Vatican News
Iwapo atujishughulishi na utunzaji wa mazingira leo hii, sayari hii itakuwaje baada yetu sisi kwa ajili ya kizazi kijacho? Iwapo atujishughulishi na utunzaji wa mazingira leo hii, sayari hii itakuwaje baada yetu sisi kwa ajili ya kizazi kijacho? 

Askf.Mkuu Auza:Mtazamo wa Papa na Umoja wa mataifa kuhusu mazingira endelevu

Tarehe 27 Machi 2018 Askofu Mkuu Bernardito Auza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani ametoa tafakari yake kuhusu mtazamo wa Papa na Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira,katika kitivo cha Cassamarca kwa ajili ya wahamiaji na utandawazi,Chuo Kikuu Fordham

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Askofu Mkuu Bernardito Auza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani kwa kuongozwa na mada ya Papa Francisko na Umoja wa Maifa kuhusu Mazingira ametoa tafakari kwa kipindi hiki tarehe 27 Machi 2019. Tafakari hiyo ameifanya katika Kitivo cha Cassamarca kwa ajili ya wahamiaji katika Chuo Kikuu cha Fordham Jijini New York, ambapo amenza kwa kuwasalimia, mapadre, Profesa Schwalbenberg na wajumbe wote wa Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Fordham, Dk. Fakharzadeh pamoja na  wajumbe wote wa chama cha Kipapa cha Centesimus Annus na washiriki wote.  Ameonesha kwanza furaha yake ya  kurudi katika somo kwa mara ya nne tena , katika kiti cha Mwenyekiti wa Chama cha Cassamarca cha  Uhamiaji na Utandawazi kwenye Chuo Kikuu cha Fordham.

Aidha anasema kwamba katika hotuba yake ya  mwezi Februari 2017, alizungumzia juu Vatican  na mapambano dhidi ya biashara ya binadamu. Na mwezi Machi 2018, alishirikisha mawazo yake juu ya vyombo vya kijamii Katoliki hasa wakati huu wa migogoro ya kimataifa.  Mwezi Septema 2018 katika somo lake aligusia juu ya Baba Mtakatifu Francisko kuhusu mtazamo wa usalama wa vyakula na wito wake wa kutafuta njia mpya. Kwa maana hiyo mwaka huu 2019 ,tafakari yake ni kujikita juu ya  mtazamo wa Baba Mtakatifu Francisko na Umoja wa mataifa kuhusu mazingira. Hata hivyo amependa kushukuru Mpango wa Chuo Kikuu cha Fordham katika Uchumi na Maendeleo ya kisiasa Kimataifa, chini ya usimamizi  wa Profesa Henry Schwalbenberg, pia  anamependa kushukuru kwa uwepo na ushirikiano wa Chama cha Kipapa cha Centesimus Annus. Mada hii msingi mbele yetu leo ni kubwa sana anasema na nyaraka nyingi na vyanzo ambavyo vimeweza kutolewa. Lakini mazingira kwa sasa ni moja ya suala pana  kwa pande zote mbili, Kanisa na dunia , kwa dhati ni moja ya mambo msingi ambayo Vatican imejaribu kuzingatia kwa kiasi kikubwa. Na kwa maana hiyo katika tafakari hiyo anapendelea kujikita katika mawazo ya Baba Mtakatifu, pia ya Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira.

Wakati Baba Mtakatifu alipozungumza katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kunako Septemba 2015, katika mada msingi aliyojikita nayo ilikuwa ni utunzaji wa nyumba yetu na ndugu kaka na dada wanaoishi katika nyumba hii lakini wamebaguliwa, ushirikiano kati ya hatua hizo mbili. Kuharibu mazingira, alisema,  ni kuharibu wanadamu na ambapo inaonekana wazi katika maneo fulani ambayo yantumiwa na kuharibika mazingira yake na wakati huo huo watu wake wanaache pembezoni mwa jamnnii suala ambalo aliita au anaendelea kubainisha ni kujenga utamaduni wa kibaguzi. Kwa kukabiliana na hali hii, alisema kuwa haitoshi, makubalino bali kinachotakiwa ni hatua madhubuti za sera za kisiasa ambazo kwa dhati zinakabiliana na hatua hiyo kwa haraka dhidi ya majanga ya kijamii, uchumi na ubaguzi. Katika Wosia wa Laudato Si unatupatia neno ekolojia fungamani,  kanuni kuu ambayo Baba Mtakatifu Francisko anatumia mara kwa mwara na ambayo ni  njia yake ya kuonesha  wasiwasi mkuu kuhusu mazingira. Mtazamo kuhusu ekolojia fungani inaanza kwa jinsi gani Baba Mtakatifu anatazama dunia. Anatazama dunia kwamba, siyo kitu cha kinachohusu wasi kuwa na wasi wasi  au uziri wa kutumia, badala yake anatazama dunia kama nyumba ya kawaida ya kuishi kila mmoja. Na nyumba mara moja inaashiria jambo la familia ambamo sisi sote tunapaswa kuishi na kujenga kwa namna flani. (LS 13, 60, 61).

Akizungumza kuhusu hali ya hewa, anasema kuna, makubaliano ya kisayansi yaliyo imara kuhusu ongezeko la joto katika  mfumo wa hali ya hewa unaleta wasi wasi mkubwa hasa kuonesha kupanda kwa kasi kwa kiwango cha bahari,  ongezeko la matukio ya tabianchi(LS 23). Aidha kuhusu mkutano wa Paris, Baba Mtakatifu anazungumzoa juu ya  maji  (LS 28), kuhusu magonjwa yanayohusiana na maji na shida mbalimbali (LS 28-29), kuhusu kupoteza kwa viumbe hai, misitu na miamba na wakati huo hata kupote jwa   ya mimea (anuai) na wanyama (LS 32-42). Miongoni mwa sababu, anazingatia zaidi juu ya gesi chafu ambazo hutoka katika shughuli za binadamu na matumizi makubwa ya mafuta machafu ya viwanda. Kwa maana hiyo anasisitiza kuwa hizi ni moja ya changamoto kuu zinazokabili mwanadamu siku zetu (LS 25) na kwamba, “kuna haja ya haraka ya kuendeleza sera ili katika miaka michache ijayo, utoaji wa hewa chafu na gesi zenye sumu nyingi ziweza kupunguzwa kwa kasi”(LS 26).

Aidha Askofu Mkuu Auza anasema kwamba, Baba Mtakatifu katika hotuba yake katika Umoja wa Mataifa anakubaliana na data za kisayansi na kwa maana hiyo hakuna haja ya kufafanua hili. Kuhusiana na hali yake ya kisayansi Papa Francisko anasema kwamba mtazamo wa watu kujihusisha na teknolojia ni mzizi wa mgogoro wa mazingira, kwa sababu unajiweka ndani ya moyo wa shughuli za binadamu na hatari (LS 101). Aidha anaongeza kusema, pamoja na kwamba Teknolojia imeleta mambo  mengi na nzuri, bila ya kuunganishwa na maadili sahihi, mambo kama nishati ya nyuklia, teknolojia ya habari, ujuzi wa vinasaba vyetu,  lakini zaidi imeweza kutumika hata kwa madhara yetu (LS 104 ). Uboreshaji wa teknolojia, bila maendeleo ya maadili, inaweza kuishia nje na kuumiza, badala ya kusaidia, sisi au dunia  yetu. Hatimaye, neno la mwisho la hekima kutoka kwa Baba Mtakatifu ni kuhusu “ ni aina gani ya ulimwengu”, Baba Mtakatifu Francisko  anauliza, “ tunataka  tuwachie  kama wale waliokuja kabla yetu  kwa watoto ambao sasa wanakua? Swali hili, anasema, sio tu kuhusiana na mazingira yaliyotengwa; suala hili haliwezi kutozingatiwa usahisi wake.

Tunapojiuliza ni aina gani ya ulimwengu tunao taka kuuacha nyuma, tunafikiri katika nafasi ya kwanza, mwelekeo wake mkuu, maana yake na maadili yake. “Iwapo hatutapambana na masuala haya ya kina”, anaongeza kusisitiza, “naamini kuwa ekolojia haitaleta matokeo muhimu na yenye maana. Lakini ikiwa masuala haya yanashughulikiwa kwa ujasiri, tunataongozwa na kujiulizwa maswali mengine ya wazi”. “Ni  kusudi lipi  la maisha yetu duniani? Kwa nini tuko hapa? Lengo la kazi yetu na jitihada zetu ni nini? Je! Dunia inatupatia kitu gani “(LS 160). Baada ya kujiuliza maswali hayo, Baba Mtakatifu  Francisko anathibitisha, “ hakuna muda mrefu zaidi kusema kwamba tunapaswa kuwa na wasiwasi kwa ajili ya  vizazi vijavyo. Tunahitaji kuona kile kinachotukuza hadhi yetu. Kuacha sayari ambayo inaweza kukarika  kwa vizazi vijavyo, ndiyo wajibu wetu wa kwanza.  Suala hilini moja ya matokeo ambayo yaathiri sana kwa maana linahusina na maana ya mwisho wa maisha yetu duniani.

30 March 2019, 14:34