Askofu mkuu Piergiorgio Bertoldi ameteuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Msumbiji. Askofu mkuu Piergiorgio Bertoldi ameteuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Msumbiji. 

Askofu Mkuu Bertoldi ateuliwa kuwa Balozi nchini Msumbiji

Askofu mkuu Bertoldi alizaliwa huko Varese, Jimbo kuu la Milano, tarehe 26 Julai 1963. Akapewa Daraja Takatifu la Upadre tarehe 11 Juni 1988. Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 24 Aprili 2015 akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Burkina Faso na Niger na kuwekwa wakfu tarehe 2 Juni 2015 na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Piergiorgio Bertoldi, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Msumbiji. Kabla ya uteuzi huu, Piergiorgio Bertoldi alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Burkina Faso na Niger. Askofu mkuu Bertoldi alizaliwa huko Varese, Jimbo kuu la Milano, hapo tarehe 26 Julai 1963. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikuhani, akapewa Daraja Takatifu la Upadre tarehe 11 Juni 1988.

Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 24 Aprili 2015 akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Burkina Faso na Niger na kuwekwa wakfu tarehe 2 Juni 2015 na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican. Historia ya maisha yake inaonesha kwamba, baada ya Daraja Takatifu ya Upadre, alijiendeleza na hatimaye akapata Shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa. Tarehe Mosi, Julai 1995 akaanza utume wa kidiplomasia na amewahi kutekeleza dhamana hii kwa mara ya kwanza kwenye Ubalozi wa Vatican nchini Uganda, Jamhuri ya Congo, Colombia, Yugoslavia ya zamani, Romania, Iran na Brazil. Tarehe 19 Machi 2019 akateuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Msumbiji!

20 March 2019, 17:22