Papa:Hatuwezi kurudisha nafasi ya uzuri wa uumbaji ulioumbwa na sisi!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko amekutana na washiriki wa Kongamano la Kimataifa kuhusu kulinda bayoanuai,Jumamosi tarehe 21 Mei 2022 katika ukumbi wa Clementina katika Jumba la Kitume Vatican. Papa amesema inahitajika utamaduni wa utunzaji, ambao ni utamaduni wa maelewano, yaani wa kuhifadhi maelewano, kuhamasisha mazungumzo kati ya maarifa na kukuza elimu jumuishi yenye nguzo za ikolojia fungamani na inayolenga uhusiano kati ya mwanadamu na mazingira. Hili ndilo wazo kuu kwa hakika la Papa Francisko kwa washiriki Kongamano hilo kuhusu kulinda bayoanuai, ambalo limeongozwa na mada:“asili katika akili. Utamaduni mpya wa asili kwa ajili ya ulinzi wa viumbe hai”, lililoandaliwa na Kitengo cha Polisi.
Papa Francisko katika hilo amewapa maelekezo ya kufuata ili kulinda nyumba ya pamoja. “Ili kuweza kuhamasisha maendeleo endelevu, ni muhimu kufungua na ubunifu kwa ratiba mpya, zilizounganishwa zaidi, zinazoshirikishwa, zinazohusiana moja kwa moja na watu na mazingira yao. Kwa njia hiyo kila mtu anahisi kuhusika katika kuchangia mkataba wa elimu, ambao huwa na kuunda watu waliokomaa, wenye uwezo wa kushinda kugawanyika na tofauti.”
Kwa upande wa Papa, “hatua yoyote haitakuwa na ufanisi ikiwa haitasaidiwa na kuungwa mkono na mchakato wa elimu unaopendelea utunzaji na ulinzi wa nyumba ya pamoja, hasa kwa kupitia vipaji vyetu sisi sote tunaitwa kujenga kijiji cha utunzaji wa kimataifa, kuunda mtandao wa mahusiano ya kibinadamu ambayo yanakataa aina zote za ubaguzi, vurugu na unyanyasaji. Katika kijiji chetu hiki, elimu inakuwa mtoaji wa udugu na kuzaa amani kati ya watu na pia mazungumzo kati ya dini”.
Katika hotuba yake, Papa Francisko pia amekumbuka mada ya Kikosi cha Polisi yenye lengo la kuimarisha mazungumzo ya haraka na mazungumzo ya uwajibikaji juu ya mustakabali wa sayari, kwa sababu changamoto ya mazingira na mizizi yake ya kibinadamu inahusu kila mtu. Papa amebainishwa kwamba Kongamano na mpango mingine ambayo huonesha nia ya kushirikiana kulinda nyumba yetu ya pamoja ambayo inatufanya tufikirie ratiba ya safari ya Mtakatifu Buonaventura wa Bagnoregio", ambaye mara kadhaa anatualika kugundua yale yanayopita maumbile pia kupitia tafakari ya uzuri wa asili”. Zawadi kutoka kwa Mungu kwa wanadamu, iliyoitwa kuilima na kuilinda. “Uzuri wa pamoja katika kile ni kifungo chenye uhusiano kati ya Muumba, kiumbe cha binadamu na viumbe vingine, ni muungano ambao hatupaswi kujidanganya kuweza kuchukua nafasi ya uzuri usioweza kurudiwa na usioweza kurejeshwa na mwingine ulioumbwa na sisi”.
Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba kuna haja ya udugu wa upole na uvumilivu kati yetu na viumbe, kwa sababu maisha na historia inaonesha kwamba hatuwezi kuwa sisi wenyewe bila wengine, kwa maana kila kitu kinahusiana sana. Hatimaye, Papa Fransisko ametoa shukrani zake kwa Polisi kwa kujitolea kwao kila siku na kuwataka kuendelea na ujasiri huo.