Vatican News
Mheshimiwa Padre Jean Pascal Andriantsoavina ameteuliwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki Antananarivo nchini Madagascar Mheshimiwa Padre Jean Pascal Andriantsoavina ameteuliwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki Antananarivo nchini Madagascar  (AFP or licensors)

Padre Jean P. Andriantsoavina ateuliwa kuwa Askofu msaidizi

Askofu mteule Jean Pascal ANDRIANTSOAVINA alizaliwa tarehe 24 Machi 1969 Jimbo Katoliki la Mahanja. Katika maisha na utume wake, amewahi kuwa Paroko-usu; Mlezi wa vijana Jimbo kuu la Antananarivo na kuanzia mwaka 2003 - 2007 akapelekwa kujiendeleza kwa masomo ya juu kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian na kujipatia Shahada ya uzamili katika Biblia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Mheshimiwa sana Padre Jean Pascal ANDRIANTSOAVINA wa Jimbo Katoliki la Antananarivo kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Antananarivo nchini Madagascar. Katika maisha na utume wake, amewahi kuwa ni Gombera wa Seminari kuu ya Falsafa ya Antsirabè. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Jean Pascal ANDRIANTSOAVINA alizaliwa tarehe 24 Machi 1969 Jimbo Katoliki la Mahanja. Katika maisha na utume wake, amewahi kuwa Paroko-usu; Mlezi wa vijana Jimbo kuu la Antananarivo na kuanzia mwaka 2003 hadi mwaka 2007

Baadaye akapelekwa na Jimbo lake kujiendeleza kwa masomo ya juu kwenye Taasisi ya Sayansi ya Biblia, Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian kilichoko mjini Roma ambako alifaulu kujipatia Shahada ya uzamili katika Sayansi ya Maandiko Matakatifu. Kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2011akateuliwa kuwa ni Mwalimu wa Taaluma, Seminari kuu ya Falsafa huko Antsirabè. Kuanzia mwaka 2011 hadi mwaka 2019 akateuliwa kuwa ni Gombera wa Seminari kuu ya Falsafa huko Antsirabè. Kuanzia Mwezi Machi 2019 amekuwa akishiriki shughuli mbali mbali za kichungaji Parokiani pamoja na kutafsiri Biblia kwenye lugha ya Kimalgasi.

Antananarivo
08 July 2019, 15:33