Papa Francisk:Fuateni nyayo za Moyo wa Yesu unaomtafuta aliyepotea!
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Katika mzunguko wa tafakari ya Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 17 Januari 2023, katika mwendelezo wa mada ya shauku ya Uinjilishaji na bidii ya kitume, katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, kwa waamini na mahujaji waliofika ameanza kusema kuwa: “Jumatano iliyopita tulianza mzunguko wa katekesi kuhusu shauku ya uinjilishi, na juu ya bidii ya kitume inayopaswa kuhuisha Kanisa na kila Mkristo. Leo hii tunazama mtindo usiopitwa wa kutangaza Yesu. Injili ya Siku ya Noeli ilikuwa inamfafanua kama “Neno wa Mungu” (Yh 1,1). Kutokana na kwamba Yeye ni Neno ambaye anatuelekeza jambo msingi wa Yesu. Yeye daima yuko katika uhusiano, anatoka nje; kamwe hayuko peke yake, bali daima katika uhusiano wa kutoa neno, na kiukweli yuko kwa ajili ya kuenezwa na kutangazwa. Ndivyo alivyo Yesu, Neno la Milele la Baba aliyemwelekeza kwetu, na aliyetangazwa kwetu. Yesu si kwamba ana maneno ya uzima tu, lakini yeye anafanya maisha yake kuwa Neno. Anaishi, daima akiwa anaelekeza kwa Bwana na kuelekea kwetu. Tutazame daima Baba aliyemtuma na kujitazame sisi ambao Yeye alitumwa kwetu.
Baba Mtakatifu amesema ikiwa kiukweli tunatazama siku zake, zilivyoandikwa na Injili tunaona kwamba nafasi ya kwanza inaonesha maelewano ya kina na Baba, sala, kwa maana hiyo Yesu alikuwa anaamka mapema, bado kukiwa giza na kwenda katika eneo la jangwa kusali (Mk 1,35; Lk 4,42), na kuzungumza na Baba. Maamuzi yote na changuo zake muhimu alizifanya mara baada ya kusali(Lk 6,12; 9,18). Katika uhusiano huo, wa sala ambayo inamfunga kwa Baba katika Roho, Yesu anagundua maana ya kuwa mwanadamu, uwepo wake katika ulimwengu kwa sababu Yeye ni utume kwa ajili yetu aliyetumwa kwetu na Baba. Akiendelea Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa kutokana na mapendekezo hayo inafurahisha ishara ya kwanza ya umma ambayo Yeye alitimiza, baada ya miaka ya maisha yake akiwa mafichoni Nazareth. Yesu hakufanya maajabu makubwa, hakuzindua ujumbe wa upendo tu, lakini Yesu alijichanganya na watu ambao walikuwa wanakwenda kubatizwa na Yohane.
Kwa hiyo Yeye anatupatia ufunguo wa utendaji wake katika ulimwengu, wa kujua kukaa na wadhambi, kuwa na mshikamano na sisi bila kujiweka umbali, katika kushirikishana kwa ujumla maisha yote. Kiukweli kuzungumzia utume wake, yeye alisema kuwa “Hakuja kuhudumiwa, bali kuhudumia na kutoa maisha yake (Mk 10,45). Kila siku baada ya sala, Yesu alijikita siku yake nzima kwa kutangaza Ufalme wa Mungu na kwa watu, hasa kwa maskini zaidi, na wadhaifu, kwa wadhambi na kwa wagonjwa (Mk 1,32-39). Yaani Yesu anawasiliana na Baba katika sala na baadaye anawasiliana na watu wote katika utume, katika katekesi, ili kufundisha njia ya Ufalme wa Mungu.
Baba Mtakatifu aidha amebainisha kwa hiyo kwamba ikiwa tunataka kuwakilisha picha ya mtindo wake wa maisha, hatuna shida ya kumpata kwa sababu Yesu mwenyewe anatupatia mwenyewe wakati akizungumzia juu yake kuhusu “Mchungaji Mwema anayetoa maisha yake kwa kondoo zake” (Yh 10,11). Kwa hakika kufanya kazi ya mchungaji haikuwa kazi moja tu, lakini ambayo ilihitaji bidii kubwa; ilikuwa ni ya kweli na mtindo wa kuishi. Kwa masaa 24 ya kuishi na zizi; kusindikiza malishoni, kulala katikati ya kondoo na kuwasaidia wale walio wadhaifu zaidi. Yesu katika maneno mengine, hafanyi zaidi kwa ajili yetu, lakini anatoa maisha kwa ajili yetu. Yeye ana moyo wa kichungaji (Ez 34,15).
Kwa hiyo kwa kuwakilisha kwa neno moja katika matendo ya Kanisa, mara nyingi wanatumia neno hilo Mchungaji. Na kwa kuthaminisha uchungaji wetu lazima kujilinganisha na mtindo wa Yesu Mchungaji Mwema. Awali ya yote tunaweza kujiuliza: Je Tunamwiga kunywea katika kisima cha sala, ili moyo wetu uweze kufanana na wake? Kuwa na kina na Yeye ni kama alivyo kuwa akishauri Abate Chautard kwenye kitabu kizuri cha “Moyo wa kila mtume”. Yesu mwenyewe alisema wazi kwa wafuasi wake kwamba: “Bila mimi hamwezi kufanya kitu (Yh 15,5). Ikiwa utakaa na Yesu utakugundua kuwa moyo wake wa kichungaji unadunda daima kwa yule aliyeanguka, aliyepotea, na aliye mbali. Na je moyo wetu? “Ni mara ngapi mtazamo wetu unakuja, kwa kufikiria watu ambao ni wagumu kidogo au ambao inakuwa vigumu kidogo kwa upande wetu. Na mara ngapi tunasema “ni shida yake, na atajijua mwenyewe...” Lakini Yesu kamwe hakusema hivyo. Badala yake alikwenda kumtafuta. Pamoja na kila mtu, na wote waliotengwa, pamoja na wenye dhambi. Alishutumiwa kwa hilo la kuwa pamoja na wenye dhambi, kwa sababu alileta wokovu wa Mungu kwa wenye dhambi”, Papa amesisitiza.
Akirejea somo lililosomwa kuhusu kondoo aliyepotea, katika Injili ya Luka 15, 4-7)., Baba Mtakatifu amebainisha kwamba Yesu anazungumza hata katika sarafu iliyopotea na mtoto mpotevu. Kwa hiyo ikiwa tunataka kufanya zoezi: “Bidii ya kitume, Sura ya 15 inapaswa kuwa daima katika mtazamo wetu” ameshauri. Hapo tunagundua kuwa Mungu hachoki kutafakari zizi la kondoo zake na wala hatari ili wasiweze kuondoka. Badala yake ikiwa mmoja anatoka na kupotea, hamwachi kamwe, kwa sababu anakwenda kumtafuta. Na wala hasemi kwakuwa amekwenda, shauri yake, biashara zake! Kwani Moyo wa mchungaji unatenda kwa mtindo mwingine kwa sababu “unateseka na kujihatarisha”. Mungu anateseka kutokana na yule anayeondoka, na wakati analia, bado anaendelea kumpenda zaidi. Bwana anateseka wakati sisi tunakwenda mbali na moyo wake. Anateseka na wale ambao hawajuhi uzuri wa upendo wake na joto la mikono yake. Lakini katika jibu la mateso hayo, hajifungii, badala yake anathubutu. Kwa hiyo anaacha kondoo tisini na kenda, pia asiye na akili, anakwenda na moyo wake wa kichungaji, unaotamani sana wale ambao wamekwenda zao; sio hasira au chuki, lakini anazidi kuwa na lengo lisilo punguzwa kwetu. Ni bidii ya Mungu.
Baba Mtakatifu amejiuliza: Je sisi tuna hisia sawa? Huenda tukawaona wapinzani au maadui wale ambao wameacha zizi. Tunaanza kusema “Na hiyo? Hapana kwakuw amekwenda mahali pengine, amepoteza imani, na kuzimu inamngoja ...”, na wakati huo sisi tunakuwa watulivu. Kinyume chake Papa ameshauri kwamba kukutana nao shuleni, kazini, katika barabara za jiji, kwa nini tusifikiri kuwa tuna fursa nzuri ya kushuhudia furaha ya Baba anayewapenda na ambaye hajawasahau kamwe? Hii si kushabikia imani, hapana! Lakini ni kuwaomba kuwa Neno la Baba liwafikie, ili watembea pamoja naye. Kueneza Injili si kugeuza watu imani. Kuwalazimisha watu ni jambo la kipagani, si la kidini au la kiinjili.
Kuna neno zuri kwao na kulipendekeza kwao, tuna heshima na jukumu letu la kuwambia neno hilo. Kwa sababu Neno, Yesu, anatuomba hilo, kila mara tumwendee kila mtu, kwa moyo ulio wazi, kwa sababu Yeye yuko hivyo. Labda tumekuwa tukimfuata na kumpenda Yesu kwa muda mrefu na hatujawahi kujiuliza ikiwa tunashiriki hisia zake, ikiwa tunateseka na kuhatarisha kupatana na moyo wa Yesu, kwa moyo huo wa kichungaji, karibu na moyo wa kichungaji wa Yesu! Si suala la kuwafanya watu waongoke, kama alivyokuwa amesema mwanzo na ili wengine wawe pamoja nasi, hapana, hili si la Kikristo, bali kitu muhimu ni lile suala la kupenda ili wawe watoto wa Mungu na wenye furaha.
Baba Mtakatifu amewasihi kusali kwa ajili ya neema ya moyo wa kichungaji, ulio wazi, wa kuwa karibu na kila mtu, kumpelekea ujumbe wa Bwana na pia kuhisi wao katika Kristo. Kwa sababu, bila upendo huo unaoteseka na kujihatarisha, maisha yetu hayaendi vizuri. Na ikiwa sisi Wakristo hatuna upendo huo unaoteseka na kujihatarisha, kuna hatari ya kujivua sisi wenyewe tu. Na kuwa Wachungaji ambao wanajichunga wao wenyewe na ambao, badala ya kuwa wachungaji wa zizi ni wachungaji wa walio bora yaani wanaojichunga wao wenyewe… kinyume chake wote wanapaswa kuwa Wachungaji wa wote, amehitimisha Papa Francisko takafakri kuhusu mtindo usiopitwa wa kumtangaza Yesu.