Leo hii,katika maisha ya kila siku,tunawezaje kutii amri ya kwenda ulimwenguni kote na kutangaza Injili kwa kila kiumbe? Ni swali alilouliza Kardinali Parolin kwa wanakarisimatiki! Leo hii,katika maisha ya kila siku,tunawezaje kutii amri ya kwenda ulimwenguni kote na kutangaza Injili kwa kila kiumbe? Ni swali alilouliza Kardinali Parolin kwa wanakarisimatiki! 

Kardinali Parolin azungumzia kazi ya Unjilishaji:bila usikivu wa Mungu hakuna uinjilishaji!

Leo hii,katika maisha ya kila siku,tunawezaje kutii amri ya kwenda ulimwenguni kote na kutangaza Injili kwa kila kiumbe?Ni swali alilouliza Kardinali Parolin wakati wa Misa Takatifu kwa washiriki wa Mkutano wa 42 wa Kanda ya Uuisho wa Roho Mtakatifu mkoani Campagana Italia,13 Oktoba 2019 na kufafanua kazi ya uinjilishaji na kuwa bila usikivu wa Mungu na matendo ya kimisionari,hakuna uinjilishaji.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Bila usikivu wa Mungu hakuna utume na kwa maana hiyo ni lazima kujifunza daima kwa upya kuanzia na Yesu sanaa ya Uinjilishaji na ili kutoweza kuangukia kwenye udanyanyifu ambao unaleta suluhisho la kibinadamu katika matatizo ya ulimwengu na kuyaona ni bora zaidi  kuliko yake. Aidha, uinjilishaji siyo  suala la kufanya kampuni binafsi, bali ni uzoefu na ushuhuda wa Kanisa linalomwilishwa na Injili. Amesisitiza hayo Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican, Domenika  tarehe 13 Oktoba 2019 kwa washiriki wa Mkutano wa 42 wa Kanda ya  makundi ya  jumuiya ya Uuisho wa Roho Mtakatifu mkoani Campagna nchini Italia.

Kardinali Parolin katika tafakari yake, amaweza kugusia hata mada ya Mwezi Maalum wa Kimisionari, inayoongozwa na kauli mbiu, “mmebatizwa na kutumwa: Kanisa la Kristo katika utume duniani”, pia kuongoza Misa Takatifu. Kwa washiriki wa mkutatano huo Kardinali amewapa hata salama kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko huku akiwaakikishia uwepo kiroho na sala karibu nao na kuwatumia baraka, na kama ilivyo kawaida yake amewaomba hata wao wasali kwa ajili yake ili Bwana aweze kumwangazia zaidi na kumsaidia daima katika utume wake. Akikumbusha juu ya mwezi Maalum wa Kimisionari na ambao unaadhimisha kumbukumbu ya miaka 100 tangu kutangazwa kwa Wosia wa Kitume Papa Benedikto XV kunako tarehe 30 Novemba 1919, amesisitizia juu ya umakini wa kuzingatia kwa ajili ya kupyaisha matendo ya kimisionari ya Kanisa huku akikumbusha kile kipindi cha vita ya kwanza ya Dunia hadi kufikia Mtaguso wa II wa Vatican. Wosia huo, amebainisha, uliweza kutoa mchango mkubwa na wenye maana wa kuweza kubadili mtazamo wa hali halisi wa umisionari katoliki duniani kwa wakati ule, ambapo hadi wakati ule  wamisionari duniani, walionekana ni wawakala wa wakoloni na ambao walikuwa akisaidia maslahi ya kisiasa na nguvu za wageni; na kumbe wosia huo ukawafanya watambue kinyume chake kwamba umisionari ni matendo hai  na halisi ya Kanisa linalobubujika uhai wake kutoka katika Injili.

Kadhalika katika kurudia pendekezo linalotolewa katika Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya Siku ya Kimisionari duniani  ambayo itaadhimishwa tarehe 20 Oktoba 2019, Kardinali Pietro Parolin  amethibitisha kwamba, bila usikivu wa mara kwa  mara kwa Mungu, utume, haupo, vile vile  kama ilivyo kwamba, bila kukubali na kujikita katika matendo hai ya  mazoezi ya kimisionari usikivu wa kweli wa Mungu haupo! Hatua ya kuanzia ameshauri ni ile fupi hasa ya Neno la Yesi ambalo linatolewa katika Injili ya Marko  (16, 15): Enendeni dunianikota mtaitangaze Injili kwa kila kiumbe. Akifafanua hilo anasema kiini cha kwanza  ni Yesu na cha pili ni ulimwengu; cha tatu ni Injili na kwa maana hiyo tunaweza kusema kwamba kati ya mambo matatu  makuu msingi linakosekana moja,uzoefu wa kikristo siyo mkamilifu na wala kukomaa. Hata hivyo maneno ya Mtaguso, hata ya Mtakatifu Agostino, Mtakatifu Paulo VI, Mtakatifu Yohane Paulo II, Baba Mtakatifu Francisko, Karl Barth na Aleksandr Solženicyn wamesindikiza tafakari ambayo imepelekea kuwa na swali kuu alilouliza  Kardinali Parolin kwamba : “Leo hii, katika maisha ya kila siku, tunawezaje kutii amri ya kwenda ulimwenguni kote na kutangaza Injili kwa kila kiumbe?"

Hata hivyo kwa kutazama masomo ya liturujia ya siku katika mahubiri yake, Kardinali Parolin, kwanza kabisa amesisitiza kwamba Kanisa katika kusikiliza Neno kila wakati linasaidia na kuokoa dhidi ya  mawazo na kufungwa katika malimwengu na mara zote tena Neno linamfanya awe mwanafunzi na sakramenti ya ufalme wa Kristo katika ulimwengu huu. Katika kutazama sura ya wakoma ambao wameelezwa katika Injili ya Mtakatifu Luka, Kardinali Parolin amefananisha na wale wote ambao leo hii wamepotoshwa na kudharauliwa na jamii ambayo, kama ilivyokuwa miaka elfu mbili iliyopita, inajaribu kuepuka kushughulikia  wale ambao hawana njia ya matibabu, jamii ambayo inawanyanyasa wanyonge, zaidi ya hayo, inaamini inaweza kujitetea dhidi yao na inanyanyapaa hali zao. Kinyume na yale ambayo Mungu hufanya, ni Baba mwenye huruma; kinyume na yale ambayo Yesu hufanya: yeye husimama na kuwape umakini wake. Ni kitu ambacho hakihusu kile kinachomtazama tu anachofanya, bali ni yeye na ndiyo mtindo wake Yesu.

 

18 October 2019, 15:45