Mababa wa Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia wanajiandaa kutoa Nyaraka za Sinodi na hatimaye, kufunga rasmi sehemu ya kwanza ya maadhimisho haya, Jumapili 27 Oktoba 2019. Mababa wa Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia wanajiandaa kutoa Nyaraka za Sinodi na hatimaye, kufunga rasmi sehemu ya kwanza ya maadhimisho haya, Jumapili 27 Oktoba 2019. 

Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia: Nyaraka za Sinodi 2019

Sinodi imetoa kipaumbele cha pekee kwa: Shughuli za Kichungaji, Kitamaduni, Kisiasa na Kiekolojia; mambo yanayo ambatana na kukamilishana. Mababa wa Sinodi wamepembua changamoto hizi kwa kutumia jicho ya Mitume wa Yesu. Sinodi hii ni amana, utajiri na zawadi kubwa ya Roho Mtakatifu kwa Kanisa Ukanda wa Amazonia. Licha ya kujikita katika wongofu wa shughuli za kichungaji!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia kuanzia tarehe 6 yanatarajiwa kufungwa rasmi tarehe 27 Oktoba, 2019 kwa Ibada ya Misa Takatifu itakayoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kuanzia saa 4:00 Asubuhi kwa saa za Ulaya. Sinodi hii imeongozwa na Kauli mbiu: “Amazonia: njia mpya ya Kanisa na kwa ajili ekolojia fungamani”. Mababa wa Sinodi kwa sasa wamepitia na kujadili na hatimaye kupitisha Hati ya Maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia kwa Mwaka 2019. Mapendekezo yatakayotolewa kwa Khalifa wa Mtakatifu Petro yatapigiwa kura Jumamosi.

Hii ni Sinodi ambayo imetoa kipaumbele cha pekee kwa mambo makuu manne: Shughuli za Kichungaji, Kitamaduni, Kisiasa na Kiekolojia; mambo yanayo ambatana na kukamilishana. Mababa wa Sinodi wamepembua changamoto hizi kwa kutumia jicho ya Mitume wa Yesu. Sinodi hii ni amana, utajiri na zawadi kubwa ya Roho Mtakatifu kwa Kanisa Ukanda wa Amazonia. Licha ya kujikita katika wongofu wa shughuli za kichungaji na kimisionari, lakini pia ni Sinodi ambayo imejikita kwa kiasi kikubwa na mchakato wa utunzaji wa mazingira nyumba ya wote, tema inayohitaji pia wongofu wa kiekolojia. Majadiliano ya kidini na kiekuemene ni sehemu ya vinasaba vya maisha na utume wa Kanisa. Sinodi maana yake ni mchakato wa Kanisa kutembea kwa pamoja, “Kairos”, ili kujipatanisha na Ukanda wa Amazonia kwa kuendelea kujikita katika mchakato wa kuziinjilisha tamaduni ili kuitamadunisha Injili; kwa kusimama kidete ili kukazia ekolojia fungamani.

Sinodi 2019

 

25 October 2019, 16:15