Mtoto amekaa karibu na Papa na limekuwa somo la kutoka moyoni

Nje ya mpango kamili wa katekesi ya Papa umeonesha na Mtoto wa miaka kumi aliyekwenda moja kwa moja kwa Papa Francisko na yeye akamkaribisha ili akae karibu na kiti cha msimamizo wa masomo wa nyumba ya kipapa Monsinyo Leonardo Sapienza:Papa amesema mtoto huyo anaonesha ujasiri na uhuru wa moyo wa wadogo wanavyo mkaribia Bwana.

Na Sr. Angelaa Rwezaula - Vatican

Jumatato tarehe 20 Oktoba 2021  wakati msomaji wa lugha ya kijerumani akiendelea kusoma somo kwa Wagalatia katikati ya Katekesi ya Papa, mtoto mmoja mdogo alipanda kwa utulivu kwenye ngazi za Ukumbi wa Paulo VI. Ni mwenye umri wa miaka 10 hivi mwenye upungufu wa akili, ambaye amekuja Roma na familia yake kutoka Mtakatifu Ferdinando wa Puglia Italia na baadaye alikweda moja kwa moja kwenye kiti cha Papa. Papa alikuwa akitamzama kwa tabasamu wakati wa kupanda ngazi. Alipomkaribia walisalimiana na kumbembeleza. Kati ya mshangao wa waaamini waliolikuwa katika ukumbi huo, wakati wanaendelea na usomaji wa barua ya Mtakatifu Paulo katika lugha mbali mbali. Papa amezungumza naye maneno na kumuuliza kama alitaka kukaa naye karibu. Baadaye kwa haraka Monsinyo Leonardo Sapienza, Msimamizi wa masomo kwa upande wa Urais wa Nyumba ya Kipapa ameamka na kumwachia kiti mtoto.

Mtoto akisalimiana na Papa baada ya kupanda ngazi
Mtoto akisalimiana na Papa baada ya kupanda ngazi

Makofi yalipigwa kwa haraka na wakati huo mtoto huyo Paulo jr. alianza naye kupiga makofi huku akitabasamu chini cha barakoa yake. Baadaye alitazama na kuamka tena akarudi kwa Papa ambaye alimshika mikono huku akiruka ruka. Papa alimwamnia tena maneno lakini Paulo akaenda nyuma ya kiti cha Papa mahali ambao wakati huo walikuwa wameleta kiti cha Monsinyo Sapienza.  Mtoto aliomba mkuu kikofia cha Baba Mtakatifu huku akimwonesha na kidole. Watu waliendelea kipiga makofi kwa sababu mtoto aliendelea kutoa sauti ya kuomba kile kikofia cheupe cha Papa, kwa hakika ilikuwa nje ya mpango wa katekesi. Mtoto huyo baada ya kumkumbatia Papa, alisindikizwa tena kwenye nafasi yake na mama yake aliyekuwa amepanda ngazi wakati huo kumchukua.

Mtoto akiwa anataka kikofia cheupe cha Papa
Mtoto akiwa anataka kikofia cheupe cha Papa
Mtoto akiwa na mama yake anamuaga Papa
Mtoto akiwa na mama yake anamuaga Papa

Papa kabla ya kuanza katekesi yake alianza kusimulia tukio hilo la mtoto  na kusema kwamba siku hiyo wanazungumzia juu ya uhuru wa imani, kwa kusikiliza barua ya kwa Wagalatia. Lakini kinachomjia kwenye akili ni kile ambacho Yesu alikuwa anasema kuhusu uhuru wa watoto wakati mtoto alipoweza kuwa na uhuru wa kukamribia na kuanza kuzunguka utafikiri yuko nyumbani kwao… Na Yesu alikuwa anasema:“ ikiwa hamtageuka kuwa kama  watoto, hamtaingia katika Ufalme wa Mbingu”. "Huo ni ujasiri wa kumkaribia Bwana;  kuwa wazi kwa Bwana na  bila kuwa na hofu ya Bwana. Mimi ninamshukuru mtoto kwa kutupatia somo hili kwa wote. Na Bwana amsaidie katika kumwiga na kukua kwake kwa sababu ametupatia ushuhuda ambao umetoka moyoni mwake. Watoto hawana mkarimani wa haraka bali unatoka rohoni  mwao na wanakwenda mbele".

Mtoto huyo kutoka Puglia sio wa kwanza katika matukio kama haya, kuwa nje ya mpango wa siku ya Papa Francisko. Ni mara nyingi wakati uliopita hasa wakati wa katekesi zake  kama hizo, watoto wengi sana ambao wamekuwa wakimkaribia au yeye mwenyewe kuwafanya wakae karibu naye moja kwa moja katika kiti chake, iwe kwenye ukumbi huo au katika uwanja wa Mtakatifu Petro na ambao mara nyingi yeye aliwakaribisha kukaa nao katika gari la kuzunguka katikati ya waamini na mahujaji.

 

20 October 2021, 16:45