Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican Paolo Ruffini,ameandikia dibaji katika kitabu cha mwandishi Monica Mondo nyenye jina la "Mahali ambapo roho inafika" Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican Paolo Ruffini,ameandikia dibaji katika kitabu cha mwandishi Monica Mondo nyenye jina la "Mahali ambapo roho inafika" 

Dibaji ya Dk.Ruffini katika Kitabu cha Monica Mondo:mahali ambapo roho inafika!

Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican,Bwana Paolo Ruffini ameandika dibaji katika Kitabu cha Monica Mondo,chenye kichwa,“mahali ambapo roho inafika."Monika ni mwandishi na mwendesha kipindi cha Soul,katika Luninga ya Baraza la maaskofu Italia.Katika dibaji,Ruffini anasisitiza umuhimu wa kutoa nafasi ya simulizi halisi,subira,kuelewa,kushuhudia na kuepuka haraka na uongo!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican Bwana Paolo Ruffini ameandika dibaji katika Kitabu cha Monica Mondo, chenye kichwa “mahali ambamo roho inafika”. Bi Monika ni mwandishi na mwendesha kipindi cha “Soul” katika Luninga ya  Baraza la Maaskofu  Katoliki Italia. Katika dibaji hiyo Bwana Ruffini anasema, “Iwapo kuna wito wa uandishi, kila mwandishi bila shaka ni yule mwenye kusimulia hali halisi; kusaidia kutambua namna ya kuona mambo ambayo wengine hawaoni, kutaofautisha  kati ya ukweli na uongo, kutoa maneno yenye kushuhudia zaidi ya yale yanayo danganya. Na ili kutosaliti wito huo kama mwandishi, inahitajika muda, yaani kuwa na muda wa kutafuta na kuelewa; inahitajika muda wa lazima; na kwa hakika muda unahitajika bila kuwa na haraka.

Kuna tabia ambayo inazuia kutazama ukweli

Bwana Riffini anatoa mfano wa kweli ya kwamba kuna tabia kwa hakika ambayo inazuia kutazama ukweli wa mambo na ambayo inatufanya kubadilisha ule ujuujuu wa kitu. Hii ina maana ya kutembea katika dunia kwa kufikiria tayari unajua kila kitu, na hukijifungia juu ya hukumu binafsi; Hii ina maana ya kutotaka kuchukua muda wa lazima ili kuweza kukutana, kwa ajili ya kujua, kwa ajili ya kung’amua na hata kujua ya wengine, na   historia yetu ya pamoja kwa sababu ili kuweza kutambua jambo ambalo linatuwezesha kufikia umoja wa lazima uliotiwa chachu ya kweli.

Jambo gani linaleta changomoto ya mawasiliano?

Bwana Ruffini akiendelea na maelezo yao ameandika kuhusu  kile ambacho kinaleta changamoto ya mawasiliano duniani, kama vile Baba Mtakatifu Francisko anavyothibitisha kuwa ni ukosefu wa uwezo wa kutazama na kusikiliza kabla ya kunena; na hili ndiyo jambo muhimu la kuchagua njia iliyo ndefu ya uelewa, badala ya ile fupi inayotolewa na watu kana kwamba wana uwezo wa kusuluhisha shida zote, au kinyume chake kama vile ni wapelelezi ambao unauwezo wa kupewa jukumu lote juu yao.  Lakini  ili kuwajua watu, Bwana Ruffini amesema, ni lazima ukutane na mmoja, mmoja. Kwa sababu hii, mahojiano ya Monica Mondo yana  nafasi yanye thamani kwa maana kwamba hana pumzi fupi kwa mkimbiaji anayateka kufupisha muda, lakini  mwenye pumzi ya utulivu kwa wale ambao huchukua muda unaohitajika ili kuweza kufikia ukweli. Na katika mantiki hiyo ya makutano, hadithi na tafsiri ya maisha, kipindi cha Soul ambacho kwa pamoja walikianzisha Yeye na wengine kwa  miaka iliyopita katika Luninga ya Baraza la Maaskofu Italia (Tv2000), ambayo hata leo hii kinaendelea katika  masafa, na kusimulia asili na tabia ya Monica,  kama mtukutu, mkalimani mzuri na mnyenyekevu wa sanaa ya televisheni ya mazungumzo, ambayo huleta faraja wakati na nafasi ili kuhakikisha kuwa historia ya kibinadamu inazungumza na mtu yeyote na kutajirisha maisha ya ndani ya kila mtu. Na Hasa kwa sababu hiyo  ameongeza kuandika, walikuwa wamefikiria “Soul” yaani “roho” kama jina bora kwa safu nzima ya vipindi na kwa bahati imefanikiwa.

Lengo la mahojiani ni kuleta ukweli wa ndani kwa wanaokubali kukaa katka kiti na mwandishi

Hata hivyo amebainisha kuwa, kile walichokuwa wanatafuta siyoo mahojiano, bali  mazungumzo na moyo wazi, ukilenga kuleta ukweli wa ndani ya wale ambao wangekubali kukaa kwenye kiti, mbele ya wachukua picha na mwandishi wa habari bila ubaguzi. Hii ilikuwa kwamba  awe ni mwanamke au mwanamme, mtu mashuhuri katika kipindi cha show, maarufu kiakilia na kitaaluma, mhusika wa amaisha ya umma, msanii au mmisionari, kwa maana ya wazo kwa hakika lilikuwa ni kutoa mwanzo wa makutano. Kwa njia hiyo, Bwana Ruffini amethibitisha kwamba, Monica Mondo amewapatia zawadi hii. Amewafanya kujua, na   ukaribu kana kwamba walikuwa karibu naye, kimwili, watu ambao wameweka ahadi ya maisha yao yote kwa nguvu  ya dhaifu ya Yesu Kristo, nguvu ambayo inabadilisha maisha ya wale wanaokubali kukutana naye kupitia ushuhuda wa udhaifu. Aidhaanaongeza kuandika:Sisi “Tunapaswa kubaki tu bila silaha na kushangazwa na miujiza ambayo Injili leo hii bado inaweza kutenda maajabu kwa wamisionari wote katika pande zote zilizo za mbali za dunia huku wakikutana kwa mara nyingine tena wakithibtishwa kwamba Mungu hutangulia kila wakati, na upendo ni wenye nguvu  zaidi hofu na uzima una nguvu dhidi ya kifo!

29 August 2019, 12:51