Papa Francisko akiadhimisha ndoa ya Letícia Schafer (mbrasiliani) na Luca (Mswiss) tarehe 18/07/2018. Papa Francisko akiadhimisha ndoa ya Letícia Schafer (mbrasiliani) na Luca (Mswiss) tarehe 18/07/2018. 

Papa:ujumbe kwa washiriki wa Hija ya familia:Wajibu ni kushirikisha na kuunganisha!

Papa Francisko amewatumia ujumbe washiriki wa Hija ya 14 ya familia kwa ajili ya familia ambayo inafanyika Septemba 11,katika madhabahu 19 ya mikoa ya Italia:”ninyi ni sura angavu ya imani katika wakati mgumu wa amateso”.Anawaalika kusali kwa ajili ya mkutano wa familia utakaofanyika Roma 2022.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika mkesha wa Ziara wa Papa Francisko ya kwenda nchini Hungaria katika jiji la Budapest na Slovakia ikayo, Jumamosi tarehe 11 Septemba 2021, Papa ametuma ujumbe wake kwa ajili ya washiriki wa Hija ya 14 ya Familia kwa Familia. Familia ni hai ikiwa imeungana katika maombi. Ni yenye  nguvu, inapogundua tena Neno la Mungu. Ni karimu, ikiwa inaendelea kuwa wazi kwa ajili ya  maisha, haibagui na inahudumia wahitaji zaidi. Katika ufupisho huo Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake amewalenga wanandoa, wazazi, babu na nyanya, watoto, wajukuu, ambao wanashiriki Hija hiyo iliyoanza kwa hakiak Jumamosi tarehe 11 Septemba 2021. Wakati wa maombi ya kitaifa, yaliyohamasishwa na Harakati ya uhuisho wa Roho, Baraza la Maskofu maaskofu Italia (CEI) na vyama vya kifamilia, ambavyo vinajikita na hija hiyo kwa njia ya mtandao, na kujumuisha maelfu ya familia kutoka Italia yote  katika maeneo 20 ya madhabahu  katika mikoa 19.

Injili ya familia

Kwa mujibu wa ujumbe wa Papa ni shukrani kubwa ya ushuhuda wa muungano na furaha ambayo inatafsiri kilio kilichozinduliwa kwa umoja yaani cha "Familia ni hai!  Vile vile anatoa shukrani kwa juhudi hii ya kuwafikia watu wengi iwezekanavyo kama ishara hai ya amoris laetitia  yaani furaha ya upendo ndani ya familia inayotokana na Injili ya familia. Familia zilizohusika katika hija zinaonesha sura nzuri ya imani kwa Yesu Kristo, katika kipindi kilichopondeka na shida nyingi, mateso na maovu mapya, kwa mujibu wa Papa Francisko. Kwa maana hiyo Papa anatilia mkazo kwa kaulimbiu iliyochaguliwa kwa mpango huu: "Katika umoja  ... furaha! kwamba chaguo ambalo limechaguliwa linarudia kutoa mwaliko wa kutafuta sio utumiaji na furaha binafsi, ambayo inausumbua moyo tu, badala yake ni ile furaha inayoishi katika muungano, ambayo inashirikishwa na kuunganishwa, kwa sababu ni heri kutoa kuliko kupokea.Kwa hakika upendo wa kindugu huzidisha uwezo wetu wa furaha, kwani unatuwezesha kufurahiya mema ya wengine, anasema Papa Francisko katika ujumbe huo. “Familia ni  hai" ikiwa itajikuta imeungana pamoja katika maombi. Familia ina nguvu ikiwa itagundua tena Neno la Mungu na thamani ya uongozi wa ahadi zake zote. Familia ni ya ukarimu na inaunda historia ikiwa inabaki wazi kwa ajili ya maisha, ikiwa haibagui na inahudumia mdhaifu na mhitaji, na kumpatia mkate wa upendo na divai ya udugu ” wa Ulimwengu.

Mkutano wa Familia Ulimwenguni jijini Roma

Papa Francisko akiendelea na roho hiyo hiyo amewakumbusha kujiandaa kwa ajili ya Mkutano wa X wa Familia utakaofanyika jijini Roma tangu tarehe 22 hadi 26 Juni 2022, na wakati huo huo pia katika jumuiya za majimbo ulimwenguni kote. Hii inatakiwa kufanya maandalizi ya dhati ambayo ni ya kiroho. Kwa sababu hiyo katika ujumbe wake Papa ametoa sala rasimi ya Mkutano wa Familia jijini Roma akiwaalika kusali kuanzia sasa.

Sala ya kuombea mkutano wa Familia 2022

Baba Mtakatifu, tuko hapa mbele yako, kukusifu na kukushukuru kwa zawadi kubwa ya familia. Tunaombea familia zilizowekwa wakfu katika sakramenti ya ndoa, ili waweze kugundua tena neema inayopokelewa kila siku na, kama Makanisa madogo ya nyumbani, wanajua jinsi ya kutoa ushuhuda kwa Uwepo wako na upendo ambao Kristo anapenda Kanisa. Tunawaombea familia zinazopitiwa shida na mateso, magonjwa, au shida ambazo wewe peke yako unajua: ziunge mkono na uwafahamishe njia ya utakaso ambayo unawaita, ili waweze kupata huruma Yako isiyo na kikomo na kupata njia mpya ili kukua katika upendo.

Tunawaombea watoto na vijana, ili waweze kukutana nawe na kujibu kwa furaha wito uliowafikiria; kwa ajili ya wazazi na babu na nyanya, ili wapate kujua kuwa wao ni ishara ya baba na mama wa Mungu katika utunzaji wa watoto, mwilini na rohoni, Wewe unawakabidhi; kwa uzoefu wa udugu ambao familia inaweza kutoa kwa ulimwengu. Bwana, ruhusu kila familia iweze kuishi wito wake kwa utakatifu katika Kanisa kama wito wa kuwa mhusika mkuu wa uinjilishaji, katika huduma ya maisha na amani, kwa ushirikiano na makuhani na kila hali ya maisha. Ubariki Mkutano wa Familia Ulimwenguni.

 

11 September 2021, 14:15