Papa Francisko:Wito wa kuacha vita Palestina,Israel na Ukraine
Na Angella Rwezaula, - Vatican
Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Dominika 22 Oktoba 2023 akiwageukia mahujaji na waamini waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Baba Mtakatifu ametoa wito kwa Nchi ya Israel na Palestina. Ni masikitiko yake kuwa: “ Kwa mara nyingine tena mawazo yangu yanageukia kile kinachotokea Israel na Palestina. Nina wasiwasi, huzuni, ninsali na niko karibu na wale wote wanaoteseka, mateka, majeruhi, waathirika na familia zao. Ninafikiria hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza na inanihuzunisha kwamba hospitali ya kianglikani na parokia ya kiorthodox ya Kigiriki pia zimeathiriwa katika siku za hivi karibuni.” Kwa njia hiyo Papa ameongeza kusema: “Ninarudia wito wangu kwa nafasi kufunguliwa, misaada ya kibinadamu iendelee kuwasili na mateka waachiliwe. Vita, kila vita duniani, pia nikifikiria Ukraine inayoteswa ni kushindwa. Vita daima ni kushindwa, ni uharibifu wa udugu wa kibinadamu. Ndugu, acheni.”
Kuombea Amani Duniani 27 Oktoba
Baba Mtakatifu Francisko amesema: “ Ninawakumbusha kuwa Ijumaa ijayo tarehe 27 Oktoba nimetangaza siku ya kufunga, maombi na toba na kwamba jioni hiyo saa 12.00, katika Kanisa la Mtakatifu Petro tutakuwa na saa moja ya maombi ya kuombea amani duniani.”
Siku ya kimisionari duniani
Baba Mtakatifu Francisko katika muktadha wa Siku, amekumbusha kilele cha Siku ya 97 ya Kimisionari duniani, “ambayo inongozwa na mada yake: “Moyo unaowaka, miguu inayotembea.” Papa amesema kuwa: “ni picha mbili zinazosema yote! Kwa hiyo, amesisitiza kuwa: “Nitatoa rai kwa kila mtu, katika majimbo na parokia, kushiriki kikamilifu siku hii kwa uhai.”
Waperu: Udugu wa Bwana wa miujiza
Kati ya waamini waliokuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ni pamoja na kuwasalimu wote: Warumi na mahujaji, hasa Masista Siervas de los Pobres hijas del sagrado Corazón de Jesús, kutoka Granada; wanachama wa Kituo cha Mfuko wa Elimu cha Roma; Umoja wa (Señor de los Milagros), yaani Bwana Miujiza wa Waperu walioko Roma ambao amewashukuru kwa ushuhuda wao! Na “waelendelee hivyo kwa uchamungu huu mzuri.”
Salamu kwa makundi mengine
Kadhalika Washiriki wa Harakati la wamisionari walei “Walinzi wote wa ubinadamu”, kwaya za aina nyingi, Mtakatifu Antonio Abate” wa Cordenons na vyama vya waamini kutoka Napoli na Casagiove. Pia amewasalimu watoto wa ‘Casa Giardino" wa Casalmaggiore, kikundi cha marafiki vijana wa Jumuiya ya Emmanuel, wakurugenzi na walimu wa “Yohane XXIII” Shule ya Kikatoliki ya Toulon, wanafunzi wa Msalaba Mtakatifu wa Neuilly. Kama kawaida yake amehimitimishwa kwa kuwatakia Dominika Njema wote, lakini tafadhali wasisahau kumuombea.