Vatican News
Balozi wa Armenia Bwana Garen Nazarian amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican tarehe 9 Machi 2019 Balozi wa Armenia Bwana Garen Nazarian amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican tarehe 9 Machi 2019  (Vatican Media)

Balozi wa Armenia awasilisha hati za utambulisho mjini Vatican

Balozi Garen Nazarian alianza shughuli za kidiplomasia mwaka 1991 na tangu wakati huo ameshika nyadhifa mbali mbali katika Wizara ya Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kama mkuu wa Ofisi tangu mwaka 1991 hadi mwaka 1996. Kati ya mwaka 1996 hadi mwaka 2002 aliteuliwa kuwa Balozi wa Armenia kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko mjini Geneva.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi, tarehe 9 Machi 2019 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bwana Garen Nazarian, Balozi mpya wa Armenia mjini Vatican ambaye alizaliwa kunako mwaka 1966, huko Armenia. Ameoa na ana watoto wawili. Historia yake inaoesha kwamba, kunako mwaka 1990 alihitimu masomo yake Chuo Kikuu cha Yerevan na kujipatia na kujipatia shahada ya uzamili katika masomo ya mashariki. Baada ya kujiendeleza zaidi katika masuala ya siasa kimataifa kwenye Taasisi ya Diplomasia mjini Moscow, mwaka 1994 aakajipatia diploma.

Balozi Garen Nazarian alianza shughuli za kidiplomasia nchini mwake kunako mwaka 1991 na tangu wakati huo ameshika nyadhifa mbali mbali katika Wizara ya Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kama mkuu wa Ofisi tangu mwaka 1991 hadi mwaka 1996. Kati ya mwaka 1996 hadi mwaka 2002 aliteuliwa kuwa Balozi wa Armenia kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko mjini Geneva. Kati ya mwaka 2001-2005 akateuliwa kuwa ni mjumbe wa Kikosi kazi kati ya Serikali ya Marekani na Armenia. Kati ya Mwaka 2005-2009 akateuliwa kuwa Balozi wa Armenia nchini Iran na kati ya mwaka 2009-2014 akateuliwa kuwa Balozi wa Armenia kwenye Umoja wa Mataifa. Kati ya mwaka 2014-2018 alikuwa ni Naibu Waziri wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa. Tarehe 9 Machi 2019 akawasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko!

Balozi Armenia
09 March 2019, 15:00