Vatican imeamua kuendelea katika Maonyesho ya Vitabu Frankfurt
Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Ni mzani chanya katika ishara ya kuendelea kwa Vatican katika Maonesho ya Vitabu mjini Frankfurt unaofunga milango yake tarehe 14 Oktoba 2018. “Uteuzi wa kufanya matukio mawili, amesema Padre Giulio Cesareo, mhariri wa Maktaba ya Uchapishaji wa Vitabu Vatican kwamba, umethibitishwa na ufanisi wa waandishi katoliki kimataifa na sio tu kuhusiana na Magisterium ya Papa Francisko, lakini pia kwa kukusanya mantiki ya hotuba zake katika mfululizo wa uchapishaji wa vitabu vingi Vatican kadhalika kuhusina na kitabu kipya: amesema, Ni kitabu kipya kiitwacho “ Ni mimi , msiogope: Maneno ya Papa Francisko juu ya wakimbizi na wahamiaji,
Nembo mpya
Hata hivyo kutokana na mambo mapya, kwa mara ya kwanza kwa ngazi ya kimataifa, Duka la Vitabu Vatican , limewakilisha nembo mpya. Ni tunda la mageuzi ya vyombo vya habari Vatican na nembo mpya hiyo, ina rangi ya njano ikiwa inafuata falsafa ya nembo ya Vatican News , Vatican Media na Radio Vaticana Italia. Aliyepeleka habari mpya huko Frankfurt ni Kamishna wa Baraza la Mawasiliano, Monsinyo Dario Edoardo Viganò, ambaye alitangaza mipango miwili itakayofanyika mjini Roma mwaka 2019 ambayo inayozungukia juu la Duka la vitabu Vatican .
Mtazamo huu ya uhariri katoliki
Mpango wote huo ameeleza Monsinyo Vigano kuwa, ni lengo la kuunga mkono ulimwengu wa huchapishaji vitabu Katoliki na kuimarisha uwezo wake”. Hata hivyo mikutano hiyo haitakuwa na sifa kama ile ya maonesho ya kimataifa, bali watakuwa na mikutano ya kawaida ambayo itaundwa kwa njia ya kukuza hasa kukabiliana na kushirikiana uzoefu tofauti. Hatua ya kwanza iliyopoendekezwa inaelekezwa kwa sekta ya Italia, itakayo fanyika mwezi Januari 2019. Na ya pili, ambayo ni ya kimataifa, labda katika nusu ya pili ya mwezi Juni 2019. Taratibu hizo tayari zimekwisha kukubaliwa na Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican, Bwana Paulo Ruffini kwa mujibu wa kamishna wa mawasiliano Monsinyo Vigano.