Vatican News
Bado  watu wengi wa asilia wanabaki kuwa nyuma na chini ya vitisho  Bado watu wengi wa asilia wanabaki kuwa nyuma na chini ya vitisho   (AFP or licensors)

Vatican katika juhudi za haki ya watu wa asili ili wajitegemee!

Pamoja na maendeleo yaliyo timizwa, urithi wa mazingira, utamaduni, tasaufi za watu wengi wa asilia wanabakia bado kuwa nyuma na chini ya vitisho. Ameyasema hayo Askofu Mkuu Bernardito Auza, Mwakilishi wa kudumu Vatican, katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini New York, katika Baraza la 73

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

 “Bila kujihusisha katika ardhi yao binafsi, kwa watu wa asili, hasa vijana, ambao daima wanalazimishwa kuhama kwa kufuta mtindo mbadala wa kazi na elimu.  Hiyo ndiyo sababu kubwa ya watu hao kujikuta katika hali mbaya ya umaskini na kuathirika, kwa sababu, wao wanalazimika kukabiliana na hali ya ubaguzi na matatizo makubwa  ya kutafuta ajira katika miji, mahali ambapo imebidi wakimbilie”. Ni maelezo yaliyomo katika hotuba ya Askofu Mkuu Bernardito Auza, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican, katika ofisi za Umoja wa Mataifa, tarehe 12 Oktoba 2018, mjini New York, akihutubia katika Baraza la 73 la Umoja wa Mataifa. Katika hotuba yake, amebainisha kwamba:“Pamoja na maendeleo yaliyotomizwa, urithi wa mazingira, utamaduni,  tasaufi za watu wengi wa asilia wanabakia bado kuwa nyuma na chini ya vitisho”.

Watu wa asila ni waathirika wa ukoloni kiuchumi na kiitikadi: Askofu Mkuu akiendelea na hotuba hiyo amebainisha juu ya uwepo wa ukoloni kiuchumi na kiitikadi uliowekwa chini ya bendera ya kile kinachoitwa, maendeleo, na kuendelea mbele, lakini bila kuhangaikia haki za binadamu hasa watu wa asili au mazingira ambayo wao wanaishi. Akitoa mfano dhahiri amesema: “Hiyo inajionesha wazi katika kitovu ha msitu wa Amazon, mahali ambapo mitindo mipya ya uchimbaji wa madini na kutoa madini msingi na rasilimali nyingi kwa upande wa makampuni makubwa na wadau wengi wa kibiashara ambao wamepelekea uharibifu mkubwa wa mazingira na ukataji hovyo wa misitu, kama ilivyo hata ile ya watu wa asili kuhama katika maeneo yao. Wakati huo huo, sera nyingi za kisiasa, na mashirika mengi ambayo kwa , kijujuu inaonesha kuwa na lengo la  kuhifadhi maeneo na kujidai ni kulinda mazingira ya asili na kuhifadhi anuahi, ambapo wamepelekea mapinduzi makubwa ya uchumi mahalia na maisha ya watu wa asili wanaoishi katika mazingira hayo”

Amazon haiwezi kuwa kisima cha kuchota utajiri ambao kwa urahisi unanyonywa:  “Ni lazima kuvunja huo ulinganisho wa kihistoria, ambao unafikiria msitu wa Amazon  na sehemu nyingine zenye utajiri wa rasilimali katika dunia yetu kama kisima cha utajiri usioisha na ambao kwa kiurahisi uendelezwe kunyonya. Lazima hata kuhakikisha kwamba nguvu za kuhifadhi na kulinda mazingira na  asili vinazingatia haki na kuwa na vyombo muhimu vya kusaidia watu wa asili ambao kwa kanda hizi ndiyo nyumbani kwao. Askofu Mkuu Auza amesisitiza kuwamba, watu wa  asili, lazima wawe mstari wa kwanza katika maamuzi yote yanayotazama moja kwa moja haki kama ile ya kutunnza taasisi yao na kushiriki michakato ya maamuzi ya nchi. Kwa mujibu wa Vatican inathibitisha kuwa, haki kwa watu wa asilin lazima wajitegemee wenyewe katika maeneo yao.

Hatua muhimu za Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuhamasisha na kulinda thamani ya watu wa asili: Hata hivyo akiendela katika hotuba hiyo, Askofu Mkuu Auza ameweza kuwa na utambuzi kwamba, “ katika miaka 20 iliyopita, Umoja wa Mataifa umepiga maendeleo makubwa ya kuhamasisha na kulinda thamani ya utamaduni, urithi na hali za ubinadamu wa watu wa asili, pamoja na kutoa kwao fursa za kuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya utamaduni na kijamii.  Kwa mfano wa ubora huo ni Azimio la pamoja la Dunia, la Haki za Watu wa Asili; kukua kwa jitihada za Mataifa katika hali hiyo; Hata ushiriki hai wa watu wa asilia wakiwa pamoja na mataifa ambao kila mwaka kuna Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa; katika masuala ambayo ni muhimu na mifano ya dhati ya mshimakamano kwa ajili ya jumuiya nzima ya kimataifa”.

Lakini hayo yote hayatoshi: “ watu wa asili wana utamaduni wao wa kuhifadhi na pamoja na mila zao hai, ambazo lazima zihifadhiwe na kulindwa. Kupotea kwa utamaduni wao na mtindo wao wa maisha unaweza kuleta mabaya au hata kupotea kwa anuwahi au kuleta madhar katika nyumba yetu ya pamoja katika kuhifadhi ekolojia. Kuwasaidia kuhifadhi utamaduni wao na mila zao, Akofu Mkuu anasisitiza, ndiyo inabaki kuwa jitihada kubwa ya kufanya kwa wakati wetu.

Papa Francisko, alisema watu wa wasili si watu wachache bali ni watu wa dhati na katika mazungumzo: Hatimaye Askofu Mkuu Auza amekumbuka kile ambacho Papa Francisko alisema tarehe 19 Januari 2018, alipokutana na watu wa asili wa Puerto Madonado nchini Perù: “Utambuzi wa watu wa asili, hauwezi kamwe kufikiriwa ni uchache bali ni udhati wa mazungumzo. Na wao wanatukumbisha kuwa sisi siyo wakuu  wa kazi ya uumbaji. Lazima na kwa dharura ya kuhamasisha, kuthamanisha na kutoa mchango msingi ambao unaweza kuwapeleka katika jamii ya pamoja na siyo kupunguza au kudharau utamaduni wao wa asili  na kuama kuwatazama kama majumba ya makumbusho ya wakati uliopita. Maono yao ya dunia hii na hekima yao, ina mambo mengi ya kutufundisha sisi tusio shiriki utamaduni wao!

ASK.AUZA

 

15 October 2018, 15:26