Uwakilishi wa Instrumentum laboris kwa ajili ya Ukanda wa Amazoni ni kwa ajili ya kusikiliza na Kanisa kilio cha watu Uwakilishi wa Instrumentum laboris kwa ajili ya Ukanda wa Amazoni ni kwa ajili ya kusikiliza na Kanisa kilio cha watu 

Instrumentum Laboris kuelekea maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu ya Ukanda wa Amazonia

Katika kuelekea maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu ya Ukanda wa Amazonia itakayofanyika mjini Vatican kuanzia tarehe 6-27 Oktoba 2019 kwa kuongozwa na kauli mbiu “Amazonia:njia mpya ya Kanisa na kwa ajili ya ekolojia fungamani”, tarehe 7 Juni wamewakilisha kwa waandishi wa habari juu ya Hati ya maandalizi ya Sinodi “kusikiliza pamoja na Kanisa kilio cha watu”.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Dunia ya Amazonia inaomba Kanisa liwe na mshikamano wake ili maisha kamili ya Yesu aliyekuja kwa ajili hiyo duniani yaweze kuwafikia wote hasa maskini. Huu ndiyo moyo wa Hati ya kitendea kazi (Instrumentum Laboris) iliyotangazwa asubuhi tarehe 17 Juni 2019 na Sekratarieti ya Maaskofu wakati wa uwakilishaji wake kwa waandishi wa habari. Hii ni kutokana na kuelekea maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu ya Ukanda wa Amazonia itakayofanyika mjini Vatican kuanzia tarehe 6-27 Oktoba 2019. Hati hiyo ni tunda la mchakato wa kusikiliza ulionzishwa tangu ziara ya Baba Mtakatifu Francisko huko Puerto Maldonado nchini  Perù kunako Januari 2018 na kufuatia na ushauri wa watu wa Mungu katika Kanda yote ya amazonia kwa mwaka mzima na kuhitimishwa na Mkutano wa Baraza la Maaskofu  kabla ya Sinodi ulifanyika mwezi Mei mwaka huu.

Kusikiliza kilio cha watu;hadi kupumua mapenzi ambayo Mungu anaomba

Eneo la Amazonia linachukua sehemu ya nchi ya Brazil, Bolivia, Perù, Equador, Colombia, Venezuela, Guyana, Suriname na Guyana ya kifaransa, katika eneo lenye milioni 7,8 ya kilometa za mraba, katika moyo wa Amerika ya Kusini. Misitu ya Amazonia inafunika karibia milioni 5,3 ya kilometa za mraba ambazo zinawakilisha asilimia 40 ya eneo la dunia ya misitu ya kitropiki.

Sehemu ya kwanza ya Hati ya kitendea Kazi

Sehemu ya kwanza ya Hati ya kitendea kazi “Sauti ya Amazonia” inawakilisha hali halisi ya eneo na  watu wake. Inaanzia na maisha na uhusiano wake, maji na mito ambayo yanatitirika kama mishipa ya uoto wa ardhi hiyo na kama chemi chemi za watu wake, utamaduni wake na ufafanuzi wake wa  kiroho unaojiwakilisha  hata katika uasili wake. Hii ni maisha na utamaduni wa maelfu na maelfu ya jumuiya za watu wa asilia, wananchi, wazalendo wenye asili ya afrika, watu wanaoishi karibu sana na mito na katika miji.

Hatari ya maisha na ufungamanisho

Maisha ya Amazonia yamehatarishwa na uharibifu na unyonyaji wa mazingira, mfumo wa ukiukwaji wa haki msingi za binadamu wa watu wa Amazoni. Hii ni kwa namna ya pekee ukiukwaji wa haki za watu asilia, kama vile haki ya maeneo yao, kujitigemea, mipaka ya eneo, mapendekezo na idhini. Kwa mujibu wa jumuiya ambazo zilipata fursa ya kushiriki Sinodi ya kusikiliza, hatari ya maisha inatokana na maslahi ya kiuchumi na kisiasa ya sekta kubwa za jamii zinazotawala leo hii, kwa namna ya pekee makampuni ya uchimbaji madini. Kwa sasa, kuna mabadiliko ya hali ya hewa, kuongezeka kwa uharibifu kwa njia ya mikono ya wanadamu kama vile (kukata miti hovyo, kuchoma moto kiholela, mabadiliko ya kutumia ardhi), hayo yote ni mambo ambayo yanapelekea kwa hakika kutokurudi kwa Amazonia kwa viwango vya juu kwa sababu ya ukataji miti hovyo, kuhamisha kwa nguvu watu na uchafuzi wa mazingira na kuweka mazingira yake katika hatari, hata shinikizo kwenye tamaduni zao.

Sehemu ya pili ya instrumentum laboris: mazingira fungamani na masikini

Katika sehemu ya Pili ya Hati ya kitendea kazi inajikita kutazama na kutoa ushauri kwa ajili ya masuala yanayohusiana na mazingira fungamani. Hati inaeleza kuwa, Amazonia leo hii ina uzuri uliojeruhiwa na kubadilishwa; ni  eneo la uchungu ambalo limetumiwa kwa nguvu kwa mujibu wa msisitizo wa ripoti ya Kanisa mahalia iliyopokelewa na Sekratarieti ya Sinodi .

Kutumia nguvu na kuenea kwa fujo  na rushwa

Katika Hati hiyo inaonesha kuwa eneo la Amazonia limegeuka kuwa nafasi ya mapigano na maangamizi ya watu, utamaduni na kizazi. Kuna aliyelazimika kuacha ardhi yake na wengi wanaangukia katika mitandao ya kihalifu, biashara ya madawa kulevya, biashara haramu ya binadamu (zaidi wanawake), kazi za suruba na ukahaba wa watoto. Ni hali halisi ya kutisha na nguvu ambayo iko nje ya sheria na haki.

Eneo  la Matumani na namna ya kuishi vizuri

Hati hiyo lakini inasema kuwa watu asilia wa Amazonia wanayo mambo mengi ya kutufundisha. Tunatambua kuwa maelfu na  na melfu ya miaka wameweza kutunza ardhi yao, maji na misitu,na wameweza kuhifadhi hadi leo hii, ili binadamu aweze kunufaika kwa furaha ya zawadi ya bure ya kazi ya uumbaji. Safari mpya za uinjilishaji lazima ijengwe katika majadiliano kwa kupitia katika  hekima za mababu hao wanooneshwa katika mbegu ya Neno. Sinodi ya Amazoni itakuwa ishara ya matumani kwa ajili ya watu wa amazonia na kwa ajili ya ubinadamu wote

Watu wa pembezoni

Katika hati ya kitendea kazi Instrumentum Laboris, inaonesha hata kazi ya watu wa asilia katika hati iitwayo (Kutengwa kwa kujitolea PIAV).  Kwa mujibu wa takwimu za Taasisi ya Kanisa maalum (kwa mfano, CIMI) na nyingine, katika eneo la Amazonia kuna watu walio huru  ambao ni kati ya 110 na 130  wanaoishi katika pembezoni mwa jamii au mara chache wanaweza kuwasiliana nao. Hawa lakini ni waathirika katika  hatari ya kujikuta katika biashara mbaya ya madawa ya kulevya na mipango ya miundombinu mikubwa yenye shughuli haramu zinazohusiana mitindo isiyo faa ya kuleta maendeleo.

Watu wa Amazonia kutoka nje,kuhamia mijini na kuacha misitu

Hati pia inaonesha kwamba Amazonia ni kati ya kanda ambayo  sehemu kubwa kuna mzunguko wa  ndani na kimataifa katika Bara la Amerika ya Kusini. Kwa mujibu wa takwimu ya watu wa ndani kabisa ya Amazonia, mzunguko umeongezeka kwa namna ya ajabu; kwa sasa ni kati ya asilimia 70-80 ya  ambao wamekwenda kuishi katika miji na wanaingia mjini kwa namna ya kudumu, kuliko watu ambao wanahama kuingia ndani kabisa ya misitu na wakati huo huo watu hao hawana uwezo wa kupata huduma msingi ya mahitaji. Hata kama Kanisa limeweza kusindikiza wimbi la wahamiaji  hao,  wameacha ndani ya amazonia pengo la kichungaji ambalo lazima liweze kutulizwa! Hati hiyo inasisitiza.

Unabii wa Kanisa la Amazonia: changamoto na matumaini

Hatimaye sehemu kubwa ya Hati ya kitendea kazi (Instrumentum Laboris) inajikita kuwaalika mababa wa Sinodi ya Amazonia ili kujadili sehemu ya pili  ya tema iliyopendekezwa na Baba Mtakatifu  Francisko yaani “safari mpya kwa ajili ya Kanisa katika Kanda”. Hali ya Makanisa mahalia inahitaji “Kanisa hai ambalo linajiwakilisha sasa katika maisha ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, utamaduni na mazingira ya wakazi wake. Kanisa inalokaribisha hata tofauti za utamaduni, kijamii na mazingira kwa ajili ya kuweza kutoa huduma bila ubaguzi wa mtu au vikundi; Kanisa bunifu ambalo linatambua kusindikiza watu wake katika kujenga na kutafuta majibu mapya ya mahitaji ya dhaurura; na Kanisa la maeelewano, linalotambua kuhamasisha amani, huruma na muungano.

Sakramenti na ibada za watu; maono ya ulimwengu

Jumuiya zina shida ya kuadhimisha Ekaristi kutokana na ukosefu wa makuhani. Kanisa linaishi Ekaristi na Ekaristi inajenga Kanisa. Kwa maana hiyo, badala ya kuanza na jumuiya bila Ekaristi inahitajika kubadili mantiki ya uchaguzi, hasa kwa kuwaandaa wahudumu waliokubaliwa kusheria ili kuweza kuadhimisha Ekaristi. Jumuiya inaomba kwa kiasi kikubwa kuthaminiwa, kusindikizwa na kuhamasishwa ibada za watu masikini na urahisi wa kujieleza imani yao kwa njia ya picha, ishara za tamaduni na baadhi ya sakaramenti ambazo zinaonesha hekima na tasaufi inayoundwa kwa hkika na eneo ka kitaalimungu kwa nguvu ya ukuu wa kuinjilisha. Kutokana na hiyo , ushauri ni kwamba, kama kungekuwapo na uwezekani wa kuwa na fursa ya ushauri wa kutafakari tena wazo la  mamlaka ya serikali (nguvu za serikali)kwamba   lazima zihusishwe katika maeneo yote(sakramenti, mahakama, tawala) kwa namna ya kufanya Sakramenti ya ushemasi wa kudumu

Huduma mpya kukidhi haja ya umbali wa utoaji huduma

Zaidi ya wingi wa utamaduni ndani ya eneo la Amazonia kuna  umbali mkubwa ambao unasababisha matatizo makubwa ya kichungaji na ambayo hayawezi kupata suluhisho kwa njia ya zana  za ufundi na teknolojia, inaleza hati hiyo. Kwa maana hiyo ushauri ni kwamba, ni lazima kuhamasisha miito mahalia ya wanaume na wanawake katika kutoa jibu la mahitaji ya umakini wa sakramenti ya kichungaji. Mchango wao kwa dhati ni hatua kubwa ya kuweza kuinjilishi kwa mtazamo wa watu asilia, kwa mujibu wa matumizi yao ya mila na desturi. Hii ni kwamba ,watu asilia waweze kuhubiri watu wao wa asili kwa kina, ule uwelewa wa utamaduni wao na lugha yao, uwezo wa kutangaza ujumbe wa Injili kwa nguvu na udhati kwa yule aliye na sanduku zito la utamaduni wao. Ni lazima kupitia kutoka Kanisa linalotembea ili kufika katika Kanisa linalobaki katika kusindikiza na kama uwepo wake kwa njia ya wahudumu ambao wanabaki na watu wao wenyewe. Hata hivyo katikam kuthibitisha juu ya useja kuwa ni zawadi kwa ajili ya Kanisa, na inahitajika katika eneo la kanda za mbali,wanasema  kuna haja ya kujifunza kwa namna ya kuona jisni gani ya uwezekano wa kutoa wakfu wa kikuhani hasa kwa watu walio wazee  ambao ni wa asilia, wanao heshimika na kukubalika na jumuiya yao. Ingawa wanaweza kuwa tayari na familia  yao imara, lakini ili waweze kuhakikisha sakramenti zinazowasindikiza na  kuwasaidia katika maisha ya Kikristo.

Nafasi ya mwanamke

Katika Hati (Instrumentum Laboris) hata hivyo wameomba kutambua ni aina gani ya huduma maalum ambayo inaweza kufanuliwa kwa upande wa wanawake kwa kuzingatia  nafasi msingi ambayo leo hii Kanisa linatoa katuka eneo la Amazonia. Wanaomba kutambua wanawake kuanzia na karama na talanta zao. Wanaomba kurudisha nafasi aliyotoa Yesu kwa wanawake; mahali ambapo wote /wake kwa waume wanaweza kukutana kwa pamoja”. Wanapendekeza pia kuhakikisha hata uongozi wao na zaidi kuwa na nafasi kubwa, katika kambi za mafunzo ya kitaalimungu, katekesi, liturujia, shule ya imani na kisiasa.

Maisha ya  kitawa

Katika Hati ya kitendea kazi, (Instrumentum Laboris) wanapendekeza kuhamasisha maisa ya kitawa mbadala na kinabii, kuhusu ushirikisho wa mashirika kikanda na baina ya taasisi kwa namna ya uwezekano wa kukaa mahali ambapo hakuna mtu anayetaka kukaa huko au kukaa na yule ambaye hakuna mtu anayependa kukaa naye. Pia wanahimizia kuwa mafunzo ya maisha ya kitawa yanayojuishwa na mchakato wa mafunzo kwa kuzingatia juu ya wingi wa utamaduni, utamadunisho na mazungumzo kati ya tasaufi na maono ya dunia ya Amazoni.

Uekumene

Hati ya kitendea kazi (Instrumentum Laboris, Sauti ya Amazonia) aidha inaonesha hata umuhimu wa tukio la kuzingatia hasa kufikira juu ya ongezeko haraka la makanisa ya kiinjili yenye asili ya kipentekoste, hasa hasa katika maeneo ya pembezoni. Hali hiyo inaonesha kwa namna moja kwamba Kanisa lipo mahali ambapo watu wanahisi kuwa mstari wa mbele na mahali ambamo waamini wanaweza kujifafanua kwa huru bila kifungwa, bila udhibiti, sheria  au mafundisho ya ibada

Kanisa na mamlaka : safari ya msalaba na ushihidi

Namna ya kuwa  Kanisa katika Ukanda wa Amazonia kwa njia halisi ina maana ya kuweka tatizo la nguvu ya kinabii juu ya mamlaka, kwa sababu katika eneo hili watu hawana fursa ya kudai haki zao dhidi ya makampuni makubwa ya kiuchumi na taasisi za kisiasa, inathibitisha hati hiyo.  Leo hii kuweka mjadala wa mamlaka ya utetezi wa eneo na haki za binadamu ni kuhatarisha  maisha binafsi na kufungua njia ya msalaba na kufodini. Wanatoa mifano kwamba, kuna idadi kubwa ya wafiadini huko Amazonia (kwa mfano nchini Brazili kati ya  2003 na  2017, watu wa asilia 1.119 wameuwawa kwa sababu ya kutetea eneo lao). Kwa maana hiyo, Kanisa haliwezi kubaki tofauti na hayo inasema Hati ya kitendea kazi; kinyume chake lazima kusaidia watu katika kulinda wale wanaotetea haki za kibinadamu na kuwakumbuka wafiadini wake, kati yao mwanamke kiongozi kama Sr.Dorothy Stang.

Na hatimaye: Wakati wa kipindi hiki cha kufanyia kazi Instrumentum Laboris, sauti ya Amazonia imesikika katika mwanga wa imani. Imetafuta kujibu kilio cha watu na katika eneo la amazonia kwa ajili ya ekolojia fungamani na kwa ajili ya michakato mipya ya safari, kwa ajili ya kukuza uwezo wa kinabii katika Ukanda wa Amazonia. Sauti hizi za Amazonia zinaomba Sinodi ya maaskofu kutoa jibu moja katika hali tofauti na kutafuta njia mpya ambayo inaweza kufikia kairós kwa ajili ya Kanisa na kwa ajili ya dunia.

17 June 2019, 12:13