Vatican News
Padre Pier Luigi Nava ateuliwa kuwa Katibu mkuu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume Padre Pier Luigi Nava ateuliwa kuwa Katibu mkuu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume  (AFP or licensors)

Padre Pier Luigi Nava ateuliwa kuwa katibu mkuu Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume

Padre Nava alizaliwa tarehe 7 Julai 1953 huko Leffe, Ubelgiji. Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa, kunako tarehe 28 Aprili 1978 akaweka nadhiri zake za daima na hatimaye, kupewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 17 Machi 1979. Akaendelezwa kimasomo na Shirika na hatimaye akajipatia shahada ya kwanza katika taalimungu toka katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Anselmi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Pier Luigi Nava kutoka Shirika la Montfortaine kuwa Katibu mkuu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume. Padre Nava alizaliwa tarehe 7 Julai 1953 huko Leffe, Ubelgiji. Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa, kunako tarehe 28 Aprili 1978 akaweka nadhiri zake za daima na hatimaye, kupewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 17 Machi 1979. Akaendelezwa kimasomo na Shirika na hatimaye akajipatia shahada ya kwanza katika taalimungu toka katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Anselmi kilichoko mjini Roma.

Padre Pier Luigi Nava katika maisha na utume wake kama Padre mtawa, amebahatika kupewa dhamana na majukumu mbali mbali kama vile: Mkuu wa jumuiya. Mshauri na Katibu mkuu wa Kanda pamoja na kuendelea kusaidia katika shughuli za kichungaji zinazoendeshwa na Shirika katika Parokia za Jimbo kuu la Roma. Kuanzia mwaka 1996 akateuliwa kuwa mjumbe wa Kamati mchanganyiko kati ya Maaskofu Katoliki Italia na Watawa.

Kunako mwaka 2000 akajiendeleza zaidi katika masomo ya maisha ya kitawa kutoka katika Kitivo cha Sayansi ya Elimu, kwenye Taasisi ya “Auxilium” iliyoko mjini Roma. Mwaka 2014 akateuliwa kuwa ni mshauri katika Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume! Ni mtaalam aliyebobea katika maisha ya kitawa hususan malezi na masuala ya Sheria na Kanuni za Kanisa!

Padre Nava
27 November 2018, 14:49