Vatican News
Askofu Rosario Saro Vella, S.D.B. ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Askofu mèya wa Jimbo Katoliki la Moramanga kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Askofu wa Jimbo la Ambanja, Madagascar. Askofu Rosario Saro Vella, S.D.B. ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Askofu mèya wa Jimbo Katoliki la Moramanga kabla ya uteuzi huu alikuwa ni Askofu wa Jimbo la Ambanja, Madagascar.  (ANSA)

Askofu Rosario Saro Vella ateuliwa kuwa Askofu wa Moramanga!

Askofu Rosario Saro Vella alizaliwa kunako tarehe 8 Mei 1952 huko Canicatti, nchini Italia. Baada ya masomo, malezi na majiundo yake ya Kikasisi na Kitawa, akapewa Daraja takatifu ya Upadre hapo tarehe 27 Mei 1979. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kunako tarehe 7 Novemba 2007 akamteuwa kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Ambanja na kuwekwa wakfu tarehe 16 Desemba 2007.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Rosario Saro Vella, S.D.B. kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Moramanga, nchini Madagascar. Kabla ya uteuzi huu, Askofu Rosario Saro Vella alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Ambanja, Madagascar. Itakumbukwa kwamba, Askofu Rosario Saro Vella alizaliwa kunako tarehe 8 Mei 1952 huko Canicatti, nchini Italia.

Baada ya masomo, malezi na majiundo yake ya Kikasisi na Kitawa, akapewa Daraja takatifu ya Upadre hapo tarehe 27 Mei 1979. Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kunako tarehe 7 Novemba 2007 akamteuwa kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Ambanja na kuwekwa wakfu tarehe 16 Desemba 2007. Hatimaye, Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 8 Julai 2019 akamteuwa kuwa ni Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Moramanga.

Papa: Moramanga
08 July 2019, 15:19