Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 1 Juni 2023 amekutana na wajumbe wa Baraza la Biashara la Amerika ya Kusini "Consejo Empresarial de America Latina" Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 1 Juni 2023 amekutana na wajumbe wa Baraza la Biashara la Amerika ya Kusini "Consejo Empresarial de America Latina"  (Vatican Media)

Hotuba ya Papa Francisko Kwa Baraza la Biashara la Amerika ya Kusini: Utu wa mtu!

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 1 Juni 2023 amekutana na wajumbe wa Baraza la Biashara la Amerika ya Kusini mjini Vatican. Katika hotuba yake amegusia mada ya kazi, uhamiaji na athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na maendeleo endelevu ya binadamu yanayosimikwa katika utamaduni wa watu kukutana kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Amekazia upyaishaji wa maisha ya kiroho kama ushuhuda wa imani tendaji katika maisha kila siku.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baraza la Biashara la Amerika ya Kusini, “Consejo Empresarial de América Latina; Business Council of Latin America” (CEAL) lilianzishwa rasmi mnamo tarehe 19 Februari 1990, katika Jiji la Mexico, kama mwitikio wa mwelekeo wa sasa wa utandawazi wa uchumi na ukuzaji wa muundo mpya wa kambi za kiuchumi ambazo zimeimarisha ukuaji wa uwazi, masoko ya biashara na mipango ya ushirikiano wa kikanda. CEAL ni Baraza linaloundwa na wajasiriamali binafsi na cha umuhimu zaidi hawa wanatoka Amerika ya Kusini, Puerto Rico, Miami na Iberia. Baraza hili lilianzishwa kwa madhumuni makuu ya kuhimiza ushiriki wa wanachama wake na makampuni binafsi katika ushirikiano na mshikamano wa kibiashara, ili kuimarisha uhusiano wa pamoja na hivyo kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi zao. CEAL inaamini kuwa michakato ya ujumuishaji itafaulu ikiwa itatoa uongozi kama wajasiriamali binafsi. Kwa maana hii, CEAL lina madhumuni ya kuhimiza ushiriki wa sekta binafsi kama wakala wa mabadiliko ya kiuchumi. Baraza linawajumuisha zaidi ya viongozi wa biashara 350, wanahisa na watendaji wa mashirika na vikundi vya biashara. Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 1 Juni 2023 amekutana na wajumbe wa Baraza la Biashara la Amerika ya Kusini mjini Vatican. Katika hotuba yake amegusia mada ya kazi, uhamiaji na athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na maendeleo endelevu ya binadamu yanayosimikwa katika utamaduni wa watu kukutana kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Amewataka kujenga mtandao wa ushirikiano pamoja na umuhimu wa kushuhudia imani yao katika matendo adili na matakatifu.

Baraza la Biashara la Amerika ya Kusini laku7tana na Papa Francisko
Baraza la Biashara la Amerika ya Kusini laku7tana na Papa Francisko

Baba Mtakatifu amewashukuru wajumbe wa Baraza la Biashara la Amerika ya Kusini, kwa kujadili mada ya kazi, uhamiaji na athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na maendeleo endelevu ya binadamu yanayosimikwa katika utamaduni wa watu kukutana kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Hizi ni tema zinazogusa maisha ya watu wengi duniani na hivyo  wanaweza kuunganisha nguvu zao, ili kukabiliana na changamoto, matatizo na fursa mbalimbali zinazoikabili familia ya binadamu katika ujumla wake. Baba Mtakatifu anasema, kazi na ajira zinapaswa kuangaliwa katika muktadha wa watu kukutana, kwa ajili ya kukuza ustawi, maendeleo na mafao ya wengi; mambo yanayohitaji sadaka na majitoleo makubwa, ili kuondokana na uwezekano wa kuwaachisha kazi baadhi ya wafanyakazi. Ikumbukwe kwamba, nyuma ya kila mfanyakazi kuna familia na jamii katika ujumla wake. Kumbe, anawataka wajumbe hawa kujenga mtandao yenye ufanisi na nguvu, kwa kusaidiana ili kuweza kukabiliana na changamoto mamboleo mintarafu kazi na ajira ili hatimaye, kutoa huduma bora zaidi kwa watu wa Mungu, bila mtu awaye yote kuachwa nyuma. Hii ni changamoto pevu. Baba Mtakatifu amewapongeza wajumbe wa Baraza la Biashara la Amerika ya Kusini, kwa kuamua kufanya mkutano wao mjini Roma, mahali ambapo kuna Kaburi la Mtakatifu Petro. Roma ni mahali ambapo kuna wafuasi wengi wa Kristo Yesu wanaojitahidi kutolea ushuhuda wa imani yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake mintarafu mwanga wa Injili. Kumbe, uwepo wao mjini Roma inakuwa ni changamoto ya kupyaisha undani wa maisha na imani yao, tayari kusonga mbele kwa ari na moyo mkuu. Kumbe, mitandao na nguvu ya Kiinjili, iwe ni chachu ya matumaini, huku wakiwa na imani kwamba, Mwenyezi Mungu atawaongoza katika safari yao!  

Baraza Amerika ya Kusini

 

02 June 2023, 16:10