Briefing Sinodi ya Maaskofu mjini Vatican Briefing Sinodi ya Maaskofu mjini Vatican 

Briefing Sinodi:Kanisa liwe mtandao wa kusililiza vijana!

Katika vyombo vya habari mjini Vatican, tarehe 5 Oktoba 2018 ,wametoa Briefing juu ya Sinodi. Kati ya walioshiriki ni Askofu Manuel Ochogavía Barahona, Baba wa Sinodi aliyechaguliwa na Baraza la Maaskofu wa Panama; Askofu Mkuu Anthony Colin Fisher aliyechaguliwa na Baraza la Maaskofu Austalia; msikilizaji kutoka Madagascar Tahiry Malala Rakotoroalahy

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

"Kusikiliza, uelewa na mawe yaliyokataliwa, ndiyo maneno makuu yalitolewa katika mchakato unao endelea wa Baraza la XV la Sinodi ya Maasko juu ya Vijana, imani na mang’amuzi ya miito”. Aliyetoa ufupi huo  kwa waandishi katika vyombo vya habari Vatican juu ya hali halisi inavyoendelea  na Bwana Paolo Ruffini, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican na mwenyekiti wa Tume ya Sinodi kwa ajili ya habari.

Bwana Ruffini akiendelea na ufafanuzi juu ya Sinodi amesema, mchakato wa tatu na wa nne wa Baraza kuu, wamegusia mada kuhusu namna ya kuwa baba na mama wa Kanisa kwa vijana, masuala ya useja, nadhari ya kijinsia , kama pia ilivyo changamoto ya nyakati za digital,hasa hasa kujikita kugusia suala la shauku walizo nazo vijana katika mitandao ya kijamii na njia ukosefu wa kuwa na tamaa ya maisha. Akifafanua  Bwana Paolo Ruffini pia amesema kwamba hata vijana wenyewe, wanahisi waathirika wa jamii inayooneka kuwa na msingi wa uongo na kwa maana hiyo nao, “ wanaomba wasikilizwe na sio kusikia tu, na kama ilivyo umakini  wa kuchukuliwa kwa uzito”.

Aibu ya Kanisa kwa ukiukwaji uliofanywa

Ushuhuda wa kina umetolewa na Askofu Mkuu Anthony Colin Fisher, Baba wa sinodi aliye chaguliwa na Maaskofu wa Australia ambaye ni wa Jimbo Kuu Katoliki la Sydney, na ambaye kwa mara nyingine tena binafsi ameomba msamaha katika suala la manyanyaso. Akizungumza mbele ya waandishi amesema: “Sisi tulipaswa kuhakikisha kwamba Kanisa linakuwa na usalama zaidi kwa watoto ",  kwa maana hiyo anaongeza, “tunaona aibu kwa kile kilichotokea”. "Kuna vijana wengi hata  vijana wa wakati ule wa zamani, waliojeruhiwa, watu ambao imani yao imesalitiwa: "Kanisa lazima lizungumze nao na sio kwao, kama kwamba ni  tukio".

Hata hivyo Kardinali wa Sydney amezungumza pia ukweli mkuu kwa mantiki ambayo inaonekana kwa sasa katika Ukumbi wa Sinodi; ukweli wa hotuba; matokeo na matumaini ambayo yananatarajiwa mbele ya vijana.

 “Kristo ni Mungu aliyejifanya kijana, amesisitiza, Yeye anatupyaisha  na kama anavyopyaisha dunia na vijana, kizazi baada ya kizazi”. Na mwisho Askofu Mkuu Fisher amezungumza juu ya furaha na matunda ya Siku ya Vijana Duniani, iliyofanyika mjini Sidney  kunako 2008, akiwa na matumaini ya kuwa inaweza pia kuwa fursa hata nchini Panama mwaka 2019.

Katika muktadha huo, Askofu Manuel Ochogavía Barahona, Baba wa Sinodi aliyechaguliwa na Baraza la Maaskofu wa Panamna na Askofu wa Jimbo la Colón-Kuna Yala, ameelzea kazi kubwa ambayo Kanisa la Amerika ya Kusini na Visiwa vya Carribbean wako wanafanya kwa sasa, kwa ajili ya mafunzo ya vijana. Akifafanua amesema, “ vijana ni nafasi abayo Mungu anazungumza kwetu, na Kanisa leo hii linaitwa kuwa karibu na vijana kwa huruma  na kujikita katika kusikiliza kila ambacho kinawatukia katika maisha yao”.

Sinodi inayopambwa na  rangi za dunia

Katika mchakato wa Briefing hiyo, amezungumza hata msikilizajia kutoka Kisiwa cha Madagascar, Tahiry Malala Marion Sophie Rakotoroalahy, Mwenyekiti wa Taifa wa Wanafunzi Katoliki. Yeye amebainisha kuwa, Sinodi ni sehemu ya kuanzia na pia ni baraka ya kweli kwa ajili ya vijana ambao wanapaswa kuwa mitume kwa vijana wengine”. Akizungumza kwa namna ua pekee katika hali halisi yao, amebainisha kwa kiasi kikubwa umakini wa liturujia. Kwa upande huo amesema: “Liturujia iko  karibu na vijana na  yenye uwezo wa kuwasaidia kutoa kiu ya matukio ya sasa”.

06 October 2018, 10:42