Kila tarehe 3 Desemba ni siku ya Kimataifa ya walemavu. Kila tarehe 3 Desemba ni siku ya Kimataifa ya walemavu. 

Papa Francisko,Ujumbe wa Siku ya Walemavu Kimataifa:'Ninyi ni rafiki'

Katika fursa ya Siku ya walemavu ulimwengu ifanyikayo kila mwaka tarehe 3 Desemba,Papa Francisko ameandika ujumbe wake na ambaye anatambua ubaguzi ulopo mwingi katika jamii na hukumu lakini amesema ni vema kupata huduma bora na kwamba janga la uviko-19 limeangazia udhaifu wa wengi.Urafiki na Yesu unaweza kuwa ufunguo wa kiroho kukubali vizingiti vya haki za kila mtu.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya Watu Walemavu duniani ifanyikayo kila mwaka tarehe 3 Desemba, Papa Francisko ameandika ujumbe wake  unaoongozwa na kauli mbiu: “Ninyi ni marafiki”(Yh 15,14). Kwa maana hiyo siku hiyo amependa kuwaelekeza moja kwa moja wote ambao wanaishi katika kila hali ya ulemavu ili kuwaambia  kuwa Kanisa linawapenda na linawahitaji kila mmoja wao ili kutumiza utume wake katika huduma ya Injili. Yesu ni rafiki yetu! Ni yeye mwenyewe aliwambia mitume wake wakati wa Karamu ya mwisho (Yh 15,14). Maneno yake yanafika hadi kwetu na kuangazia huduma yetu ya kuwa na uhusiano na Yeye na katika uwepo wa Kanisa. Urafiki na Yesu hautenganishwi. Yeye hatuachi kamwe hata ikiwa wakati mwingine utafikiri yuko kimya. Tunapokuwa na haja naye, anapatikana na yuko karibu yetu kila mahali tuendako. (Wosia wa Christus vivit, 154). Sisi kama Wakristo tulipokea zawadi katika moyo wa Yesu na urafiki ya Yeye. Ni fursa kubwa ambayo tuliipata inayotusindikiza na ambayo inageuka kuwa wito wetu kuwa marafiki zake. Kuwa na Yesu kama rafiki ni faraja kubwa na inawezekana kufanya kwa kila mmoja wetu, kuwa mfuasi wa shukrani, furaha na mwenye uwezo wa kushuhudia kwa udhaifu binafsi ambao sio kizingiti cha kuishi na kuwasiliana na Injili. Urafiki wa imani na binafsi na Yesu unaweza kuwa ufunguo wa kiroho ili kukubali vizingiti ambavyo wote tunafanya uzoefu na kushi kwa namna ya upatanisho binafsi wa hali halisi. Na unaweza kuzaa furaha ambayo inajaza moyo na maisha yote(wosia Evangelium gaudium 1) kwa sababu kama alivyo andika mfasiri wa maandiko kuwa urafiki na Yesu ni cheche ambazo zinawasha shauku”.

UJUMBE WA PAPA WA SIKU YA WALEMAVU KIMATAIFA

Kanisa ni nyumba yetu: Ubatizo unamfanya kila mjumbe kuwa na jina kamili la jumuiya ya kikanisa na kutoa kwa kila mmoja bila kubaguliwa na wala kutengwa, uwezekano wa kutamka kuwa “mimi ni Kanisa”, amesisitiza Papa.  “Kanisa kwa hakika ni nyumba yenu na sisi sote kwa pamoja ni kanisa kwa sababu Yesu alichagua kuwa rafiki yetu. Ndani mwake tunataka kujifunza daima kuwa bora katika mchakato wa kisinodi ambao umeanza hivi karibuni, hata kama sisi sio jumuiya timilifu lakini ya wafuasi walio katika safari ambapo wanafuata Bwana, wenye kuhitaji msamaha wake” (Katekesi 13,Aprili 2016).  Katika watu ambao kati ya matukio ya historia kwa kuongozwa na Neno la Mungu, Papa anasema wote wako mstari wa mbele na hakuna anayeweza kujifikiria amepotea (Hotuba kwa waamini Roma 18 Septemba 2021). “Kwa maana hiyo kila mmoja wenu amealikwa kutoa mchango wake katika mchakato wa kisinodi”. Papa Fancisko anaamini kuwa ndani mwake utakuwa kweli mchakato wa kikanisa, ulioshiriki na kushirikishwa, jumuiya ya kikanisa itatoka ndani humo ikiwa kweli imetajirika. Hata hivyo Papa amebainisha kuwa kwa bahati mbaya bado lakini leo hii walemavu walio wengi wao wanahudumiwa kama miili ya kigeni katika jamii,(…) na wananahisi kuishi bila uwepo na wala kushiriki na kuna bado mambo mengi ambayo yanawazuia kuwa wazalendo kamili (Ft 98). Ubaguzi  huo bado upo mwingi kwa ngazi mbali mbali za maisha ya kijamii.

Huo unakuzwa na hukumu, ujinga na utamaduni ambao unageuka kuwa mgumu kuelewa thamani ya kila mtu. Kwa namna ya pekee, kwa kuzingatia bado ulemavu ambao ni matokeo ya mwingiliano kati ya vizingiti vya kijamii na mipaka ya kila mmoja  Papa amesema utafikiri ni ugonjwa, ambao unachangia kutenga maisha yao na kuweka chachu ya utelekezwaji wao. Kile ambacho kinaonekana katika Maisha ya Kanisa, ubaguzi mbaya (…) ni ukosefu wa umakini kiroho (EG. 200) ,ambapo wakati mwingine umejionesha hasa katika kukaribia Sakramenti, na kwa bahati mbaya  wao wamefanya uzoefu. Mafundisho ya Kanisa yanaeleza wazi kuhusiana na hilo Papa amesisitiza na kwamba  hivi karibuni katika Melekezo ya Katekisimu ya Kanisa imethibitishwa  wazi kuwa hakuna yeyoye anaweza kukataliwa kupata Sakramenti kwa watu wenye ulemavu (n. 222). Mbele ya ubaguzi urafiki wa Yesu ambao sisi sote tunapokea katika zawadi yake, ambayo alitukomboa na unaturuhusu kuishi na kuona tofauti kama utajiri. Yeye kwa hakika hatuiti kamwe watumishi, wanawake na wanaume wa hadhi iliyo nusu, lakini anatuita marafiki.  “Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.( Yh 15,15).

Kipindi cha majaribu kutokana na janga: Urafiki na Yesu utatulinda katika wakati wa majaribu. Papa anatambua vema, jinsi ambavyo janga la UVIKO-19, ambalo bado linakuwa vigumu kuondokana nalo sasa, umeleta na unaendelea kuleta majaribu makubwa katika maisha ya walio wengi hasa wao. Papa amekumbusha kwa mfano ulazima wa kukaa kwa muda mrefu nyumbani; matatizo ya wanafunzi wengi wenye ulemavu kufikia zana za mafunzo yao wakiwa mbali na huduma za watu ambao kwa nchi nyingi zilikatishwa; na walio wengi wao walipata shida kweli kukabiliana nazo. Lakini Papa hasa amefikiria wale ambao wanaishi na wao ndani ya majengo ya kutunza na mateso ambayo yaliwafikisha hata kuwapo utengano wa kuwaona ndugu zao wapendwa. Katika maeneo hayo virusi vilikuwa vya nguvu licha ya watu kujitoa sana lakini waathirika walikuwa wengi. Papa amesema lazima watambue kuwa Papa na Kanisa walikuwa kariibu kwa njia ya pekee kwa upendo na upole.

Injili ni kwa wote: Kanisa liko katibu na wale ambao wako pamoja nao na wanaendelea kupambana dhidi ya Virusi vya Uviko. Papa amesema kama ilivyo janga la virusi linataka kutuonesha kwamba kuna ulazima ambao tunapaswa kutunzana kila mmoja,  bila ya kuona hali ya ulemavu kama kizingiti cha kuweza kupata tiba bora inayowezekana. Kwa maana hiyo Papa ametoa mfano kuwa  tayari mabaraza ya maaskofu kama yale ya Uingereza na Walles na ya  Marekani wameingilia kati kuomba kuheshimiwa haki za wote katika utunzaji bila ubaguzi. Kutokana na urafiki wa Bwana ndipo unatokea wito wetu. Papa amesisitiza kuwa “Yeye alituchagua sisi; akatuweka ili tukazae matunda; na matunda yetu yapate kudumu (taz Yh 15,16).” Kwa kujiwakilisha kama mzabibu wa kweli alipenda kila mmoja awe tawi, lililounganishwa na Yesu kwa namna ya kutoa matunda. Yesu ndiyo anapenda tufikie furaha ambayo tumeumbwa kwa ajili hiyo. Yeye anatutaka tuwe watakatifu  na si kusubiri kuwa tunafurahia maisha ya unafiki, yaliyo na maana na ambayo hayapo. (Gaudet et Exultate 1).

Injili pia ni yako! Papa amesisitiza kwani amesema ni Neno linalomhusu kila mmoja, ambalo linalotoa faraja na wakati huo huo linaalika kuwa na uongofu. Mtaguso wa II wa Vatican, unazungumza kuwa: Bwana Yesu, aliye mwalimu na mfano wa kimungu wa ukamilifu wote, aliwahubiria wanafunzi wake wote na kila mmoja peke yake wenye hali yoyote, utakatifu wa maisha ambao Yeye mwenyewe ndiye mwanzishaji na mtimilizaji wake: “Ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu” (Mt 5:48. Akawapelekea wote Roho Mtakatifu ili awasukume kwa ndani kumpenda Mungu kwa moyo wote, kwa roho yote, kwa ufahamu wote, na kwa nguvu zote (Mk 12:30), na kupendana kama vile Kristo alivyowapenda”.  Hii nii dhahiri kwa wote kwamba waamini wote wakristo wa hali yoyote au daraja lolote huitwa kufikia utimilifu wa maisha ya kikristo na ukamilifu wa upendo; kwa utakatifu huu huhamasishwa kiwango cha maisha kiwafaacho zaidi wanadamu, hata katika jamii ya kidunia. Kwa lengo la kuufikia ukamilifu huo waamini watumie nguvu walizopata kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo, ili wakifuata nyayo zake na kufananishwa na mfano wake, wakiyatii mapenzi ya Baba katika mambo yote, wajitoe kwa moyo wote kwa ajili ya utukufu wa Mungu na huduma ya jirani.(LG 40)

Papa Francisko ameongeza kwamba vitabu vya Injili vinatuambia kwamba watu fulani wenye ulemavu walipokutana na Yesu, maisha yao yalibadilika sana na wakaanza kuwa mashuhuda wake. Hii ndiyo kesi, kwa mfano, ya mtu kipofu tangu kuzaliwa ambaye, aliponywa na Yesu, anathibitisha kwa ujasiri mbele ya kila mtu kwamba yeye ni nabii (Yn 9:17); na wengine wengi wanatangaza kwa furaha kile ambacho Bwana amewafanyia. “Ninajua kuwa baadhi yenu wanaishi katika hali tete sana”. Papa hata hivyo amependa kuwageukia wao hasa, labda kwa kuwauliza mahali  ambapo kuna ulazima wa  wanafamilia wao au wale walio karibu nao kusoma maneno yake haya au kuwasilisha wito wake na kuwaomba wasali. “Bwana husikiliza kwa makini maombi ya wale wanaomtumaini. Mtu awaye yote asiseme: “Sijui kuomba” kwa sababu, kama vile Mtume asemavyo, “Roho huja kutusaidia udhaifu wetu; kiukweli hatujui kuomba ipasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa” (Warumi 8:26).

Kwa hakika, katika Injili, Yesu huwasikiliza wale wanaomgeukia hata kwa njia isiyofaa, labda tu kwa ishar a(Lk 8:44) au kilio (Mk 10,46). Katika maombi kuna utume unaofikiwa na kila mtu na Papa amependa  kuukabidhi kwa namna ya pekee. “Hakuna aliye dhaifu kiasi cha kutoweza kuomba, kumwabudu Bwana, kulitukuza jina lake takatifu na kuombea wokovu wa ulimwengu. Mbele ya Mwenyezi, sote tunajikuta tuko sawa. Wapendwa kaka na dada, maombi yao leo hii ni ya dharura zaidi kuliko hapo awali.  Mtakatifu Teresa wa Avila aliandika kwamba “katika nyakati ngumu marafiki wenye nguvu wa Mungu wanahitajika ili kusaidia walio dhaifu”. Wakati wa janga hili umetuonesha wazi kuwa hali ya mazingira magumu inatuunganisha sisi sote: “Tuligundua kuwa tuko kwenye mtumbwi mmoja, sote tukiwa dhaifu na tumechanganyikiwa, lakini wakati huo huo muhimu wote tumemeitwa kupiga makasia pamoja. Njia ya kwanza ya kufanya hivyo ni kuomba. Sote tunaweza kuifanya;na hata kama, tutakuwa  kama Musa, tunahitaji kuungwa mkono (rej. Kut 17:10), tuna hakika kwamba Bwana atasikiliza maombi yetu. Amewatakia kila baraka na Mama Maria awalinde.

25 November 2021, 17:40