Hotuba ya Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican katika Mkutano wa kimataifa tarehe 28 Februari 2019 chuo kikuu cha kipapa cha Gregoriana Hotuba ya Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican katika Mkutano wa kimataifa tarehe 28 Februari 2019 chuo kikuu cha kipapa cha Gregoriana 

Kard.Parolin:Makubaliano ya China na michakato kwa nchi za Afrika

Katibu wa Vatican Kardinali Parolin ameudhuria mkutano wa Kimataifa kuhusu makubaliano ya Vatican na Serikali katika karne ya XIX –XXI. Mifano ya kuendeleza katika imani na uhuru wa dini.Nje ya kikao hicho amezungumza kuhusu mchakato wa makubaliano ya China juu ya maaskofu na harakati za makubaliano na baadhi ya nchi za Afrika

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kardinali Piero Parolin Katibu wa Vatican akizungumza na Vatican News kuhisiana na  mchakato wa Jumhuri ya watu wa China baada ya makubaliano ya muda uliotiwa saini tarehe 22 Septemba mwaka jana huko Beijing anathibitisha kwamba mchakato huo ulichukua muda mrefu na ambao hatimaye walifikia hatua hiyo ya kutangazwa kwa maaskofu wa China na ambao unapaswa kuanza kwa dhati na ambao ni matarajio ya kutoa matunda kwa ajili wema wa Kanisa na nchi kwa ujumla. Amesema hayo nje ya Mkutano  wa Kimataifa uliokuwa unaongozwa na  mada ya  makubaliano ya Vatican na Serikali katika karne ya XIX –XXI. Mifano ya kuendeleza katika imani na uhuru wa dini. Ni mkutano uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Kipapa Gregoriana, Roma na  ambao unafungwa tarehe 1 Machi 2019.

Sehemu  ambazo hazitambulikana pamoja

Kardinali Parolin akifafanua zaidi juu ya suala hili anasisitiza kuwa makubaliano ya muda ni kesi ambayo bado haijakamilika kati ya sehemu zote mbili kwa maana bado hakuna utambulisho rasimi sehemu mbili lakini, ni makubaliano ya muda. Hata hivyo amekumbusha kuwa lengo la makubaliano haya kwa upande wa Kanisa katoliki ni kutaka kutimiza utume wake, hasa wa kuomba uhuru wa dini kwa waamini wa iman tofauti na kuwezesha Kanisa kupanua huduma zake kwa  kutoa mchango wa dhati wa maendeleo ya kitasaufi na zana katika nchi na ili  kukuza amani kama inavyoonesha kwatika hati ya mtaguso wa II wa Vatican Gaudium et spes.

Makubaliano na nchi ambazo wakatoliki ni wachache

Vile vile Kardinali Parolin amekumbusha hata  makubaliano ya miaka karibuni uliyofanyika katika nchi zenye  wakatoliki ni wachache kuanzia  nchini Tunisia ( 1964), nchi ya Morocco (1983), Israeli (1993) hadi kufikia Mamlaka ya nchi ya Palestina mwaka (2015), na kwa maana hiyo ameonesha ni kwa jinsi gani, nyakati zilizopita, Vatican ilitafuta kwa njia zozote  kuwa na mapatano na nchi ambazo siyo wakristo. Kwa upande mwingine pia ameelezea juu ya suala la makubaliano na chi za Mashariki ambazo hazina haja ya kuwa na makubaliano hayo lakini wakatoliki wamekuwa wakitafuta kuhakikisha uhuru wa Kanisa dhidi ya vishawishi vya Serikali kutaka kuingilia mipango yake ya ndani na katika uteuzi wa maaskofu.

Hakuna makubaliano katika nchi za Kingereza

Suala jingine lilikuwa lile la mahusiano ya Vatican na nchi ambazo hazina makubalino au mapatano kama ilivyo kwa nchi nyingi zenye utamaduni wa kiorthodox, lakini zaidi nchi za Kingereza kama vile Uingereza na Marekani au zenye utamaduni wa kingereza kwa ajili ya matatizo ya asili ya utamaduni. Katika suala hilo nyeti , makubaliano yapo ya kijujuu kati ya sehemu mbili. kwa kutoa mfano Kardinali Parolin ametoa mfano wa nchi ya Vietnam, kwa maana leo hii makubaliano kwa ajili ya kutangaza maaskofu ni kwa njia ya kutamka bila maandishi maalum. Hiyo ni kutokana na kwamba kuna nchi nyingi ambapo Kanisa haigii katika makubaliano yoyote na linaishi na kutenda kazi yake na nchi serikali hizo anabainisha Kardinali Parolin. Japokuwa anasema ni chombo singi na umuhimu wake katika  kuhakikisha misingi yake  ya kuleta uhuru wa Kanisa ndani ya mzunguko wake kwa ujumla.

Uhuru wa dini ni haki msingi wa binadamu

Leo hii uhuru wa dini na ambao ni haki msingi wa binadamu na jumuiya ni muhimu  kwa ajili ya kanuni katika mantiki ya pamoja ya kushirikiana kati ya Kanisa na Serikali, ili kuweza kuzuia migogoro. Hata hivyo hadi sasa, imejionesha wazi umuhimu wake na haki hiyo anathibtisha itaendelea kuonekanewshwa.Kwa maana hiyo Vatican inatendeleza jitihada za kuweka makubaliano katu ya nchi nyingine ambazo zilikuwa bado. Hata hivyo Kardinali Parolin ameweza kufafanua juu ya mchakato mingine inayoendelea kwa mfano anathibitisha kuwa kwa miaka ya mwisho wameweza kufanya kazi pamoja na chi za Afrika na ambazo kwa hakika zenyewe zimeonesha upendeleo huo na kuwaepo  uwezekano wa kuanza mchakato na ambao unakaribia kuisha kama ilivyo hata mchakato mzima wa kazi kubwa ya nchi ya China.

01 March 2019, 16:26