Baraza la makardinali, washauri wa Baba Mtakatifu Francisko Baraza la makardinali, washauri wa Baba Mtakatifu Francisko  

Mkutano wa Baraza la Makardinali washauri wa Papa,8-10 Aprili 2019

Tangu tarehe 8 hadi 10 Aprili 2019 unafanyika Mkutano wa Baraza la washauri wa Papa kwa lengo la kuendeleza shughuli ya mabadiliko ya Katiba ya kitume na mambo mengine yanayohusu Kanisa la Ulimwengu.

Kuanzia tarehe 8 hadi 10 mjini Vatican unafanyika mkutano wa Baraza la Makardinali washauri wa Baba Mtakatifu Francisko akiwepo hata yeye, pia ni Mkutano wa 29 wa Baraza hilo. Mkutano wao wa mwisho ulikuwa umefanyika kuanzia tarehe 18-20 Februari na mbapo walikuwa wameendelea kufanya kazi kuhusiana na Katiba mpya ya Kitume na ikiwa inaongozwa na kauli mbiu ya muda: Praedicate evangelium. Hati hiyo itatolewa tafakari katika mabaraza ya Maaskofu kitaifa na Sinodi ya Makanisa ya Mashariki, Mabaraza ya Kipapa, Mabaraza ya mashirika Makuu  ya kike na kiume, hata kwa baadhi ya vyuo vikuu vya kipapa.

Wakati wa hitimisho la Mkutano wa 28 wa Baraza hilo, naye msemamaji wa mpito wa vyombo vya habari Vatican akizungumza na waandishi wa habari, Dk. Alessandro Gisotti alikuwa amesisitiza kwamba, hati hiyo labda inaweza kutangazwa rasmi mwaka kesho. Hata hivyo alibainisha kuwa hati hiyo inahitaji kufanyiwa marekebisho na kutazamwa na wanasheria ambao watahamasishwa na Baba Mtakatifu kama ishara ya upamoja.

Mapambano dhidi ya manyanyaso

Kiini cha Baraza la mwisho pia kiligusia juu ya mkutano kuhusu ulinzi wa Watoto ambao ulikuwa ufanyike siku chache kabla ya mkutano huo kuanza, yaani Mkutano ulioanza tarehe 21-24 Februari 2019. Kadhalika walikuwa wamegusia hata juu ya kujiudhuru kwa Askofu mstaafu wa Washington Theodore McCarrick. Makardinali washauri walijiwekwa ahadi ya kuwa jitihada za Kanisa katika kupambana dhidi ya kila aina ya manyanyaso ndani na nje ya Kanisa.

Lengo  na muundo wa Baraza la Makardinali washauri wa Baba Mtakatifu

Baba Mtakatifu Francisko alianzisha chombo hiki cha Makardinali washauri  kunako tarehe 28 Septemba 2013, akiwa na lengo la kutaka kuwa na washauri kwenye ngazi ya utawala wa Kanisa la ulimwengu na zoezi la kujifunza mpango mpya wa Katiba ya Kitume ya Roma. Mkutano wa kwanza ulifanyika tarehe 3 Oktoba 2013. Na kwa sasa Baraza hili linajumuisha Makardinali sita: Mratibu ni Kardinali  Óscar Andrés Rodríguez Maradiaga, Askofu Mkuu wa  Tegucigalpa, Kardinali  Giuseppe Bertello, mwenyekiti wa Serikali ya mji wa Roma, Kardinali  Oswald Gracias, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Bombay, Kardinali, Reinhard Marx, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Monaco na Frisinga, Kardinali Sean Patrick O'Malley, Askofu Mkuu wa  Boston, Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican. Aidha katika Baraza hili wapo hata Askofu  Marcello Semeraro wa Jimbo Katoliki  Albano, katibu wa Baraza na  Askofu  Marco Mellino, msaidizi Katibu aliyeongezeka.

09 April 2019, 09:18