwa na mada:Changamoto za Kanisa la Amazonia:ushirikiano wa lazima kati ya Mashirika ya kimataifa na Kanisa Katoliki na uongozi wa maadili.Na hatimaye nyimbo na muziki kutoka Bolivia.

Na sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika eneo  kubwa la kuingilia kwenye Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, Jumamosi mchana tarehe 19 Oktoba 2019, ndipo imefanyika Semina katika mantiki ya Sinodi inyaoendelea mjiniVatican. Walioandaa semina hiyo ni pamoja na Sekretarieti ya Sinodi ya Maaskofu kwa ushirikiano na Uwakilishi wa Kudumu wa Vatican Katika Shirika la la Kimataifa  lililopo Roma la FAO,IFAD,PAM, pamoja na Taasisi ya “Razón abierta” ya Madrid, kwa msaada wa Mfuko wa Templeton, katika mantiki ya mradi unaotazama mafunzo kwa ajili ya “Uongozi wa Maadili.” Kama mada inavyojieleza, mbele ya changamoto za Kanda ya Amazonia semina hiyo ni kutaka kusisitizia juu ya umuhimu wa kazi ya pamoja kati ya Mashirika ya Kimataifa na Kanisa Katoliki, huku ikienda sambamba na Wosia wa Baba Mtakatifu  Francisko wa “Laudato si” na  malengo ya Ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu.

Watoa mada:matatizo ni mengi lakini pamoja inawezekana kuyakabili

Mara baada ya salam kutoka kwa Kardinali Lorenzo Baldisseri, ambaye ni Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu amemekaribisha kwa neno la utangulizi kutoka kwa Kardinali Pedro Ricardo Barreto Jimeno,  Rais mwakilishi wa Sinodi na makamu Rais wa Mtandao wa Kanisa la Amazonia (Repam) ili afungue Semina. Matatizo ya kibinadamu ni mengi na ambayo yanaweza kukabiliwa kwa pamoja katika njia ili kutafuta namna ya kuyatatua na vile vile wasiwasi kuhusu sayari yetu isiharibu furaha yetu na matumaini ambayo yanatoka kwake Kristo, ameseka  Kardnali Barretto katika Semina hiyo.

Aidha zimefuata hotuba nyingine kutoka kwa  René Castro-Salazar, Mkurugenzi mkuu mtendaji wa FAO katika Kitendo cha Hali ya hewa, Bioanuwai, Ardhi na Maji; ya  Mattia Prayer Galletti, Mtaalam wa ufundi katika shirika la IFAD na hotuba ya  Francisco Torralba, Profesa, Mtaalamu wa Masuala ya kijamii katika Chuo Kikuu cha Ramon Llull huko Barcellona, nchini Uhispania.Hitimisho lilikuwa na nafasi ya mratibu wa Semina Padre Federico Lombardi, ambaye ni Rais wa Mfuko wa Josefu Ratzinger – Benedikto XVI, na ambaye amewakaribisha pia Monsinyo Fernando Chica Arellano, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika makao ya FAO, IFAD e PAM Roma. Baadaye imefuata tamasha la muziki kutoka kikundi kiitwacho Coros y Orquestra Palmarito & Urubichà, cha nchini Bolivia kilicholetwa makusudi kwa ajili ya Sinodi na mabacho kinafuatilia nyimbo na mziki mahalia kwa siku hizi za Sinodi ya Maaskofu.

Kwanini kuhamasisha hiyo semina

Hata hivyo katika nafasi ya uratibu wa siku hiyo na Padre Lombardi ameleezea ni kwa jinsi gani Mfuko umeweza kuandaaa mkutano huo. Kazi yake ni kuendelea kupanua mada kubwa ya Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI  na  kuonesha mwendelezo kamili na Baba Mtakatifu Francisko, ambapo katika utume wake anaendelea kutafakari mada nyingi sana ambazo zilikuwa tayari zimeanzishwa na mtangulizi wake. Amekumbuka kuwa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI wakati mwingine aliitwa Papa kijani, kwa sababu alihutubia  hotuba nyingi kuhusiana na kazi ya uumbaji, ambayo ni masuala yanayopanuliwa sana na Baba Mtakatifu Francisko.

Uwezekano wa kujifungulia utashi wa sera za kisiasa ili kuokoa sayari

Na katika hotuba yake Bwana René Castro-Salazar wa  FAO amesisitiza kwamba watu wote, binafsi na Mataifa lazima yahisi kuhusika katika mabadiliko kwa ajili ya kuokoa dunia. Uwezekano wa kufanya hivo upo amesisitza zaidi  huku akitaja mfano wa matendo hai mema katika mada ya mazingira yaliyo chukuliwa na nchi kama ya  Chile na Costa Rica. Uwezekano wa ufundi kwa ajili ya kubadili  na kufanya mapambano katika kukabiliana na madiliko ya tabianchi yapo amerudia , na kwamba kinachotakiwa ni utashi wa sera za kisiasa ili kufanya hivyo. Na kwa maana hiyo kuna hitaji  la ushirikiano wa wote na mataifa katika mabara yote na ni lazima hata kwamba binadamu aweza kurudi kuwa ndiyo kitovu cha michakato yote ya maisha yanayoguzia nyumba yetu ya pomoja.

 

21 October 2019, 09:36