Papa Francisko na Patriaki Tawadros kuadhimisha pamoja miaka 10 ya kukutana kati yao na pia 50 kwa watangulizi wao, Papa pailo VI na Shenouda III mnamo 1973. Papa Francisko na Patriaki Tawadros kuadhimisha pamoja miaka 10 ya kukutana kati yao na pia 50 kwa watangulizi wao, Papa pailo VI na Shenouda III mnamo 1973.  (Vatican Media)

Papa na Patriaki Tawadros:ziara yake itusaidie kukua katika umoja

Papa Francisko na Patriaki wa Kikopti-Kiorthodox wa Alexandria pamoja katika Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa Katekesi ili kuadhimisha miaka 10 baada ya mkutano wa kwanza 2013 na miaka 50 tangu mkutano kati ya Mtakatifu Paulo VI na Patriaki Shenouda III mnamo 1973.“Ziara hii inatuleta karibu na siku ambayo tutakuwa kitu kimoja.”

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Baada ya miaka kumi hasa na miezi kadhaa iliyopita tangu Jorge Mario Bergoglio alipochaguliwa katika kiti cha Mtume Petro, Papa Francisko na Patriaki Tawadros II wanakutana kwa mara nyingine tena. Ni miaka kumi tangu salamu ya kwanza kati ya Askofu wa Roma na patriarki wa Kikoptic-Kiorthodox wa Alexandria, na hamsini tangu kufanyika  mkutano wa kihistoria kati ya watangulizi wao Mtakatifu Paulo VI na Patriaki  Shenouda III mnamo tarehe 10 Mei  1973 ambao ulimalizika kwa kutiwa saini kwa tamko la kawaida la Kikristo la kukumbukwa siku hiyo. Kwa hiyo kumbu kumbu hii inamfanya Patraikia awe katika ziara hiyo hadi Dominika tarehe 14 Mei 2023.

Papa na Tawadros
Papa na Tawadros

Kwa hiyo, Baba Mtakatifu akiwa katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, Jumatano tarehe 10 Mei 2023, amewaelekea waamini na mahujaji wote kwa kwamba anamsalimu Tawadros II, Papa wa Alexandria na Patriaki wa Makao ya Mtakatifu Marko na wajumbe mashuhuri anaoandamana naye. Na kumshukuru kwa kukubali  mwaliko wake wa kufika  Roma kusherehekea pamoja na Papa kumbukumbu ya miaka hamsini ya mkutano wa kihistoria wa Papa Mtakatifu Paulo VI na Papa Shenouda III mnamo mwaka 1973. Ulikuwa ni mkutano wa kwanza kati ya Askofu wa Roma na Patriaki wa Kanisa la Kikopti la Kanisa la Kiorthodox, ambao ulifikia kilele cha kutiwa saini kwa tamko la kawaida la Kikristo la kukumbukwa, hasa mnamo  tarehe 10 Mei 2023.

Miaka 10 tangu kukutana kwa mara ya kwanza Papa na Patriaki Tawadros pia miaka 50 kati ya Paulo VI na Shenida III

Papa Francisko ameongeza kusema kuwa Katika kumbukumbu ya tukio hili, Tawadros alikuja kumuona kwa mara ya kwanza mnamo tarehe 10 Mei miaka kumi iliyopita, miezi michache baada ya kuchaguliwa kwake na kwa Papa Francisko na alipendekeza kusherehekea “Siku ya Urafiki wa Kikoptic kila tarehe 10 Mei na Wakatoliki ambayo inaadhimishwa  kila mwaka tangu wakati huo.  Papa amebainisha jinsi ambavyo wanapigania simun a kutumiana salam una kubaki kuwa ndugu wazuri ambao hawagombani!

Viongozi wakuu wawili wa Kanisa Katoliki na Kikopti huko Misri
Viongozi wakuu wawili wa Kanisa Katoliki na Kikopti huko Misri

Papa amemshukuru kukubali mwaliko wake kwa kuadhimisha matukio hayo mawili na anaomba kwamba “nuru ya Roho Mtakatifu iaangazia ziara yenu Roma, mikutano muhimu mtakayokuwa nayo hapa, na hasa mazungumzo yetu ya kibinafsi”. Ameshukuru kwa dhati kwa kujitolea kwake kwa urafiki unaokua kati ya Kanisa la Kiorthodoksi la Kikoptic na Kanisa Katoliki. Utakatifu wake, wapendwa Maaskofu na marafiki wote, pamoja na wote  ninamwomba Mwenyezi Mungu, kwa maombezi ya Watakatifu na Mashahidi wa Kanisa la Kikoptic, atusaidie kukua katika umoja katika kifungo kimoja na kitakatifu cha imani, matumaini na upendo wa Kikristo.” Kwa kuongeza Papa amesema akizungumzia juu ya “wafiadini wa Kanisa la Kikoptic ambao pia ni wetu, ninataka kuwakumbuka wafia imani kwenye ufukowa Libya, ambao walifanywa wafiadini miaka michache iliyopita. Ninawaomba wote waliohudhuria kusali kwa Mungu abariki ziara ya Papa Tawadros huko Roma na kulinda Kanisa zima la Kiorthodoksi la Kikoptic. Ziara hii na ituletee hatua moja karibu na siku itakayobarikiwa tutakapokuwa wamoja katika Kristo!”

Salamu kutoka kwa Patriaki Tawadros

Kwa upande wake, Patriaki Tawadros akitoa salamu kwa  Papa amependa kuwasilisha pongezi zake kwake, pia kwa niaba ya washiriki wa Sinodi Takatifu na muhimili mzma wa Kanisa la Kiothodoksi la Kikopti  katika maadhimisho ya miaka 10 ya kuchaguliwa kwake kuwa Papa na Askofu wa Roma. Anashukuru yote ambayo wamefanya wakati huu wa huduma kwa ulimwengu wote katika maeneo yote, na anaomba kwamba Kristo akuweke katika afya njema na kukubariki kwa maisha marefu. Na kwa kutazama hapo amependa kurudi  nyuma miaka kumi iliyopita, katika tarehe kama hiyo , na amekumbuka  upendo wake sana katika kumkaribisha pamoja na wajumbe wa Kanisa la Kikoptic wakati wa ziara yake ya kwanza, na jinsi walivyotumia wakati mtakatifu pamoja na yeye na uliojaa upendo wa kidugu ambao uliwajaza.

Maadhimisho ya Siku ya Urafiki wakikatoliki na Wakopti
Maadhimisho ya Siku ya Urafiki wakikatoliki na Wakopti

Mkuu wa Kanisa ka Kikopti amesema mapendo haya yamekuwa kauli mbiu tunayoadhimisha kila mwaka katika "Siku ya Upendo wa kidugu, amesisitiza na kwamba wanazungumza kwa njia ya simu ili kuifanya upya kila mwaka, na ni siku inayofumbata roho ya Kikristo na upendo unaowaunganisha katika kumtumikia Mungu na kuwatumikia ndugu zao katika ubinadamu, ili waweze kutambua ndani yetu kile ambacho Yohana mpendwa alisema: “Wapenzi, na tupendane, kwa sababu pendo latoka kwa Mungu; kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu” (1 Yoh 4:7). Tumechagua upendo, hata tukienda kinyume na wimbi la ulimwengu wenye uchoyo na ubinafsi; tumekubali changamoto ya upendo ambayo Kristo anatuomba na tutakuwa wakristo wa kweli na ulimwengu utakuwa wa kibinadamu zaidi, kwa sababu ulimwengu wote utajua kwamba Mungu ni upendo na kwamba hili ndilo jina lake kuu zaidi”.

Wakati wa Baraka za mwisho
Wakati wa Baraka za mwisho

Tarehe hiyo pia amesema Patriaki kuwa inafanya  kumbukumbu ya miaka 50 ya Utakatifu wake Papa Shenouda III kwa kumtembelea Mtakatifu Papa Paulo wa Sita, na kuifanya kuwa muhimu zaidi na yenye ushawishi mkubwa kwa mahusiano kati ya Makanisa mawili.  Patriaki Tawadros amesema haweza kusahau kumshukuru Papa kwa furaha nyingi kwa ziara yake ya thamani nchini Misri mnamo mwaka wa 2017, ambayo ilikuwa baraka kubwa sana kwa Misri yote aliposema: “Hatuko peke yetu katika safari hii ya kusisimua ambayo, kama katika maisha, si rahisi na wazi kila wakati. Kwa njia hiyo Bwana anatusaidie  tusonge mbele na kuanzia sasa sisi ni mfano hai wa Yerusalemu wa mbinguni”. Hebu tutembee pamoja katika njia ya uzima, tukikumbuka kwamba “hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, uzima wa milele” (1Yoh 2:25), akitusindikiza na kututegemeza kwa maombi kulingana na ahadi hii.  Kwa hiyo licha ya tofauti za mizizi na mali zetu, tunaunganishwa na upendo wa Kristo anayekaa ndani yetu na jeshi la baba zetu, mitume na watakatifu wanatuzunguka na kutuongoza. Tumekujia kutoka Nchi ambayo Marko Mtume alihubiri, na Kiti chake kilianzishwa huko Aleksandria na kuwa moja ya sehemu za kale za kitume ulimwenguni, nchi ya Misri.

Katekesi ya Papa 10 Mei 2023
Katekesi ya Papa 10 Mei 2023

Patriaki Tawadros amesisitiza kuwa historia na ustaarabu husema kwamba ni mali ya asili: baba yake ni historia na mama yake ni jiografia. “Nimekuja kwako kutoka katika Kanisa la Coptic lililoanzishwa zamani kwa unabii katika kitabu cha nabii Isaya: “Siku hiyo kutakuwa na madhabahu katika nchi ya Misri na mnara mpakani mwake”. Ilitakaswa kwa kutembelewa na Familia Takatifu, iliyobariki dunia kutoka mashariki hadi magharibi, kutoka kaskazini hadi kusini. Misri: nchi ambayo utawa wa Kikristo ulienea na kujiimarisha pamoja na watakatifu wake Anthony, Macarius na Pachomius, ikitia moyo shule ya Alexandria, kinara wa taalimungu katika historia, ambayo ilikuwa na bado ni mahali patakatifu kwa maombi mbele za Mungu kwamba haijawekwa mikononi mwa Mungu tu bali pia moyoni mwake.

Papa akipokea zawadi
Papa akipokea zawadi

Kwa hiyo Patriaki Tawadros amesisitiza kuwa amesimama hapo mahali ambapo mtume Paulo na Petro walihubiri na amefurahi kukutana na Papa katika uwanja huo mzuri sana; Ametafakari safu hizi zinazounga mkono mahali hapo, akikumbuka ahadi ya Mungu kwa malaika wa Filadelfia: “Nitamweka mshindi kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka tena kamwe” (Ufu 3:12). Kwa hiyo amewaomba wate washike ahadi hiyo, ili tshinde uovu wa dunia, pamoja na udhaifu wake wote kama baba zetu walivyotufundisha, na kuishi sawasawa na wajibu tulionao, na kuishi kama manukato mazuri ya Kristo katika ulimwengu huu na kujikusanyia kwa amani yake. Katika ulimwengu huu tunatembea jinsi alivyotembea, na tuimbe pamoja na Daudi katika zaburi yake: “Uzishike hatua zangu katika njia zako, wala miguu yangu haitatikisika” (17:5), na tuombe kwa ajili ya ulimwengu wote amani ipitayo. kila akili, kuomba kwa sababu inafika kila mahali na kwa sababu ni kipaumbele cha viongozi na watu. Ninaomba pamoja nawe leo ili Mungu asikie maombi yetu. Asanteni nyote!

Wanandoa wapya wakimsalimia Papa baada ya katekesi
Wanandoa wapya wakimsalimia Papa baada ya katekesi
Papa na Tawadros kuadhimisha miaka 10 na pia 50 tangu Papa Paulo VI alipokutana na Shenouda III
10 May 2023, 16:26