Vatican News
Askofu Mkuu Edgar Peña Parra akiwa na Papa Francisko Askofu Mkuu Edgar Peña Parra akiwa na Papa Francisko 

Papa amefanya uteuzi mpya wa Askofu Mkuu Edgar Peña Parra

Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, alizaliwa huko Maracaibo nchini Venezuela mnamo tarehe 6 Machi 1960. Akapewa daraja Takatifu la upadre tarehe 23 Agosti 1985 na kupewa jimbo la Maracaibo. Kabla ya kuteuliwa kwake na Papa Francisko kuwa katika Ofisi ya Sekretarieti Kuu ya Mambo ya ndani Vatican, alikuwa Balozi wa Vatican nchini Msumbiji

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko amemteua msaidizi kwa ajili ya Ofisi ya Sekretarieti Kuu ya Mambo ya ndani Vatican, Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, ambaye hadi uteuzi wake alikuwa Balozi wa Vatican nchini Msumbiji. Ataanza utume wake rasmi tarehe 15 Oktoba 2018.

Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, alizaliwa huko Maracaibo nchini Venezuela mnamo tarehe 6 Machi 1960. Akapewa daraja Takatifu la upadre tarehe 23 Agosti 1985  na kupewa jimbo la Maracaibo. Anayo shahada ya sheria na alianza shughuli zake za  kidiplomasia Vatican kunako mwaka 1993. Amewahi kushika nafasi mbalimbali zikiwemo kuwakilisha Shughuli za papa za kitume nchini Kenya na Jugoslavia, Ofisi za ya uwakilishi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva, katika Ubalozi wa Vatican nchini Afrika ya Kusini, Honduras na Mexco.

Aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Telepte mnamo tarehe 8 Januari 2011 na kupewa daraja la uaskofu mnamo  tarehe 5 Februari 2011. Kadhalika amekuwakatika ofisi za ubalozi wa Vatican nchini Pakistan tangu 2001 -20014 na Balozi wa kitume nchini Msumbiji tangu tarehe 21 Februari 2015 hadi kufikia uteuzi wake.

 

 

 

16 August 2018, 15:58