Vatican News
Kiliturujia kila tarehe 29 Mei ni Kumbukumbu ya Mtakatifu Paulo VI Kiliturujia kila tarehe 29 Mei ni Kumbukumbu ya Mtakatifu Paulo VI 

Kila tarehe 29 Mei Kiliturujia ni kumbukumbu ya Mtakatifu Paulo VI!

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia tamko lililotolewa na Baraza la Kipapa la Ibada na Sakramenti za Kanisa kwamba kumbukumbu ya Mtakatifu Paulo VI itakuwa inaadhimishwa kila tarehe 29 Mei katika kutoa umuhimu wa ulimwengu mzima wa mifano ya utakatifu wa watu wa Mungu

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Kwa kuzingatia utakatifu wa maisha ya Baba Mtakatifu, ushuhuda wake katika matendo na maneno, kwa kuzingatia huduma yake katika uchungaji wa kitume kwa ajili ya Kanisa duniani kote, pia  Baba Mtakatifu Francisko kwa kusilikiza maoni na matashi ya Watu wa Mungu, ameridhia kwamba maadhimisho ya Mtakatifu Paulo VI yaandikwe katika Kalenda Kuu ya Kirumi na kufanyika kumbukumbu ya kawaida ya kiliturujia kila tarehe 29 Mei.

Liturujia ya kumbukumbu ya Mtakatifu Paulo VI

Ndiyo maandishi yaliyomo katika Hati kutoka kwa Baraza la Kipapa la Ibada na Sakramenti za Kanisa iliyotolewa tarehe 6 Februari lakini ikionesha kuandikwa tarehe 25 Januari 2019 sambamba na Sikukuu ya Mtakatifu Paulo mtume wa watu. Katika Hati hiyo imeandikwa kuw: Kumbukumbu hii inapaswa iwekwe katika Kalenda na Vitabu vya kiliturujia kwa ajili ya maadhimisho ya Misa na masifu. Maandishi ya kiliturujia lazima yaandaliwe na kuambatanisha na hati hiyo, ambayo inatakiwa itafsiriwe na kuidhinishwa mara baada ya kupitishwa kwa waraka na kutangazwa na Mabaraza ya Maaskofu. Hati hiyo inaonesha maisha, kazi na huduma ya Mtakatifu Papa Paulo VI.

Tarehe 29 Mei siku ya kupewa daraja Takatifu la upadre

Naye Kardinali Robert Sarah Rais wa Baraza la Kipapa la Ibada na Sakramenti za Kanisa amethibitisha kuwa tarehe hiyo imechaguliwa kwa sababu tarehe 29 Mei 1920  ndipo alipopewa daraja la takatifu la upadre, kwa maana siku ya kuzaliwa kwake mbinguni inaangukia tarehe 6 Agosti, sambamba na sikukuu ya kung’ara kwa Bwana. Aidha anasema iwapo mtakatifu ni yule ambaye anatumia muda wake kutoa matunda ya neema ya kazi na kujifananisha maisha yake na maisha ya Kristo, Papa Paulo VI aliweza kufanya hivyo kwa kujibu wito katika utakatifu kama mbatizwa, padre, askofu na Papa na sasa anatafakari Mungu uso kwa uso. Yeye daima alikuwa akisisitiza kuwa, ni katika kutafuta upendo wa Mungu ambao unafanyika kwa njia ya sala, kitubio na kujisadaka, vinaweza kuhakikishia  mafanikio ya kweli ya maisha ya kikristo na kitume na kijikita katika matendo ya dhati kwa kuwa mstari wa mbele wa kumtangaza Bwana katika utakatifu. (Hotuba yake katika sikukuu yake yatehe 21 Juni 1976 (Mk. 1, 15) na (Mt.5, 48).

Paulo VI:kuwa na Kanisa Mama la upendo

Kardinali Saraha akiendelea na ufafanuzi wa maisha yake anasema, Mtakatifu Paulo VI akiwa padre kunako mwaka 1931 na alipokuwa amekwisha anza kutoa huduma yake Vatican na baada ya kukataa sheria maalum ya kuongeza ambayo ilikuwa ni tofauti na maisha yake ya kikristo kama mtindo wa maisha ya kawaida, alisema kwamba, anataka kukuza kwa namna ya pekee ule upendo ambao ni muhimu na maisha ya tasaufi ya maisha katoliki. Katika maandishi yake anasema: nitakuwa na Kanisa Mama la Upendo, na katika liturujia zake ndiyo ilikuwa kanuni ya tasaufi ya dini. Kwa kutafakari kutoka fumbo la ekaristi alikuwa akichota ulazima wa kujitoa maisha yake kila sehemu, kwa kuonesha kama misa ya maisha yake, umoja na daima wa bure. (maandishi yake wakati wa mafungo katika Monasteri ya Montecassino).

Vitabu vya kiliturujia

Kwa kuunganisha na hati hiyo, aidha Kardinali Sarah amebainisha kwamba wametoa maandiko ya kuongeza katika vitabu vya kiliturujia (kalenda,Misale ya Waamini,Liturujia ya Masifu na Ufiadini). Maombi ya pamoja yanatoa sauti ya kile ambacho Mungu amemtendea mtumishi wake mwaminifu na kwa maana sala inasema:Ulimkabidhi Kanisa lako Mtakatifu Paulo VI kulingoza, Mtume jasiri wa Injili ya Mwanao na kwa kuangazwa na mafundisho yake tunaweza kushirikiana na naye ili kueneza duniani ustaarabu wa upendo. Hii ni moja ya ufupisho msingi wa tabia ya utume wa Papa huyo na mafundisho yake katika Kanisa ambalo ni la Bwana (Ecclesiam Suam), linalojikita kutangaza Injili kama alivyokuwa akikumbusha katika Evangelii nuntiand, hati ambayo inatoa mwaliko wa kushuhudia kuwa Mungu ni Upendo anasisitiza Kardinali Sarah.

Katika Masomo ya Kitabu cha masifu,kuna haya mahubiri yake ya mwisho wakati wa Mtaguso 

Katika masomo yaliyopo kwenye Kitabu cha masifu, kuna masomo ya kibiblia kwa ajili ya Misa, yaliyochaguliwa kwa ajili ya mapapa na masomo ya masifu ambayo baadhi kuna hatua za mahubiri ya mwisho wa Mtaguso wa pili, tarehe 7 Desemba 1965, kwa ufupisho katika mada:ili kujua Mungu lazima kumjua mtu. Mtakatifu Paulo VI aliishi kabla na baada ya kuwa papa kwa kutazama kila wakati Kristo na ambapo alikuwa akihisi ulazima wa kila mtu kumtangaza. Alikuwa amemwonesha katika barua yake ya kwanza ya Kichungaji akiwa Askofu Mkuu wa Milano, iliyokuwa na kielelezo cha Mtakatifu Ambrosi kunako mwaka 1955: Omnia nobis est Christus: Kristo ni wa lazima. Kristo anatosha. Kristo ni yote kwa ajili yetu. Katika mzizi wa mahubiri yake alionesha mapema shauku ya kuonesha kwa mapadre na walei ule upendo hai kwa Kristo, wa kutamtambua na ulio huru.

Upendo kwa ajili ya Kristo ni upendo kwa ajili ya Kanisa lake

Katika tafakari la tarehe 5 Agosti 1963 mwezi mmoja baada ya kuchaguliwa kwake katika Kiti cha Mtakatifu Petro aliandika: Ninapaswa kurudi katika msingi: mahusiano na Kristo ambayo yanapaswa yawe kisima cha unyenyekevu wa kweli: “nenda mbali nami kwa sababu mimi mdhambi…” niwe na uwezekano: "nitawafanya wavuvi wa watu…” kuishi kwangu ni Kristo…”. Upendo kwa ajili ya Kristo ni upendo wa Kanisa lake. Hata katika wazo la kifo aliweza kuandika:“ninaomba kwa Bwana ambaye ananipatia neema ya zawadi ya kifo changu cha upendo kwa ajili ya Kanisa. Ninaweza kuthibitisha kwamba daima nimekuwa ninalipenda na kwa ajili yake hakuna kingine chochote nimeweza kuishi”.

Mtetezi wa maisha ya binadamu, wa amani na maendeleo ya binadamu

Kwa kuongozwa na kupenda sura na shughuli ya kitume ya Mtakatifu Paulo, na wakati Roho Mtakatifu aliongoza ni nani awe kwenye kiti cha Petro, Kardinali Sarah anasisitiza kuwa, hakujibakiza nguvu zake katika huduma ya Injili ya Kristo, ya Kanisa na binadamu, kwa mtazamo wa mwanga hawali ya yote wa wokovu wa Mungu. Mtetezi wa maisha ya binadamu, wa amani na maendeleo ya kweli ya kibindamu, kama alivyokuwa akionesha katika mafundisho yake, anataka Kanisa kwa kuongozwa na Mtaguso,lijikite katika matendo ya dhati misingi na kawaida,l igundue daima utambulisho wake, kwa kushinda migawanyiko ya wakati uliopita na kuwa makini kwa nyakati mpya. Kanisa la Kristo linaliweka Mungu akiwa nafasi ya kwanza ili kutangaza Injili na hata kutoa msaada wa ndugu, kujenga ustaarabu wa upendo uliooneshwa kwa njia ya Roho ya Pentekoste.

Kumbusho la kweli ni  Paulo VI aliyelijenga kwa njia ya ushuhuda wa kitume

Katika maandishi yake binafsi Mtakatifu Paulo VI alikuwa ameandika; hakuna kutengeneza kumbusho kwa ajili yangu. Hata kama mwezi Oktoba 1989 waliweza kutengeneza kumbusho katika Kanisa Kuu la Milano, lakini kumbusho ya kweli, Kardinali Sarah anahitimisha akisema, Mtakatifu Paulo VI alilitengeneza kwa njia ya ushuhuda wake, katika matendo yake, kwa ziara zake za kitume,kwa njia ya uekumene, kwa njia ya kazi ya Nova Vulgata  ni toleo la Biblia ya kilatino kwa matumizi rahisi) kwa njia yaupyaisho wa kiliturujia; kwa njia mafundisho mengi na mifano, huku akionesha uso wa Kristo,utume wa Kanisa, wito wa binadamu wa sasa na kwa kupatanisha wazo kikristo na dharura za wakati ule mgumu ambapo aliweza kuongoza kwa kujitoa kabiasa, kuteseka sana na Kanisa.

/content/dam/vaticannews/pam/audio/agenzie/netia/2019/02/07/13/mtakatifu-paulo-vi-134860959.mp3
07 February 2019, 11:52